Sangarara
JF-Expert Member
- Sep 29, 2011
- 13,100
- 5,655
Rais wa Marekani Donald Tramp anasemekana anafanya maamuzi yake katika uendeshaji wa nchi hii kwa misingi ambayo ameiandika katika kitabu chake kiitwacho "ART OF THE DEAL"
Msingi mkuu wa aina zote alizoziandika katika kitabu hicho na ambazo anazitumia katika uendeshaji wa biashara zake na sasa serikali ya Marekani ni "WIN-WIN STRATEGY" ambapo pande mbili za majadiliano ni lazima kila moja ikubali kupoteza kitu ili ipate hitaje lake kuu.
Haina hii ya ufikiaji wa maamuzi sio iliyozoeleka katika Tasnia ya siasa, kitu ambacho sasa kinasababisha karibia ulimwengu mzima kumgeuka na kuonyesha kutokubaliana na baadhi ya maamuzi yake ya toka alipoingia madarakani rasmi tarehe 20 mwezi wa kwanza 2017 ambayo.
Kwa mfano wakati mivutano kati ya Taifa la Israel na Palestina ukiongezeka katika siku za karibuni ukichagizwa na Marekani kugoma kupiga kura katika baraza la Umoja wa Mataifa juu ya mgogoro wa mataifa hayo mawili katika siku za mwisho mwisho za utawala wa Barack Obama, Mwanzoni mwa mwezi huu aki wa amesimama jukwaa moja na waziri mkuu wa Israel huku akitegemewa kuzungumzia mgogoro wa Israel na Palestina katika muktadha wa usuruhishi unaoshirikishawemataifa mbalimbali pamoja na baraza la umoja wa Mataifa na Hasa Muktadha wa Taifa lake mwenyewe unaopendekeza uwapo wa Mataifa Mawili katika mji wa Yerusalemu yeye akadai hajali kitu, liwe Taifa moja au mawili kwake yote ni sawa.
"I am looking at two-state or one-state, and I like the one that both parties like"
Wafuatiliaji wa msuguano baina ya Mataifa hayo mawili wanadai, Israel, Upande ambao Tramp anaupendelea ndio wamekuwa wakisupport Two-State solution kwa muda mrefu huku Mataifa ya Kiarabu yakipendelea One-State solution.
Ghafla, mwaka 2009 Barack Obama akafanikiwa kuwashawishi Waarabu wakubaliane na two-state solution kitu kinachosemekana kilisaidia kusukuma majadiliano ya usuruhishi mbele kwa hatua kubwa sana, Lakini ghafla tena, majuzi hata waziri mkuu wa Israel Mwenyewe nae akaanza kutoa kauli zinazomaanisha nae anadhani hata one-state solution iko sawa tu.
Huku akilalamikiwa kwamba anataka kurudisha mafanikio yaliyofikiwa katika majadiliano hayo nyuma sana na kwamba anachokifikiria ni kitu kilichoshindikana huko nyuma, Donald tramp inasemekana yawezekana ndio akawa ana mkakati bora zaidi wa kufikia muafaka wa mvutano huo.
Yeye anachokitaka ni Palestina na Israel wakae mezani bila kuingiliwa waamue wenyewe, Yasemekana Tayari Waziri mkuu wa Israel yuko Tayari kuwapatia Wapalestina kila wanachokitaka lakini mfukoni anakikaratasi chenye jambo ambalo atalitaka kutoka kwa Palestina, wakimpatia Mgogoro unakwisha.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa John Pombe magufuri, katika muda mfupi sana aliokaa madarakani amekwisha wakwaza Watanzania kiasi cha kutosha, ukiacha ubinyaji wa uhuru wa vyombo vya habari na uendeshaji wa siasa za kidemocrasia, kuna jambo juu ya kauli zake za vitisho,dharau na kutokujali pamoja na utayari alionao katika kutumia nguvu za kijeshi katika utekelezaji wa majukumu ya kiraia,
Kuna swala la mfumo mbovu wa usimamizi wa uchumi na mahusiano kati ya wawekezaji na wafanyabiashara na serikali pamoja na ukosefu wa pesa.
Kuna usimamizi mbovu wa sera za serikali na matumizi mabovu ya fedha kama kuelekeza fedha kwenye miradi isiyo na tija huko kwao chato.
Ni mengi sana, cha msingi ajipime na kuamua juu ya uelekeo wake, na kama atakili kufanya baya, nina jambo la kumshauri, kama yuko Tayari achukue hatua sasa na kujisafisha ili aanze upya, ninaamini akiwapa watanzania jambo moja tu leo watasahau kila ubaya, na huu upepo wote utatulia.
Let us bargain.