Rais Samia umeweza kufanya mengi, bado hili

Rais Samia umeweza kufanya mengi, bado hili

Samia atosha tukutane2030

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
17,213
Reaction score
48,767
Habari!
Rais Samia mtu 🔥 🔥 🔥 kipindi unaingia watu wengi kwa chuki zao binafsi walikutabiria kushindwa. Bahati mbaya kwao umeweza kutenda ambayo mh. Magufuli a.k.a Jiwe hakuweza.

Ni kama masihara vile. Lakini kwakuwa bado wana kinyongo hujifanya hawaoni kitu ulichofanya. Na sasa wamehama kwenye maendeleo wanazingumzia ya tarehe 29 Oktoba.

Awali ya yote nakupa shukrani kwa kutujali sisi WAFANYAKAZI.

Nilianza kazi 2015 Juni mpaka Magufuli anakufa Machi 2021 niliambulia ongezeko la sh. elfu 20 tu, ni sawa na ongezeko la sh elfu 3 kwa mwaka.

Sasa hivi umeshika mpini kila mtumishi anaweza kujenga nyumba ya wastani, anaweza kununua usafiri na kumiliki biashara ya kumkwamua tofauti na kipindi cha Magufuli.

Tangu Magufuli afe nimepanda cheo mara mbili, nyongeza ya mshahara mara 4( mara mbili kwaajili ya kupanda cheo na mara mbili ongezeko la tamko).

Turudi kwenye mada.
2017 Magufuli alianzisha kampeni ya kuweka usawa kwa watumishi.

Watumishi wenye sifa sawia walipwe sawa bila kujali yuko ofisi gani. Labda posho ndo zitofautiane. Tume ikamaliza kazi 2018 na haijaleta mrejesho , Mzee akanyuti kimya. Siwezi kumlaumu, kwa ufupi Magufuli alianzisha jambo lililomzidi uwezo ndio maana akatokomea nalo.

Wewe Mh. Samia hili jambo kwako ni dogo kabisa.

Siandiki kwa kuvutia ngozi upande wangu. Mimi niko kwenye shirika la umma, nalipwa vizuri kiasi, ninalipwa posho ya usafiri, mawasiliano, pango na lunch.

Wakumbuke na wengine mama huna baya.

Si jambo jema mtumishi mwenye diploma kumzidi mshahara mtumishi mwenye degree kwakuwa tu mwingine yuko huku mwingine yuko kule.
 
Back
Top Bottom