Rais Trump aendelea kutetea matumizi ya dawa ya Hydroxychloroquine kama tiba ya COVID-19

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Rais wa Marekani, Donald Trump kwa mara nyingine ametetea matumizi ya hydroxychloroquine kupambana na virusi vya corona, akiwachanganya maafisa wake wa afya.

Amedai kuwa dawa hiyo ya kutibu malaria ilikataliwa kutibu Covid- 19 kwa kuwa tu yeye ndiye aliyeipendekeza.

Kauli yake imekuja baada ya Twitter kumfungia mtoto wake mkubwa kwa kuchapisha taarifa kuhusu kutumia hydroxychloroquine.

Hakuna ushahidi kuwa dawa hiyo inaweza kupambana na virusi na wadhibiti wa dawa wanatahadharisha kuwa inaweza kusababisha matatizo ya moyo.

Mwezi uliopita, mamlaka ya chakula na dawa nchini Marekani (FDA) ilitahadharisha kuhusu matumizi ya dawa kwa ajili ya tiba ya virusi vya corona, baada ya ripoti kuhusu ''matatizo makubwa ya moyo'' na masuala mengine ya kiafya.

Mamlaka hiyo ilisitisha matumizi ya dharura ya dawa hiyo kutibu Covid-19. Shirika la afya duniani (WHO) limesema kuwa ''mpaka sasa hakuna ushahidi'' kuwa dawa hiyo ina ufanisi kutibu au kuzuia virusi vya corona.

Tafiti zilizofanywa na WHO, na Taasisi za kitaifa za masuala ya afya na watafiti wengine hazijapata ushahidi kuwa hydroxychloroquine zinapotumika na dawa ya azithromycin au bila dawa hiyo kama ilivyoelezwa na Trump inasaidia kutibu virusi vya corona.

Trump alianza ushawishi wa dawa hiyo kwa mara ya kwanza mwezi Machi. Aliwaambia wanahabari siku ya Jumanne: ''Ninapopendekeza jambo, wanapenda kusema 'usitumie' ''

Trump, 74, aliwashangaza waandishi wa habari mwezi mwezi aliposema kuwa alianza kutumia dawa hiyo ambayo haijathibitishwa kutibu corona.

Siku ya Jumanne, alisema: ''Ninaweza kusema hivyo kwa kutegemea machapisho mengi niliyoyasoma kuhusu suala hili, ninafikiri inaweza kuwa na matokeo chanya katika hatua za mwanzoni.

''Sifikiri kama unapoteza chochote kwa kufanya hivyo, inaonekana tu kuwa si maarufu sana.''

Rais Trump na mtoto wake Donald Trump Jr. ni miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii waliosambaza video siku ya Jumatatu ya jumuia ya madaktari wajiitao American Frontline Doctors, wanaohamasisha kuwa hydroxychloroquine ni tiba ta Covid-19.

Facebook na Twitter waliondoa maudhui hayo, wakisema kwamba ni taarifa za kupotosha.

Twitter pia ilimfungia mtoto wa Trump kwa saa 12 kama adhabu kwa kusambaza kipande hicho cha video.

Video hiyo ilionesha madaktari wakiongea nje ya Mahakama ya Juu nchini humo katika tukio lililoratibiwa na kundi moja ambalo limesaidia pia kufadhili kamati ya siasa inayomuunga mkono Trump.

Katika video hiyo, Dkt Stella Immanuel, kutoka Houston amesema amefanikiwa kutibu wagonjwa 350 wa virusi vya corona kwa hydroxychloroquine.

Rais alisema siku ya Jumanne: ''Ninafikiri ni madaktari wanaoheshimika. Kulikuwa na mwanamke ambaye ameeleza vizuri sana kuhusu hilo.''

Mwanzilishi wa chama cha madaktari wa mstari wa mbele nchini Marekani, Simone Gold ameshutumu makampuni hayo ya mitandao ya kijamii kwa kuiondoa video hiyo yenye taarifa kuhusu hydroxychloroquine.

Siku ya Jumatatu usiku, Trump pia alirejelea ujumbe wa twitter ukimkosoa Dkt Anthony Fauci, anayongoza kikosi kazi cha Ikulu kinachopambana na virusi vya corona.

Lakini alipozungumza Jumanne Rais Trump alikana kumkosoa Mkurugenzi huyo akisisitiza kuwa: '' ninapatana naye vizuri sana.''

BBC Swahili
 
Trump si mjinga anajua fika kwamba kampein za vitisho kuhusu matumizi ya HCQ inatokana na Makampuni makubwa ya madawa na chanjo ya huko Merikani kuhonga media, Govt Officials na WHO ili watishe tishe watu Duniani kuhusu matumizi ya dawa za HCQ huku wakijua fika kwamba dawa za Chloroquine zimetumika Duniani kwa zaidi ya miaka 75 bila ya kusababisha madhara yoyote kwa watumiaji, swali ni:Why now?

Jibu ni rahisi kabisa - makampuni makubwa ya madawa yalisha jipanga kupiga hela ndefu kutokana na janga la corona, sasa wakiona wanapendekeza matumizi ya dawa ambazo ni cheap kununua, mfano HCQ hapo wanaona deal ya kufuja tax payers' money big time itakufa, hiyo ndio sababu kubwa yakuipiga vita HCQ ili hisitumike kutibu Corona - ebu angalia wanavyo mshambulia daktari wa Kinajeria anaye ishi Texas baada ya kuwatibu wagonjwa zaidi ya 350 kwa kutumia mseto wa HCQ, zinc na broad spectrum anti biotic capsules - wamemujia juu sana na kumudhihaki na hasipo kuwa makini they can kill her - ndio wamiliki wa makampuni makubwa ya madawa ya huko Merikani yalivyo ni mafiosa.
 
Hapo Trump amenena ukweli. HCQ inaonekana haifai kwasababu alisema inatibu Corona.
 
Na ventilators.Kuna Dr mmoja alishalalmika sana hi tabia ya wagonjwa wa covid kuwekwa kwenye ventilators moja kwa moja anapokuwa admited.Kumbe ni siasa za Big Pharma companies kupiga hela kwa kuuza ventilators..Hata ukitizama tweets za Elon Musk utaona kabisa kuna kitu hakipo sawa pale US kuhusu hii Covid.Kuna mchezo unachezwa hapa.
 
Dahhh kwa nchi zetu zenye uelewa mdogo na ufahamu mdogo juu ya magonjwa ya kuambukiza najinsi ya kupambana nayo ni hatari sana maana nchi inaambiwa vazi la kujikinga na Corona ni laki 3 sasa wahudumu wapo wangapi dahh hawa jamaa wangetufirisi tuu na huu mpango wao waache walumbane sisi tunasubiri neno la mwisho na dawa ya CoVid 19 ata kama ni mseto sisi tutatumia kwetu Tz tumeanza na kujifukiza
 
Back
Top Bottom