Rais Samia atapendwa kuliko atakavyochukiwa

Master Legendary

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
549
785
Kwa Utamaduni wa Watanzania Kifo kinaheshimika sana na kinachukuliwa kwa hofu na heshima kubwa sana,Nilishangaa sanasana kuona kuna Watu wanakamatwa kwa kusherehekea kifo cha Kiongozi wao Mkubwa wa Nchi na nimeendelea kufuatilia kauli za Viongozi wakubwa tu nikaona kuna zenye mwelekeo wa kushukuru Kiongozi huyo kuondoka.HII IMENISTUA NA KUNISHANGAZA SANA.

Tuwe wakweli Mzee wa Msoga aliweza kujitahidi kugusa Maisha ya watu ingawa wabongo hawasemi hadi siku mtu akiondoka,kwa unafiki sasa hivi wanamponda ila naomba mreserve maneno yangu siku Mzee wa Msoga akiondoka ndiyo mtajua kwa kiasi gani alikuwa anapendwa na kagusa Maisha ya watu na Makundi mengi ya Watanzania.

Ukiacha unafiki wa Watanzania na Siasa na mambo mengine ya Udini,Jinsia,Ukanda nk.Trend anayokwenda nayo Mama Samiah ni ya kugusa Mioyo ya Watu na anatumia Vizuri Karama hiyo aliyopewa na Mungu kuponya majeraha na kugusa Watanzania Wengi.

Ninachokiona akiendelea kwa kasi hii huko mbele huenda akawa Rais kipenzi cha Watanzania kuwahi kutokea.

Kongole kwa Washauri wa Mhe.Rais mnaupiga mwingi mno na mnampatia sanasana,endeleeni kuumiza Vichwa Mama anaingia Mioyoni vizuri sana.

Hii hoja ni kwa Maslahi ya Taifa kumsapoti Pascal Mayalla ,Genge mkiingia hapa mtachezea Block.
 
🐒🐒🐒
16565816466093.jpg
 
Hizi ni sifa za kawaida sana, tofauti na wenzako ww unajua kuweka paragraph kwenye uandishi wako. Lakini hujaongea jipya lolote.
 
Itategemea na mpendaji kaweka wapi perception yake, kama katazama macho na kusikiliza sauti tu, ok, lakini kama ameangalia mambo ya msingi zaidi kama utii wa sheria, No.
 
Kitendo cha kuropoka na kuaribu uchumi sioni jipya kwake aendelee kuwakumbatia bmaeberu tu
 
Yafaa nini mtu kuoneshwa mapenzi baada ya kifo chake?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom