Rais tunayemtaka 2015 - je ni sawa au?

Rais tunayemtaka 2015 - je ni sawa au?

John mnyika ndo rais wangu wa wakati huo kwa sasa akichemka hata kura simpi pia.

mamndenyi mh Mnyika ni kiongozi ambae ajawahi kutokea katika karne ya ivi karibuni na kamwe jj hawezi kuchemka ata kidogo.
 
Nimesema tatizo si ulevi kwani wote wamelewa; hakuna msafi hata mmoja si upinzani wala watawala wote ni walewale tu waganga njaa na wakipata fursa tutaona rangi zao vizuri hakuna msafi hata mmoja. Tunachohitaji ni kubadili mfumo wa kutawalana tutenge ulaji mbali na uongozi mbali

Kwa kumbukumbu yangu, Mwl. Nyerere alikuwa hapendi kabisa mtumishi wa Umma au Kiongozi wa chama kuwa mfanyabiashara, alijua wazi kuwa matokeo yake ndo hayo, sasa ndani ya CCM ni yupi ambaye si mfanyabiashara, si mwizi, si fisadi? kwa namna hiyo kiongozi wa kweli wa kubadilisha mwelekeo uliopo atatokaje ccm?
 
mbna Mwigulu hajatajwa humu..?

Mwigulu hana sifa kwa sababu kauli zake zinaligawa taifa sawa na wenzie akina Nape kwa mfano Nape hana sifa kwa ajli ya domo lake chafu hilo domo lake ndilo linakimbiza makada wa CCM kwa maelfu. mtu kama Rage hana sifa ni kwapu kwapu sana tena tapeli pia laghai'
 
kama tunahitaji rais nadhani swala la ujana,uzee,ummee,ukee halina maana.Tunahitaji rais mtendaji,msafi kwa matendo,asiyemrahisi wa kurubuniwa na anatakiwa asiwe kwenye corrupt system.Kwa maoni yangu,dr.Slaa,mh.Myika na mh.Tundu Lissu wanaweza kutuvusha.Mh.Makamba pia anaweza kumudu bila kumsahau dr.Mwakyembe ila kikwazo chao ni chama,yaani system ndani ya chama chao itawagharimu mda mrefu saana ili kuweka mambo sawa
 
kama tunahitaji rais nadhani swala la ujana,uzee,ummee,ukee halina maana.Tunahitaji rais mtendaji,msafi kwa matendo,asiyemrahisi wa kurubuniwa na anatakiwa asiwe kwenye corrupt system.Kwa maoni yangu,dr.Slaa,mh.Myika na mh.Tundu Lissu wanaweza kutuvusha.Mh.Makamba pia anaweza kumudu bila kumsahau dr.Mwakyembe ila kikwazo chao ni chama,yaani system ndani ya chama chao itawagharimu mda mrefu saana ili kuweka mambo sawa
Uko sawa kabisa!
 
Mimi bado nina imani kubwa kwa DR SLAA, sidanganyiki wala sibadilishi imani yangu.

Zitto namkubali sina tatizo juu ya uwezo wake ila nakwazwa na ile single yake ya "niwataje au nisiwataje" kutuonesha kwamba ana nidhamu ya uoga ktk kuwakabili watu wenye nguvu kubwa kipesa, hivyo hata akiwa Rais atashindwa kuwachukulia hatua wafanyabiashara wa dawa za kulevya, kama kuwataja tu walioficha pesa uswiz ameshindwa.

haya ndio maneno, huyo Tutor B nadhani ni mmoja kati ya walioanzisha ile ngo ya kamati/umoja wa vijana ila wagangie njaa ..
 
Last edited by a moderator:
ujazba wake unaujuaje kama sio ujuha jingalishi mkubwa wewe

Hv nyie vjana wa Chadema mna akili kweli au Mmelogwa? Hv toka lini Binadamu alieshndwa kumuogopa,kumheshmu na Kum2mikia Mungu/Muumba wake.., itakuaje ukja Mpa Urais ili aku2mikie Mwanadam mwenzanke? So cna shaka kua Dr Slaa hana sifa za kua Rais wa nchi hii hata kdogo period
 
Kwa kumbukumbu yangu, Mwl. Nyerere alikuwa hapendi kabisa mtumishi wa Umma au Kiongozi wa chama kuwa mfanyabiashara, alijua wazi kuwa matokeo yake ndo hayo, sasa ndani ya CCM ni yupi ambaye si mfanyabiashara, si mwizi, si fisadi? kwa namna hiyo kiongozi wa kweli wa kubadilisha mwelekeo uliopo atatokaje ccm?
Sio biashara tu hata nyumba ya kupangisha kiongozi hakutakiwa kuwa nayo unataka kuniambia leo hii ni kiongozi gani wa upinzani hana biashara? kama sio fisadi anakwepa kodi hakuna biashara katika nchi hii inayoweza kuzalisha faida bila kukwepa kodi kutokana na mlolongo wa kodi zisizo na kichwa wala miguu; sasa hapo nani msafi unamtuhumu mwenzio kwa ufisadi lakini unakwepa kodi au unaibia watu kupitia mzani au kuuza vitu vilivyoisha mda huko kwenye unga ndio usiseme kabisa hakuna cha upinzani wala askofu wala shehe wala waziri. Hakuna aliye msafi ishu ni kuanza upya na miiko mipya ya uongozi nyani haonagi kundule ndio maana mnaona viongozi wa upinzani ni wasafi madudu yao yakianikwa hapa mtakimbia watu wameyaweka tu kama rungu la mwisho. Usisahau ni Nyerere huyo huyo aliyesema upinzani wa kweli utatoka ccm kwa maneno mengine upinzani hautaingia Ikulu mpaka baadhi ya ccm watimkie huko na haohao ndio watakaokuja kwenye uongozi wa nchi; utabiri huu unakuwa kweli kila uchao na ccm haiondoki madarakani isipofarakana na hata wakifarakana ni hao hao watakaoongoza nchi wakitokea upinzani au ugombea binafsi. Mimi sijaona kiongozi bado upande wa upinzani tuna matatizo mangapi na wamefanya nini kuleta nafuu zaidi ya makelele na vurugu huwezi kuwa mzuri kwa kuwa m-baya.
 
sifa za rais ajae---2015.
Watanzania changamkieni kutoa ushauri kwenye rasimu ya katiba mpya ili iwe yenye faida kwa wote isinufaishe kikundi fulani kama ya hivi sasa inavyowanufaisha chama tawala cha ccm. Katiba mpya iendane na malekebisho makubwa katika taasisi ya urais, bila kufanya marekebisho katika taasisi hii basi hata katiba mpya itakuwa ni bure kabisa kwa maana haitakuwa na uwezo wa kuboresha mastakabali (future) wa taifa letu.

Msitakabali wa watoto wetu na wajukuu zetu unategemea jinsi tutavyojipanga kuchagua rais atakae toa maamuzi ambayo yatawalinda mbeleni, tusijiangalie sisi tu, ndio maana wanzetu nchi za inje kama marekani, china au japan wanatushinda kila nyanja kiuchumi, kiutamaduni, kisiasa hata kijeshi kwa sababu wanaangalia mbele miaka mia moja au hata miaka mia mbili, sisi hatuna utamaduni huo ambao sasa inabidi au inatulazimu tuanze.

