Rais Samia Suluhu Hassan, leo Agosti 9, 2025 amechukua fomu ya kuwania muhula wa pili wa Urais katika ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (#INEC) akiwa ameongozana na Mgombea Mwenza, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ambao wanajiandaa kwa Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.