Suphian Juma
Senior Member
- Apr 2, 2019
- 140
- 579
RAIS SAMIA, ALMASI LA WARIDI MCHANGANI
Na: Suphian Juma
VIPAUMBELE 10 VYA RAIS SAMIA
Nawasalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Basi siku hiyo asubuhi nikawasili kazini katika Ofisi za KWANZA TV kama ilivyo kawaida eneo la Posta, jijini Dar es salaam. Ilikuwa mwaka 2017. Tukiwa kwenye kikao cha asubuhi cha kupanga wapi pa kwenda kutafuta habari, ikaonekana ya kwamba tukio la kwanza litakuwa kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mwl Nyerere, JNICC uliopo mkabala na Ofisi yetu ya KWANZA TV, ambapo Makamu wa Rais wa Tanzania wa wakati huo Mama, Samia Suluhu Hassan ndiye alitakiwa kuwa Mgeni rasmi wa Maonesho ya Utalii ya Kimataifa yajulikanayo kama Swahili International Tourism Expo.
Nilipata kiu kubwa ya kuwahi kwenda ukumbini Kama Mwandishi wa Habari si tu kwenda ku-cover tukio lile bali pia angalau kumwona Mama Samia 'mubashara' ambaye kwa miaka yake mitatu Serikalini, alishaanza kujipambanua Kama Kiongozi mwenye busara, mwajibikaji na aliyejaa maarifa kwenye hotuba zake.
Akipita kwenye mabanda pale ukumbini JNICC nilifanikiwa kumshika mkono kwa salaam. Mama Samia kimwonekano tu, ukimwangalia kweli ni mama aliyejaa upendo si kwa maneno tu mdomoni tu bali pia hata moyoni. Si mnajua akina mama walivyo na upendo asilia? Makamu wa Rais aliwafariji Wafanyabiashara na Wawekezaji kwa maneno ya upole yaliyosheheni matumaini ya uzima katika Sekta ya Utalii. Maneno yake hadi sura yake haikuonesha ku-fake jambo- Alikuwa HALISI.
Leo napenda kutoa hisia zangu juu ya Uongozi (sipendi kutumia neno Utawala) wa Rais Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Rais wa Awamu wa Sita.
Nafahamu kuna mjadala mzito unaendelea kuhusiana na nini tafsiri ya "kumsifu ama kumkosoa Rais Samia." Lakini pia nafahamu nchi hii inaongozwa na Katiba ambapo katika Ibara ya 18 inanipa ruhusa kumpongeza, ama kumsifia, kumshauri kama ambavyo naheshimu maoni ya wengine wanaomkosoa Rais wetu- ndio Uhuru wa mawazo. Hivyo sitegemei kuambiwa najipendekeza ama nawinda UTEUZI- ambavyo hata hivyo hivi vyote viwili naona ni vya kheri hata nikitafsiriwa hivo Kama ambavyo imekuwa desturi huko mitandaoni nikimpongeza Mama.
Kujipendeza kwa maana ya kumpongeza Kiongozi sahihi ni kuwa mtu sahihi, hivo hivyo hata jambo la Kuteuliwa katika kutumikia watu ni baraka maana unaaminiwa na unaenda kuyageuza maono ya wengi (WANANCHI) kuwa matokeo-vitendo chanya.
Naomba pia nitangulize kusema tangu tupate uhuru kila Rais; iwe Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete ama Magufuli, wote wana mema wametufanyia Kama Taifa na Kama Binadamu kuteleza kupo, Ila leo Kama ilivyo; Kipenda roho hula nyama mbichi, hakika najisikia kujikita kuusema wema wa Rais Samia kama namna pia ya kumpa morali ya kutuvusha kwenda kwenye 'Tanzania ya ahadi kwa SOTE.'
Rais Samia kama wasemavyo wahenga: "nyota njema huonekana asubuhi", hakika katika makao yake mapya Ikulu chini ya miezi miwili sasa, nadhani mtaungana nami kwamba Tanzania, Afrika na hata dunia tumepata 'Almasi la Waridi.'
KWA WASIOFAHAMU; Almasi la Waridi kutoka Afrika Kusini, kwa mujibu wa chapisho la BBC la Novemba 14, 2018 ni aina ya madini ya Almasi adimu na ghali mno duniani- unaambiwa karati moja tu huuzwa dola milioni 50 katika soko la dunia la madini. Imagine....!!