Kwa mstakabali mzuri wa taifa letu rais ajae awe na sifa nyingi , mbili kati ya hizo ni:_

1. Rais ajae awe na sifa ya ujasili wa kuvunja mkataba wa kuuza tanesco umeme iliowekwa na makampuni ya richmund. Dowans na iptl. Mkataba huu ukiachwa uendelee huko mbeleni utasababisha maafa makubwa sana kwa sababu gharama za umeme mpaka sasa ni kubwa sana na tunaambiwa bado shirika linaendeshwa kihasara, kikubwa zinatakiwa fedha nyingi kuwalipa hawa jamaa wanaouzia umeme tanesco. Madhara yake sasa. Gharama kubwa za nishati ya umeme zinasababisha jamii ijikite katiak utumiaji wa mkaa wa mimea au miti, wanajamii ngazi zote mahala popote wanatumia mkaa kupikia ili hali wajiko ya umeme wanayo lakini wameyaweka uvunguni kukwepa gharama, watumishi wa serikali waalimu, polisi, wanasiasa wanatumia mkaa kupikia. Wanasiasa wabunge,wakuu wa mikoa na wilaya wanatumia mkaa kupikia katika familia zao, wafanyabiashara wahindi, waarabu, wasomali sehemu za kariakoo , kisutu wote wanatumia mkaa kupikia kukwepa gharama kubwa za nishati za umeme, pia sisi walala hoi tunatumia kuni au mkaa kupikia suala la umeme hatuliwaziii kabisa. Gharama za umeme zingekuwa chini wakundi mengine yote niliyoyataja hapo juu yangetumia nishati ya umeme, ni sisi walala hoi tu tungeendelea kutumia mkaa na kuni sasa hebu jiulize hali hii ikiendelea miaka 30 ijayo itakuwaje kimazingira ? Milima , vyanzo vya maji vitasalimika kweli? Je kutakuwa na mvua ya kutosha itayowezesha sera ya kilimo kwanza. Ni wazi kabisa hali ya mikataba kama huu wa dowans ukiendelea miaka 50 ijayo taifa la tanzania litapotea katika uso wa dunia. Nini kifanyike. Tunahitaji rais ambae atalinusuru taifa kwa kuliwezesha kutumia umeme utaofuliwa na gesi yetu ambao ni nyingi sana, gesi hii itumike kufua umeme tuachane na umeme wa kununua wa iptl na dowans ili gharama za umeme zipunguwe makundi mengine yatumie umeme watuachie sisi walala hoi tutumie mkaa na kuni. Watu wa mtwara wanahitaji elimu ya uraia tu wataelewa wanashindwa kuelewa kwa sababu viongozi wanaoenda kuwahabarisha hawana maadili.

2. Sifa kuu ya pili ya rais ajae awe na uwezo wa kuvunja mkataba wa mtoto wa mfalme wa saudia wa kukodisha kipande cha ardhi ya loliondo na kutumia kuwindia kwa miaka 30. Makataba huu ni mbovu na unatia aibu ni sawa mtu anakuwa na ubia na mke wako nay eye anakuwa na haki ya kulala nae , mikataba kama hii wajukuu hawataweza kutuelewa, ni sawa na ule mkataba wa kikoloni uliowekwa mwaka 1928 eti nchi za maziwa makuu zilinyimwa ruhusa kutumia maji ya ziwa victoria ruksa hiyo ikapewa misri pekee kutumia maji hayo kupita mto nile si mnaona wenyewe akina lowasa walivyoushitukia mkataba huu pale walipoanza project ya kupeleka maji shinyanga?

Kwa hiyo lowassa ,sijui membe,wasira hawana sifa hizi, watanzania anzeni kutafuta rais ataewasaidia nyie watoto wenu na wajukuu zenu.

Rais atayeweza kifanya haya haraka iwezekanavyo uzalendo wake hauna shaka yoyote kama mlivyoongea vijana, maana kila moja atajiita mzalendo lakini nini kipimo cha uzalendo? Vipimo ndiyo hivyo.

Ebaeban tel.aviv

hapo kwenye nyekundu mkuu!
Huyo ndiye tunayemtaka 2015 anazo sifa ulizozitaja.
Hao wengine acha wajifunze kwanza.
 
Back
Top Bottom