Rais Trump amemfukuza Mshauri wa Sera Stive Bennon

Rais Trump amemfukuza Mshauri wa Sera Stive Bennon

pantheraleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
693
Reaction score
889
Rais wa Marekani Donald Trump Ijumaa amewaambia maafisa wa ngazi ya juu ameamua kumfukuza mshauri wa sera, Steve Bannon.

Bannon ambaye kuanzia mwanzo wa miezi sita ya malumbano ya kiuongozi amekuwa ni katika washauri wake Trump ambaye ana utata mkubwa kuliko wote.

Bannon, ambaye amepewa sifa ya kumsaidia Trump kuingia madarakani, alikuwa na migongano kwa miezi kadhaa na watu wengine ambao ni wenye sauti katika ofisi ya West Wing ya ikulu.
voa-trump-amfukuza-bannon-white-house-860x450_c.jpg

Mkuu wa wafanyakazi wa White House John Kelly na Steve Bannon walikubaliana kuwa Ijumaa iwe siku ya mwisho kwa Bannon kutumikia wadhifa wake huo.

Msemaji wa White House Sarah Huckabee Sanders amesema White House inamshukuru Bannon kwa utumishi wake.

Bannon kwa mujibu wa gazeti la The New York Times amesisitiza kwamba kuondoka kwake ilikuwa ni chaguo lake, na alikuwa amepeleka barua ya kujiuzulu kwa rais siku 11 zilizopita ili itangazwe rasmi kuanzia wiki hii.

VOA SWAHILI: Fahamu kwamba habari hii imekujia hapa kutoka VOA Kiswahili. Haki miliki za Picha na Maandiko niza Shirika la VOA.
 
Trump naye hata haelewi afanye nini

from Katesh using Siemens C55
 
Hii habari kutoka VOA mbona ina ukakasi? Tumwamini nani? Heading inasema amefukuzwa, ndani kwenye maelezo, jamaa aliandika barua ya kuacha kazi mwenyewe.
 
Miaka minne itaisha hivihivi na hakuna atakachokuwa kafanya zaidi ya kutimuatimua tu
 
Back
Top Bottom