Hebu tujadili maeneo makuu 10 kama vipaumbele vya Mama Samia kama Rais alivyoanza kujipambanua nayo tangu punde alipoingia Ikulu tuone kama kweli ni Almasi la Waridi?
KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI;
Katika eneo hili sote tunajua mazingira ya kuanzisha biashara na uwekezaji miradi nchini, kwa muda sasa si rafiki. Adui hapa ni kodi zisizohimilika. Mwekezaji Mkubwa wa Afrika, Bwana Dangote mwaka jana tu alipokuwa anahojiwa na chombo fulani cha habari alisema Tanzania ni nchi pekee yenye kodi kubwa mno kuliko nchi yoyote aliyowahi kuwekeza duniani.
Rais Samia akiwaapisha Mawaziri wiki majuzi na hata juzi kwenye Kongamano la Viongozi wa dini alitamka; Serikali yake itahakikisha Wawekezaji na Wafanyabiashara wadogo na wakubwa watapunguziwa mzigo wa kodi, kuwekewa Sera rafiki isiyobadilikabadilika ili kuwalinda Wafanyabiashara na Wawekezaji.
Mhe. Rais Samia alipokuwa anawaapisha Mawaziri, alimwagiza Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Mwigulu akashirikiane na TRA na mamlaka zingine za Serikali na Sekta Binafsi kuzalisha walipa kodi wapya kwa kuondoa kodi kandamizi. Waziri Mwigulu ana historia ya uchapakazi naimani hatamwagusha mama na hatimaye Tanzania itakuwa nchi bora zaidi -Kivutio cha Biashara na Uwekezaji Afrika na Duniani. Mama Samia si Almasi la Waridi tu jamaani?
KUUTAFSIRI UCHUMI MKUU KUWA UCHUMI WA WATU;
Hii imekuwa changamoto kubwa sana kwa wananchi, alipokuwa akiwaapisha Mawaziri/Makatibu wa Wizara, Rais Samia alitamka wazi kwamba Watanzania hawana pesa mfukoni, na kwamba dhamira yake ni kuufanya uchumi mkuu yaani ule wa takwimu za kuingia uchumi wa Kati, kuleta matokeo chanya ya kuonekana kwa kila mwananchi mmoja mmoja. Pesa ionekane mtaani, watu waweze kujikimu na gharama za maisha yaani pawepo na uwiano baina ya kazi wanazofanya na matunda ya kazi hizo. Nauliza bado tu huyu sio Mkombozi wa wananchi? Bado ni wale wale Viongozi wasio na dira kama mnavyodai humu mitandaoni?
UHURU WA HABARI NA DEMOKRASIA;
Almasi la Waridi letu limeweka wazi kwamba vyombo vya habari vitakuwa huru. Kuna mtu ana hofu na hili? Hebu tamthiminini katika mwezi mmoja huu wa Mama Samia; Magazeti, TVs, Online Platforms zinavyoripoti masuala hususani ya Serikali, naimaini mtaungana nami kwamba 'wamejiachia', na habari za kiuchunguzi zinachapishwa, na hata hakuna aliyepewa onyo na Waziri wa Habari wala Mkurugenzi wa Habari Maelezo ama Rais mwenyewe.
Kama raia na mwanachama wa CCM nimekoshwa sana maana katika Ilani yetu ya 2020/2025 imeeleza: Uhuru wa vyombo vya h abari, Sura ya sita kifungu cha 125(b)(d); Kuhakikisha kuwa uhuru wa vyombo vya habari unaimarishwa na kulindwa na kwamba wamiliki na wanahabari wanazingatia maadili na weledi katika kazi zao. (d) kuhakikisha uhuru wa kupata na kutoa habari unaendelea kutekelezwa kwa mujibu wa sheria na wadau wote wanazingatia wajibu wao. Rais wetu licha ya kutangaza vyombo viwe huru, ameamua kutekeleza kwa vitendo kwa kuamuru vyombo vya habari vilivyofungwa viachiwe huru.
