technically
JF-Expert Member
- Jul 3, 2016
- 12,510
- 51,049
Kwanza nikumbushe Mimi sio mwanachama wa chama chochote cha siasa na sitegemei kuwa mwanasiasa.
Niliapa kuongea ukweli daima sitanyamaza wala kuwa mnafiki maana hakuna anayenitisha na kunishutua ndani ya Tanzania hii.
Anayenitisha ni Mungu pekee ambaye alinipa uhai na kunifanya niishi sio binadamu mwenzangu asiyetaka kuambiwa ukweli.
Rais kama unaweza kuvunja katiba na kuzuia Uhuru wa watu kupata habari usizozipenda maana Yake umewafanya watanzania ni wajinga tu unachotaka wewe ndio wanachotaka wao.
Yaani kila siku bunge lipo gizani ambalo wabunge ndio wawakilishi wetu wa kero za wananchi wakati wewe upo live.
1: Kuzindua daraja la kigamboni upo live hata kama lilijengwa na kikwete.
2: Kuweka msingi wa hostel upo live
3: Siku ya mahakama upo live...
4: Kuapisha Mkuu wa majeshi ,Wakuu wa mikoa,Wakuu wa wilaya,Wakurugezi ,Wakuu wa magereza ,Jaji mkuu upo live tu lakini bunge lipo Giza.
5: Upo Simiyu,Bukoba,Shinyanga,Singida,Dodoma,Kahama live....
5: Mikutano ya Ccm upo live tena unaongea sana peke yako wengine uwapi nafasi ya kuongea.........
6: Msibani upo live hata unabatiza watu majina kuwa wapo na wake zaidi ya mmoja.........
7: kuzindua ndege upo live tena huku ukiwakejeli wapinzani wako wakati pesa ya kodi zetu wote ndio zilinunua ndege.....
Lakini bunge kimya kuna haja gani ya wewe Rais kutumia kodi zetu kwenye anasa kama za msiba,uzinduzi wa hostel na kwingine wakati bunge linalotunga Sheria za kusimamia rasilimali zetu kama Madini ,Gesi,Ujenzi wa reli,mikataba hatari ya wachina lipo gizani?.......
Hoja ya kusitisha matangazo ya bunge ilikuwa ni garama je Garama unazotumia kwa mwaka wewe kuwa live zinalipwa na nani kama sio kodi za watanzania?...........
Unapata wapi nguvu ya kutumia kodi zetu kwa kutafuta publicity wakati hoja za msingi kama Maji,Umeme, madawa ya kulevya vinajadiliwa kimya Bungeni ?
Mh Rais Kwanini wewe haulipi kodi mpaka Leo wewe ni kama nani unataka watu walipe kodi wakati umeshindwa kugusa hata mshahara wako kulipa hata hiyo 9%?..........
Kweli umeamua kuwageuza watanzania wote wajinga kuwafanya wazoee shida zao kwa kuwafanya mazuzu na wapumbavu kwa kutumia uelewa wao Mdogo na elimu yao ndogo?.............
Masikini Tanzania umekuwa nchi isiyo salama kwa wote wenye fikra pinzani ....
Zitto kawa mkimbizi na watanzania wamezoea.....
Lema kawa mfungwa asiyejua hatma Yake na watanzania wamezoea........
Lissu kawa Mtu wa kukanatwa kila siku na watanzania wamezoea ........
Lakini nikwambie tu ukweli hautofanikiwa kuwafumba midomo watanzania wenye uelewa wa mambo tutaendelea kuhoji mpaka pale haki ya msingi ya Uhuru wa habari itajapokuwa haki yetu maana ipo kikatiba .........
Hao wanaokushangilia ndio wanakuzika na ninapomaliza kuandika tu hapa wanakuja hapo chini kuingiza hoja za kipuuzi kama kumuongelea Lowassa...