Rais Samia ni Kiongozi muongoza njia

Rais Samia ni Kiongozi muongoza njia

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
40,623
Reaction score
26,271
Ndugu zangu Watanzania,

Kiongozi Bora ni yule mwenye uwezo na ubunifu wa kuonyesha na kuongoza njia. Ni yule awezaye kutangulia mbele na kufuatwa na wengine. Ni yule awezaye kuwa na dira na ramani ya kule anakotaka kwenda,Kiongozi asiye na dira Wala ramani Wala muelekeo Wala kujuwa wapi anakotaka kwenda lazima atawapoteza watu wake.

Kiongozi asiye na maono hawezi kuwaongoza watu kwa mafanikio, kiongozi asiye na dira ataongoza watu wake Kama kipofu, kila kitu atafanya kwa kukisia na kubahatisha tu. Jambo ambalo Ni hatari Sana katika uongozi maana wakati wowote ule ni lazima atawapeleka watu wake shimoni na kuwaangamiza,kiongozi asiye na dira atafanya kila kitu kwa kugusa gusa tu pasipo kumalizika Wala kufanikisha,kila Siku atakuwa anaanza upya na kupanga mipango na mikakati isiyo kamilika.

Rais Samia Ni kiongozi muongoza njia, Ni kiongozi anayejuwa wapi anataka kulipekeka Taifa letu, anajuwa Ni wapi Taifa hili linapaswa kuwa kimaendeleo, Anajuwa Nini kinapaswa kupewa kipaombele, Anajuwa Ni uchumi wa aina gani unapaswa kujengwa kuweza kuwanufaisha watanzania.

Rais Samia anajuwa Ni miradi ya aina gani inapaswa kujengwa na kupewa kipaombele,anajuwa Ni wapi papelekwe fedha za kutosha, anajuwa Nini afanye katika kila secta inayogusa maisha ya watanzania.

Ndio maana watanzania tunaona Rais wetu akizungumza na kila mtu na kila kundi na kila taaisisi kwa kuwa anatambua ya kuwa ili safari iwe njema na nzuri na tufike kwa pamoja Ni lazima kila mtu awe na amani Moyoni mwake, Tuaminiane, Tusikilizane, Tushirikiane na kuwa wamoja katika kulitumikia Taifa letu.Ndio sababu ya kuungwa mkono na kila mtanzania katika safari yetu ya kuelekea nchi ya ahadi yenye asali na maziwa na itiririshayo fursa za kila aina, Ndio sababu ya nchi Kuendelea kuchanua kwa furaha na amani katika mioyo ya watanzania, Ndio sababu ya kutamalaki kwa utulivu na Amani hapa nchini, Ndio sababu ya kila mmoja wetu kuongea na kutamka maneno ya kizalendo juu ya Rais wetu na Taifa letu.

Watanzania Tuendelee kumuunga mkono mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani ,kwani ameonyesha dhamira njema na ya dhati katika kuijenga nchi yetu na kuwa mfano wa kuigwa katika uzalendo uliotukuka katika kifua chake juu ya Taifa letu,Ndio sababu ya kuwa mfano wa kuigwa Barani Afrika.

Kazi Iendeleee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627
 
Haya alikimbiwa kila Rais akiwa madarakani na akitoka hutukanwa

USSR
 
Tulikuwa na jasiri muongoza njia, Sasa tuna kiongozi muongoza njia😎
Wote tuseme weweeeeeeeh😁
 
Myangulizi wake alikuwa mporaji, mtekaji na muuaji yaani mtoa roho za watu.
 
Ndani ya miaka miwili ya uongozi wake amefanikiwa kuimarisha utawala bora na wa sheria, demokrasia na haki. Mungu ampe afya njema azidi kuliongoza Taifa.
 
Ndani ya miaka miwili ya uongozi wake amefanikiwa kuimarisha utawala bora na wa sheria, demokrasia na haki. Mungu ampe afya njema azidi kuliongoza Taifa.
Hakika Mwenyezi MUNGU Aendelee Kumjalia Afya njema na nguvu za Kuendelea kututumikia watanzania maana ameonyesha dhamira njema ya kututumikia watanzania na kutukwamua kiuchumi
 
Back
Top Bottom