Rais Samia Suluhu awatakia watanzania wote pasaka njema

Rais Samia Suluhu awatakia watanzania wote pasaka njema

Baraka Mina

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2020
Posts
593
Reaction score
611
Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za kuwatakia watanzania wote Pasaka Njema.

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ametoa salamu hizo za heri ya Pasaka kwa watanzania kupitia akaunti yake ya Twitter leo tarehe 04/04/2021.

Sambamba na kuwatakia Pasaka njema watanzania, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amewaomba watanzania kuadhimisha sherehe hiyo kwa kuliombea taifa, kudumisha upendo na mshikamano pamoja na kufanya kazi kwa juhudi na maarifa ili kuijenga nchi.

Ujumbe aliouchapisha katika akaunti yake unasomeka hivi:

"Nawatakia watanzania wote Pasaka njema, tuadhimishe ufufuko wa Yesu Kristo huku tukiliombea Taifa letu la Tanzania kudumisha amani, upendo na mshikamano. Tuendeleze jitihada za kuijenga nchi yetu kwa kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa.
Yesu amefufuka, Haleluya Haleluya."


Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan
siku ya jana (03/04/2021) aliwasili jijini Dar Es Salaam akitokea jijini Dodoma na kupokelewa na viongozi mbalimbali wa kiserikali katika uwanja wa ndege wa kimaitaifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (JKNIA).

Screenshot_20210404-055204.png

FB_IMG_1617505821307.jpg

FB_IMG_1617505835274.jpg
 
Tusisahau kumuweka kwenye maombi maalum ya kumuombea Mhe. Rais wetu, Mungu aendelee kumjaza hekima busara na nguvu ya kuendelea kuliongoza Taifa letu.
Amen, ni jambo jema na hakika Mwenyezi Mungu atasimama upande wake na kumuongoza katika kuitenda kazi hii.
Kwa pamoja tutamuombea Mhe. Rais pamoja na wote wenye mamlaka katika nchi hii.
 
Sawa ila asisubiri mpaka akumbushwe

Tanzania ni multi cultural state (jamii mchanganyiko)

Watanzania bado wana picha kichwani na lile waliloshuhudia siku ya uapisho wa mawaziri

Kitendo cha katibu mkuu kiongozi mpya (Hussein Katanga) kutosalimu upande wa pili, na yeye mama kupotezea badala ya kusawazisha kosa la katibu mkuu kiongozi
 
Sawa ila asisubiri mpaka akubushwe
Naamini Mhe. Rais alisubiri wakati mwafaka ufike ndipo aweze kutuma salamu kwa watanzania.
Kwa sababu amechapisha salamu za Pasaka kwa watanzania mnamo saa 06:12 usiku wa leo 04/04/2021.

Pia katika hafla ya uapisho wa Katibu Mkuu Kiongozi, Mawaziri na Manaibu Waziri (01/04/2021, Ikulu - Chamwino Dodoma) Mhe. Rais aliwatakia watanzania kila la heri na pasaka njema.

Suala la Katibu Mkuu Kiongozi ni la ubinadamu. Tugange yajayo.
 
Mwambien siku nyingine ajaribu kulipa heshima jina la mkombozi wetu yaani BWANA YESU KRISTO.
Haitoshi kusema " yesu amefufuka"
Kuna Yesu wengi, ila ukisema YESU KRISTO hapo unakuwa umeweka utofauti.
Imani za watu ziheshimiwe
 
Ule mchakato wa kubadili katiba atawale milele mbona kimya atusikii tena vipi mataga
Msimamo wa Chama Cha Mapinduzi ulitolewa Bungeni na Ndg. Humphrey Polepole Mbunge wa kuteuliwa na Katibu wa NEC - Itikadi na Uenezi.
Naomba kunukuu.
“Masuala ya Chama cha mapinduzi hujadiliwa kwenye vikao vya chama, hapa bungeni wabunge wana uhuru wa kuzungumza lakini kinachozungumzwa humu ndani hakiathiri msimamo wa Chama cha Mapinduzi ambao tumeshautoa, Rais hataongeza muda."
 
Mwambien siku nyingine ajaribu kulipa heshima jina la mkombozi wetu yaani BWANA YESU KRISTO.
Haitoshi kusema " yesu amefufuka"
Kuna Yesu wengi,ila ukisema YESU KRISTO hapo unakuwa umeweka utofauti.
Imani za watu ziheshimiwe
Mkuu Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ameandika Yesu Kristo.
Unaweza kupitia tena ujumbe wake huu.

"Nawatakia watanzania wote Pasaka njema, tuadhimishe ufufuko wa Yesu Kristo huku tukiliombea Taifa letu la Tanzania kudumisha amani, upendo na mshikamano. Tuendeleze jitihada za kuijenga nchi yetu kwa kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa.
Yesu amefufuka, Haleluya Haleluya."
 
Asante sana Mama yetu
Amen, kama alivyosema nasi tutekeleze kuwa kwa pamoja tuadhimisha sherehe hii kwa kuliombea taifa, kudumisha upendo na mshikamano pamoja na kufanya kazi kwa juhudi na maarifa ili kuijenga nchi.
 
Rais makini, ametaja ipasavyo. Tuache uchonganishi
Mkuu Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ameandika Yesu Kristo.
Unaweza kupitia tena ujumbe wake huu.

"Nawatakia watanzania wote Pasaka njema, tuadhimishe ufufuko wa Yesu Kristo huku tukiliombea Taifa letu la Tanzania kudumisha amani, upendo na mshikamano. Tuendeleze jitihada za kuijenga nchi yetu kwa kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa.
Yesu amefufuka, Haleluya Haleluya."
 
Tusisahau kumuweka kwenye maombi maalum ya kumuombea Mhe. Rais wetu, Mungu aendelee kumjaza hekima busara na nguvu ya kuendelea kuliongoza Taifa letu.
Kitu cha kuzingatia asimamie haki, siyo kama yule mwendazake, ambaye alikuwa na staili ya kuwabambikia kesi, wale wote anaowaona wako "critics" na utawala wake
 
Sawa ila asisubiri mpaka akumbushwe

Tanzania ni multi cultural state (jamii mchanganyiko)

Watanzania bado wana picha kichwani na lile walishuhudia siku ya uapisho wa mawaziri

Kitendo cha katibu mkuu kiongozi mpya (Hussein Katanga) kutosalimu upande wa pili, na yeye mama kupotezea badala ya kusawazisha kosa la katibu mkuu kiongozi
Kuna watu mna vipaji vya kulalamika.
 
Back
Top Bottom