Wanasiasa na vyama vya Siasa sasa wanazungumza watakavyo, utamsikia leo Tundu Lissu anaongea yake, Mbowe naye na yake, Zitto na mambo yake ya uchambuzi wa CAG, huko Zanzibar na Jimbo la Muhambwe katika uchaguzi Mdogo, ACT Wazalendo kupitia Kiongozi wao Zitto Kabwe wametangaza mambo shwari, uchukuaji fomu, kampeni hadi (kuelekea) matokeo ni HURU HURU HURU.... Jamaani nauliza Tanzania hatujaokota Almasi la Waridi?
KUBORESHA MAHUSIANO YA KIMATAIFA;
Katika hotuba zake takribani tatu Sasa, Rais Samia hajaacha kushindilia nyundo kwenye uimarishaji wa Mahusiano ya Kimataifa. Mwl Nyerere alishawahi kunena kwamba; Matatizo yetu hatutayaondoa kwa kujifanya/kujidanganya hayapo. Kwa hakika kwa muda sasa hatusemwi vema duniani.
Rais wetu alipokuwa anamwapisha Mama Balozi mtaalam wa Diplomasia, Mama Mulamula kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, alisisitiza; Tanzania sio kisiwa, hatuwezi kujitenga na dunia, tukiahirikiana na wenzetu duniani tutafika mapema tunapopataka kimaendeleo. Kwa nia hii ya Rais wetu mazao yetu, madini, uwekezaji na ukuaji wa uchumi Sasa utapaa. Yamkini najivunia Almasi hii ya Waridi.
KUBORESHA MASLAHI YA WAFANYAKAZI NA KUIMARISHA NIDHAMU SERIKALINI;
Nadhani tutabaliana kwamba kwa Serikali zilizopita nidhamu katika ofisi za umma zimeimarishwa na ndio maana Sasa ukiingia ofisi yoyote angalau utasikilizwa kwa umakini na kutatuliwa tatizo lako. Changamoto kuu iliyopo ni kwamba Wafanyakazi karibu wote kwa miaka kadhaa sasa hawajapandishwa mishahara, kupandishwa madaraja wala kulipwa malimbikizo ya madai yao kwa Serikali.
Nadhani Sasa ni muda mwafaka kundi hili kupewa stahiki hizi ili kuendana na gharama za maisha kama alivyosema Rais Samia. Itakuwa uonevu wa juu mno kuwashurutisha Wafanyakazi watoe matokeo chanya maofisi huku wana stress za maisha, wasimudu gharama za maisha yao na familia zao. Imani yangu Rais Samia atatangaza habari njema Mei Mosi mwaka huu.
VITA DHIDI YA UFISADI NA RUSHWA;
Samia mapema kabisa ndani ya wiki akiwa Ikulu ameonesha kwa vitendo kwamba si rafiki wa wezi na mafisadi wa mali/kodi za umma. Mtaona wazi alipomsimamisha kazi Mkurugenzi wa Bandari na alivyoagiza ukaguzi maalum (Special Audit) wa fedha za maendeleo zilizotolewa kati ya Januari na Machi 2021 Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Sisi kwenye Chama Cha Mapinduzi, CCM kupitia Ilani yetu ya 2020/2025 Sura ya 6 ukurasa wa 164 kifungu cha 116(b) tumeelekeza wazi kwamba wote wanaohusika na uzembe, wizi, ubadhilifu na matumizi mabaya ya ofisi za umma wachukuliwe hatua. Rais wa Serikali na M/kiti mtarajiwa wa Chama chetu anachukua hatua. Nakoshwa sana kama mwanachama wa CCM.
KUENZI TUNU ZA TAIFA;
Kama waasisi wa Taifa letu walituridhisha umoja, upendo, utu, mshikamano na amani ndivyo ambavyo Rais wetu Samia tangu aingie madarakani mwezi Machi 2021 amekuwa kinara cha kutuunganisha sote bila kujali tofauti zetu za kiitikadi na imani.
Mama Samia amekuwa chapa ya umoja wa kitaifa, kipenzi cha makundi yote nchini- si wanasiasa, wasomi, Wafanyakazi, wakulima, wafugaji, wavuvi wala jamii za Kimataifa sote tumeanza kujamiana vema na kuheshimiana licha ya tofauti zetu. Watu wanamwagia Sifa haswaa. Kwanini tusiseme tumeokota Almasi la Waridi mchangani?
