Rais Samia atembelea ofisi za CCM mkoa wa Tabora

Rais Samia atembelea ofisi za CCM mkoa wa Tabora

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
Joined
May 13, 2018
Posts
439
Reaction score
742
TAARIFA KWA UMMA

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan leo Jumatano tarehe 18 Mei, 2022 ametembelea ofisi za Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora ambapo alipata nafasi ya kusaini vitabu vya wageni, kukutana na kufanya mazungumzo na kamati ya siasa ya mkoa huo.

Pamoja na mambo mengine Mwenyekiti wa CCM Taifa alipokea taarifa ya mwenendo wa uchaguzi wa ndani ya chama unaoendelea na kujadiliana masuala mbalimbali yenye ustawi na CCM na wananchi wa Tabora kwa ujumla.

Awali Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora Ndg Hassan Wakasuvi akimkaribisha Ndg Samia Suluhu Hassan alimueleza kuwa Chama Cha Mapinduzi mkoani Tabora na wananchi kwa ujumla wanaridhishwa na utendaji wa serikali anayoiongoza katika kuimarisha utoaji huduma, ujenzi wa miundombinu na ukuzaji wa uchumi kwa wananchi mkoani humo ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025.

"Nimekuwa mwanachama wa chama hiki na kiongozi kwa miaka 25 lakini tukio la Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutembelea ofisi za chama chetu na kuzungumza na viongozi wake hili ni tukio la kwanza kwa mkoa wa Tabora. Haya ni mahusiano mazuri baina ya chama na serikali, tunakushukuru sana na tunakukaribisha Tabora." alisema Ndugu Wakasuvi

Rais Samia Suluhu Hassan yupo mkoani Tabora kwa ziara ya kikazi ya siku tatu aliyoianza tarehe 17 Mei, 2022 na ataihitimisha tarehe 19 Mei, 2022 kwa kuwahutubia wananchi wa mkoa wa Tabora katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.

Shaka Hamdu Shaka
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa
Itikadi na uenezi
18 Mei, 2022.

IMG-20220518-WA0045.jpg
IMG-20220518-WA0044.jpg
IMG-20220518-WA0043.jpg
IMG-20220518-WA0046.jpg
 
Huyu mkuu wa mkoa nilijua tu lazima avae nguo zenye picha ya chifu hangaya. Nilikuwa natafuta sana picha zake.
 
Batilda Buriani amekuwa mtu wa hovyo sana pamoja na doctorate yake..

Huyu mama enzi ya JK alikua bold sana hata akiongea unaona kabisa kichwani zimo sijui kakumbwa na nini siku hizi kajitoa ufahamu kwa uchawa uliopitiliza... elimu zetu waafrika hazitusaidii ndo maana si rahisi kutofautisha wasomi na washenzi...

Haki zao huona kama fadhila... huyu mama kawa kituko pale Tabora kwa uchawa wake kwa Hangaya... PATHETIC!!
 
Mkuu mbona habari haimzunhumzii kabisa huyo mkuu wa mkoa Dr. Batilda? Kwann unamnanga?
 
Kushona nguo zenye picha ya mama Samia ni ujinga
Sasa hizo nguo tu ndiyo zimekupa uthibitisho kuwa hata kichwani ni mweupe?

Yawezekana hozo nguo kashona kwa mahaba tu aliyonayo kwa mhe rais SSH ambaye ni mwanamke mwenzie.
 
Huyu mkuu wa mkoa nilijua tu lazima avae nguo zenye picha ya chifu hangaya. Nilikuwa natafuta sana picha zake.
Dogo siky hizi na weweni mpinzani? Jiwe alikamata bongo zenu fedhuli nakuwaacha wakiwa.

Hopeless kabisa!
 
Sasa hizo nguo tu ndiyo zimekupa uthibitisho kuwa hata kichwani ni mweupe?

Yawezekana hozo nguo kashona kwa mahaba tu aliyonayo kwa mhe rais SSH ambaye ni mwanamke mwenzie.
Yes ni mtupu kichwani, kwa kuwa angekua ana akili vizuri angejiamini bila kuwa chawa. Hapo anaonyesha hajiamini na ni mtupu kichwani, njia pekee ya kubaki kwenye nafasi ni hiyo ya kushona nguo za picha ya raisi.

Hakuna mapenzi hapo, hapo inalindwa nafasi yake tu.
 
Safi sana, akitembelea mikoa,asisahau Ofisi za Chama.

CDM vyama vyao vya kwenye mikoba, ujanjaujanja tu
 
Safi sana, akitembelea mikoa,asisahau Ofisi za Chama.

CDM vyama vyao vya kwenye mikoba, ujanjaujanja tu
We pimb, umezaliwa juzi, hujui hizo ofisi na viwanja vya mpira walivyopora ccm vilijengwaje, kaa kwa kutulia,
 
We pimb, umezaliwa juzi, hujui hizo ofisi na viwanja vya mpira walivyopora ccm vilijengwaje, kaa kwa kutulia,
Zilijengwa na wanachama wa ccm, kama ulihama CCM ukahamia upinzani basi ulizikataa haki zako, ni sawa na Leo ukihama chama Cha Mbowe, huwezi kwenda kudai matofali uliyochangia
 
Kushona nguo zenye picha ya mama Samia ni ujinga
Kuvaa nguo za hapa nchini ni uzalendo wa hali ya juu kwani anakuza uchumi wetu kuliko wale wanaokwenda fanya shopping nje ya nchi!
Anatakiwa asifiwe badala ya kumshambulia.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom