Rais Samia umewasahau Wastaafu wanaolipwa na Hazina

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,798
71,218
Kuna kundi dogo la wazee ambao bado wako hai wanaolipwa pension na Hazina limesahauliwa sana.

Wazee hao wachache ni wale waliokuwa wamestaafu kabla mifuko ya jamii haijaanzishwa na walikuwa watumishi wa serikali.

Inasikitisha kumuona Meja wa jeshi au Daktari mstaafu akilipwa shilingi laki moja leo na huku hali yake ikiwa Hoi bin taaban.

Pension ya wazee hawa wachache ambao bado wako hai ni ndogo mno kwani viwango vya mishahara wakati wanastaafu vilikuwa vya chini na pension zao hazijapandishwa kwa miaka mingi sana.

Mama wakumbuke hawa wazee waliotumikia taifa kwa uadilifu mkubwa na wengine wamelipigania taifa hili katika vita.
 
Tuliongezewa 2015 from 50 - 100,000/=.
Nasikia wataongeza 23% labda tutapata 123,000/=.
Kwa kweli hao walipaswa walao wawaongeze flat rate ya laki moja na kuwa 200,000/ tuu.
Ni mfano mbaya sana kutowathamini hao wazee ambao wengi wao walikuwepo toka enzi za serikali ya Nyerere na wachache Mwinyi na kwa uadilifu wao hawakujilimbikizia mali za rushwa wala wizi
 
Nitashukuru kweli wakitukumbuka.

But I know they will not even think about it.
They wish we die fasta. ...!!!
 
Hivi wakuu hii pension ya kila mwezi wastaafu kwa mwezi wanakuwa wanalipwa sh ngp?

To be specific
Mfano mwalimu ambae mshahara wake wa mwisho ulikua 1.2Million.
Atakuwa analipwa Kiasi gn kwa mwezi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naunga mkono hoja..wazee hawa wametelekezwa na taifa walilolitumikia, hii haikubaliki.
Kuna kundi dogo la wazee ambao bado wako hai wanaolipwa pension na Hazina limesahauliwa sana.

Wazee hao wachache ni wale waliokuwa wamestaafu kabla mifuko ya jamii haijaanzishwa na walikuwa watumishi wa serikali.

Inasikitisha kumuona Meja wa jeshi au Daktari mstaafu akilipwa shilingi laki moja leo na huku hali yake ikiwa Hoi bin taaban.

Pension ya wazee hawa wachache ambao bado wako hai ni ndogo mno kwani viwango vya mishahara wakati wanastaafu vilikuwa vya chini na pension zao hazijapandishwa kwa miaka mingi sana.

Mama wakumbuke hawa wazee waliotumikia taifa kwa uadilifu mkubwa na wengine wamelipigania taifa hili katika vita.
 
Kuna kundi dogo la wazee ambao bado wako hai wanaolipwa pension na Hazina limesahauliwa sana.

Wazee hao wachache ni wale waliokuwa wamestaafu kabla mifuko ya jamii haijaanzishwa na walikuwa watumishi wa serikali.

Inasikitisha kumuona Meja wa jeshi au Daktari mstaafu akilipwa shilingi laki moja leo na huku hali yake ikiwa Hoi bin taaban.

Pension ya wazee hawa wachache ambao bado wako hai ni ndogo mno kwani viwango vya mishahara wakati wanastaafu vilikuwa vya chini na pension zao hazijapandishwa kwa miaka mingi sana.

Mama wakumbuke hawa wazee waliotumikia taifa kwa uadilifu mkubwa na wengine wamelipigania taifa hili katika vita.
Rais hawezi wasahau hao wapiga kura wake waaminifu..

Stay tuned siku Mwigulu akisoma bajeti utasikia..Nao wamepandishiwa pensheni.
 
Taifa lisilothamini mchango wa watu wake ni taifa mfu.
Taifa lisilothamini wazee wastaafu ni taifa linalojitenga na baraka za Mwenyezi Mungu.
 
Back
Top Bottom