KUDUMISHA MUUNGANO;
Sasa hivi salam kuu ya Taifa letu ni: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kila asimamapo Rais wetu Samia hutusalimu kwa maneno haya akimaanisha tufanye yote ila tusiubeze wala kufikiria kuuvunja Muungano wetu. Rais Samia yupo radhi kutatua kero ama Changamoto za Muungano ambazo mara kadhaa zimeibua hoja za kuubeza Muungano wetu.
Si salam tu wala hotuba zake za kuhimiza hili, Ila Rais wetu wiki jana ameiambia dunia kwa vitendo kwamba ana mahaba mazito na Muungano pale alipomtuma Rais wa Zanzibar, Dkt Hussein Mwinyi akamwakilishe katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za SADC uliofanyika Msumbiji- kitendo ambacho nadhani hakijawahi kutokea tangu mwaka 1964. Mara nyingi kwenye majukwaa haya ya Kimataifa, imekuwa desturi asipoenda Rais basi atawakilishwa na Makamu wake. Huu ni mwanzo mujarabu wa kuustawisha Muungano wetu na kutatua kero za Muungano ili pande zote mbili; za Tanzania Bara na Tanzania Visiwani kufaana vilivyo. Kudos Mama Samia, Almasi la Waridi.
KUONDOA KERO ZA WANANCHI NA KUDUMISHA HUDUMA ZA JAMII;
Kero za WANANCHI ni nyingi. Katiba yetu Ibara ya 8 imeweka wazi kwamba wenye mamlaka ya juu zaidi katika nchi ni WANANCHI. Na hata katika Ilani ya CCM Sura ya 6 imeeleza wazi WANANCHI ambao ndio wenye nchi yafaa waheshimiwe na kujaliwa ipasavyo.
Rais Samia katika vipaumbele vyake hili amelitaja mara nyingi. Mtaona suala la kuondoa kodi kandamizi, kuhakikisha huduma bora kama vile za maji, umeme, afya, elimu n.k zinawafikia wananchi amesisitiza sana. Ameagiza walimu 6000 kuajiriwa, vijana elfu 12 kusomeshwa bure katika vyuo vya Ufundi Stadi (VETA).
Huu ni mwanzo mzuri wa kwenda kuajiri watumishi wapya wa kada zote nchini. Mtakumbuka majuzi alisema si uungwana kumlazimisha kijana aliyetoka chuo juzi ajiajiri. Tafsiri yake ana dhamira na Serikali yake kuwaajiri vijana na kuwewekea mazingira rafiki ya wao kujiajiri badala ya kuwasahau au kuwatenga na fursa muhimu wanazoziweza; lengo ni kujikimu kimaisha na kujenga Taifa. Vijana wategemee faraja kubwa katika uongozi wa Mama yao kipenzi, Rais Samia.
Katika eneo hili la Kero za WANANCHI nizunguzie kidogo kuhusu Sekta ya AFYA; tumemsikia pia Rais Samia alivyoanza kulidhibiti gonjwa la Corona. Juzi akiongea na Watanzania kupitia Kongamano la Viongozi wa dini, ametangaza kwamba ameunda Tume ya Wataalam ili kupata ushauri kuhusu gonjwa hili. Aidha amesisitiza kwamba wakati tunasubiri tamko la Serikali, vema sote tuchukue tahadhari dhidi ya Corona ikiwemo kunawa mikono, kuvaa barakoa, kuzingatia umbali baina yetu n.k Jamaan huyu si Almasi la Waridi? Tunataka nini zaidi ya upendo huu asilia wa Mama?
Kero nyingine ni UTOAJI HAKI kwa WANANCHI na makundi mbalimbali. Rais wetu hataki mtu aonewe. Hapa nitoe mfano wa masuala ya Haki Jinai. Nimeona Mtandaoni wengi wanalalamika madhila wanayopata wafungwa/mahabusu- hapa naomba nimrejee Mwanaharakati Tito Magoti aliyeandika Barua ya wazi kwa Rais Samia. Rais wetu wiki chache zilizopita alishasema hataki dhuluma, hataki kesi zicheleweshwe wala mahabusu na wafungwa kulundikwa magerezani.
