Rais Samia hongera kwa kuupiga mwingi

Rais Samia hongera kwa kuupiga mwingi

adobe

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2009
Posts
2,770
Reaction score
1,887
Mama nakupongeza kwa kufanya kazi kuondoa kero zinazowakabidhi Watanzania, Mungu akubariki sana.

Kuondoa uozo hapo Utumishi haikua kazi ndogo, viongozi hapo Utumishi baada ya Magufuli kuingia walijikomba kwake na kuanza kurekebisha sheria zilizowekwa na Mkapa na kuleta za kwao ili kukomoa/kusaidia wapendwa wao. Hata hilo la Utumishi kusimamia ajira hata kwenye Masharika ya Umma na Taasisi, huyo Ndumbaro ndiye aliyebadilisha.

Kwa kuacha shughuli za Masharika zifanywe na Utumishi ni kuwanyang'anya Bodi za Wadhamini zilizoteuliwa na kukasimiwa usimamizi wa Masharika na Taasisi kazi hiyo na kuiweka mfukoni kwa Ndumbaro.

Raisi na Mama yetu futa marekebisho yote yaliyofanywa na Ndumbaro na genge lake , itasaidia Masharika na Taasisi kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

Utumishi pameoza, ikiwezekana Katibu Mkuu mpya apasafishe 50%.
 
Anaupiga mwingi kwa kweli!! Hata kama hawataki kimoyo moyo wanakiri hili.

Wasiojulikana hivi wapo wapi siku hizi? Daah Mungu wetu jamani ni fundi acheni tu!!
 
Kama Jenister Mhagama anaendelea kuwepo utumishi,bado kuna tatizo.
Sijawahi kumuelewa huyu chawa
katika utumishi.
Mama asipoondoa huyu chawa pale utumishi hakuna kitu.

Huyu Waziri yupo tayari kufanya uovu wowote ili apewe cheo. Kumbuka alivyoharibu mfumo wa mafao yeye na Magufuli Pombe
 
Hali ya uchumi ni ngumu sana huku mtaani pesa hakuna na gharama za maisha zipo juu.

Wanaonufaika ni wanasiasa tu peke yao ila kwa mwananchi wa kawaida hali ni tete.

Huko kwenye siasa nako majina ni yale yale tunayoyasikia miaka yote hivyo kwakweli hakuna unafuu wowote kusema kuwa kuna jambo la kupongezwa limefanyika.
 
Mama asipoondoa huyu chawa pale utumishi hakuna kitu.
Huyu Waziri yupo tayari kufanya uovu wowote ili apewe cheo. Kumbuka alivyoharibu mfumo wa mafao yeye na Magufuli Pombe
Hilo nalo mkalitazame
 
Mama asipoondoa huyu chawa pale utumishi hakuna kitu.
Huyu Waziri yupo tayari kufanya uovu wowote ili apewe cheo. Kumbuka alivyoharibu mfumo wa mafao yeye na Magufuli Pombe
Hawa wamatengo walikua waovu sana kwa watoto wetu, ni upendeleo mwanzo mwisho na visingizio mchakato haujakamilika
 
Hawa wamatengo walikua waovu sana kwa watoto wetu, ni upendeleo mwanzo mwisho na visingizio mchakato haujakamilika
Mhagama na ndugu yake Ndumbaro walikua miungu watu pale utumishi, ilipaswa hata mhagama nae atoswe maana wana mawazo ya muasisi wa roho mbaya tanzania 2015-2021,
ndumbaro alishiriki kunajisi utumishi wa watanzania, alikuwa anajitungia na kutungua sheria za watangulizi wake bila kuangalia madhara yake huko mbeleni.
hawa wamatengo ni wa hovyyo na roho mbaya sana
 
KAZI NA IENDELEE
 
Mama asipoondoa huyu chawa pale utumishi hakuna kitu.

Huyu Waziri yupo tayari kufanya uovu wowote ili apewe cheo. Kumbuka alivyoharibu mfumo wa mafao yeye na Magufuli Pombe
masalia ya mwendazake angeyamwaga yote maana zile upupu alizowajaza hazijawatoka
 
Back
Top Bottom