Mhe. Rais Samia wakati akiwaapisha Mawaziri, alimwagiza Waziri wa Sheria na Katiba, Prof Kabudi akahakikishe kesi za hovyohovyo za Serikali ZIFUTWE, hii ni habari lulu kwetu WANANCHI na makundi yote nchini wahanga wa adha hizi. Tuna Rais kipenzi Cha HAKI. Naimani huu ni mwanzo mzuri wa kuachiwa huru wote wasio na hatia. Jamaan nauliza huyu Mama si Almasi la Waridi?
KUENDELEZA NA KUANZISHA MIRADI YA MAENDELEO;
Katika nchi yoyote ile duniani, miradi ya kimkakati ni muhimu sana katika uchechemuzi wa uchumi wa Nchi. Rais Samia ametangaza kuendeleza miradi ya Mtangulizi wake, Hayati Magufuli 'kadri itakavyofaa na kuwezekana'. Hapa tumeona majuzi ameenda Uganda kusaini mkataba wa mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima-Uganda hadi rasi ya Chongoleani Tanga-Tanzania ambapo ajira zaidi ya elfu 10 zitatolewa.
Miradi kama hii na mingine mipya ambayo itaanzishwa chini ya uongozi wa Mama Samia itapunguza kero ya ukosefu wa ajira, italiongezea taifa letu mapato na kupanua wigo wa maendeleo kwa ujumla. Faida itakuwa kwetu sisi wananchi na Taifa iwe directly au indirectly, sasa ama baada ya muda fulani, kikubwa hapa ni subra na ku-trust the process.
Ingawa pia kwakuwa Rais wetu ni Kiongozi anayependa mawazo mbadala, kwenye suala la miradi naimaini atazingatia zaidi ushauri wa wanauchumi wabobezi kama alivyokuwa tayari kusikia ndimi za Wataalam wa Afya kabla ya kuamua juu ya Corona.
Aidha kushauri juu ya 'approaches' za uendeshwaji miradi hiyo ni muhimu sana, mfano mimi ningeanza kushauri kutotumia 'cash' kuendesha miradi kama ya ndege kama alivyoshauri Mchumi Mbobezi Prof Assad (X CAG) badala yake tukope, lengo kutoathiri uchumi wa watu na kuendeleza umaskini badala ya kuutokomeza umaskini kama ilivyo dira yetu ya Taifa.
Ndugu zangu kwa kupitia hivi vipaumbele 10 vya Rais wetu, bado Kuna mtu ana mashaka kwamba Mama Samia ni Asset pale Ikulu? Kwamba yeye ni wale wale jamii ya Viongozi wa kutotupeleka mbele kimaendeleo? Kwamba yupo pale Ikulu kujinuisha yeye mwenyewe, Familia na Chama chake?
Yes tuna haki ya kukosoa, na tuendelee kukosoa kwa kujenga, yes tuna haki ya kumshauri, tuendelee kumshauri tusonge nae njia sahihi, ila chonde chonde TUSIMBEZE maana hakika ameonesha nia njema, na ameanza kuibadili hiyo nia kuwa matendo mema. Wajibu wetu sote; WANANCHI, AZAKI, Wanasiasa, Wasomi, Viongozi wa dini, Jamii za Kimataifa na kipekee kabisa WATUMISHI WA UMMA, tumsaidie kuitekeleza adhima yake kuwa vitendo- TUWAJIBIKE.
TUSIMWANGUSHE Jemedari wetu, kama ambavyo yeye hajatuangusha kwenye vipaumbele vyake. Yeye peke yake HAWEZI, tumshike mkono, kupitia yeye tuitazame mbele yetu kwa MATUMAINI makubwa, tuzizike tofauti zetu kama alivyosisitiza yeye mara tu alipoingia Pahala patakatifu-Ikulu.
Kwa wenye shukrani kwa kidogo kabla ya kupata kikubwa nadhani sasa Tanzania tumepata Kiongozi mithili ya "Almasi la Waridi" ambaye ni adimu sana katika mawanda ya Siasa na Uongozi nyakati hizi. Tukishindwa kulitumia vema dini hili kwa manufaa ya Taifa, kosa litabaki kuwa letu wenyewe.
Nakaribisha Mjadala.
Mungu mbariki Rais Samia.
Mungu ibariki Tanzania na Watanzania.
Suphian Juma,
Mwanachama wa CCM.
Singida, Tanzania.
Kwa maoni na ushauri:
Email: yessuphian@gmail.com
Phone (Whatsapp zaidi): +255 717027973