Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 34,059
- 79,412
RAIS NI MPAKWA MAFUTA WA MUNGU LAKINI VIPI ANAPOASI?
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.
1. Kwa wasomi na wanazuoni wa theolojia hasa kwenye Biblia na Quran mtakubaliana na mimi kwenye jambo hili.
2. Mungu alitumia mbinu ya kuwapaka mafuta aina ya watu wafuatao;
a) Wafalme
b) Makuhani
c) Manabii.
3. Kupakwa mafuta ni kiashiria kuwa Mungu amekupa kibali cha kuongoza Watu hasa kwa level ya kitaifa. Yaani taifa.
4. Kuongoza taifa na kupakwa mafuta na Mungu ni heshima ya kipekee ambayo huwapata wachache sana.
5. Katika maisha yako, hata ufanye jitihada gani huwezi lazimisha Mungu akupake mafuta yaani uwe masihi. Mungu ndiye huchagua watu wakupaka mafuta.
6. Rais yeyote unayemuona Duniani ni Masihi. Mpakwa mafuta. Bila kujali anaongoza kwa namna ipi.
7. Tukieleza mambo ya kina mfalme Sauli au Mfalme Daudi unaweza usiyaelewe.
Chukulia mfano kwa hapa Tanzania, Magufuli au huyu Samia.
8. Ukimuita Leo Samia suluhu umwambie kama aliwahi kudhani atakuwa Rais ninauhakika atakuambia hakuwahi kufikiria na hata uwezo wa kufanya mafekeche ili awe Rais hakuwa na huo uwezo.
9. Kuna watu tulifikiri wangeweza au kustahili kuwa Rais mfano Hayati Lowasa lakini licha ya jitihada zote lakini ilishindikana.
10. Kirahisi sana, Samia Hasani Suluhu kwa sasa ndiye Mpakwa mafuta. Yaani kura ya Mungu imeangukia kwake.
Unafikiri ni watu wangapi nchi hii wanasifa kumzidi Samia lakini hawajawa Rais. Wapo! Wengi tuu! Lakini Mpakwa mafuta hazingatiwi kwa sifa tunazotumia mimi na wewe.
Hata Daudi hakuwa na sifa kuwazidi Kaka zake Saba, yeye akiwa wa nane. Lakini Mungu alimchagua na akampaka mafuta.
11. Kumaanisha kwa hapa Tanzania, samia ndiye Namba moja kimwili na kiroho. Yaani yeye ndiye mtawala.
12. Kuwa masihi wa Mungu(mpakwa mafuta) ni jambo kubwa na lenye heshima lakini pia linahitaji uangalifu mkubwa kuliendea na kutekeleza majukumu.
13. Rais au mfalme ni mungu mdogo kwa level ya kitaifa na sio kimataifa.
14. Ni jukumu la Rais kutenda kazi ya Mungu kwa uangalifu sana kwa sababu hesabu yake ni kubwa.
Ukipewa vikubwa unadaiwa vikubwa.
Ukipewa vidogo unadaiwa vidogo
15. Kila mara nazungumzia jambo hili. Na sitachoka kulisema kila nikipata nafasi.
16. Mambo makuu yanayomfanya Rais aonekane ameasi mbele ya Mungu. Yaani kaacha Job descriptions yake kama mpakwa mafuta;
a) Kuua wasio na hatia;
Katika vitu Rais anatakiwa awe makini sana ni suala la mauaji. Ni kweli kabisa ni ngumu kuongoza dola bila kuua ngumu sana. Yaani kama huwezi kuua ni kwamba huna sifa za kuwa mtawala.
Lakini unamuua nani, kwa sababu zipi hilo ndilo la muhimu kabisa.
Kuua mtu asiye na hatia ni kujiingiza kwenye ugomvi na aliyekupaka mafuta. Ni kwenda kinyume na kazi uliyopewa.
Daudi alipomuua mume wa Uria mambo yake yalianza kumuendea Kombo. Yeye mwenyewe alijua amekosea licha ya kuomba toba lakini ile dhambi ilimuandama sana.
b) Kujitukuza na kujifanya wewe ni Mungu.
Ni kweli wewe ni Rais na mtawala unahitaji kuheshimiwa. Lakini sio kuabudiwa.
Kuabudiwa ni nafasi ya Mungu mwenyewe.
Kupinga kukosolewa hata kama ni kwa heshima.
Kutaka kusifiwa na kuitwa majina yenye sifa za kiungu alafu unachekelea. Hapo lazima moto uwashwe. Mrejee Farao, Nimrodi, Nebukadreza, na belteshaza. Hao wote ni wafalme waliotaka kujifanya Mungu.
17. Ni kweli hata iweje serikali za kibinadamu haziwezi kukosa kasoro. Ndio ubinadamu na tulitaka wenyewe kujiongoza.
Lakini lazima Rais kama muwakilishi wa Mungu ahakikishe kwa uwezo wake wote HAKI inafanyika.
18. Ni kweli kabisa Mungu ndiye analeta utisho ndani ya mioyo ya watu ili wamheshimu Mtawala aliyempaka mafuta.
Na ni kweli kabisa Mungu huyo huyo akikukataa walewale watu unaowaongoza na wanaokulinda anaweza kubadili roho zao na kuzifanya ziasi.
19. Unapoongea na Rais lazima ujue unaongea na Mtu aliyepewa nafasi kubwa sana hivyo ni muhimu kumheshimu.
19. Na kama anafanya mambo ya hovyo. Ni muhimu kumkosoa na kumrekebisha kwa heshima bila kumtoa upako wake.
20. Ni jukumu la Rais kutafuta watu sahihi wakumshauri na kumsaidia kazi yake ili aitende kwa Haki na uaminifu.
Rejea kisa cha Nebukadreza alivyoingizwa mlenge(danganywa) kwahila na baraza la mawazi na maliwali na kumsokomeza Nabii Daniel kwenye Tundu la simba.
So wasaidizi wa Rais au mtawala wasipokuwa waaminifu huweza kusababisha Rais au mtawala asiwe mwaminifu.
21. Tupoelekea kwenye uchaguzi ni muhimu kila jambo liendeshwe kwa uangalifu na haki ili mambo yaende sawasawa.
22. Ni muhimu kwa wasaidizi wa Rais, wakuu wa vyombo vya usalama. Kutumia mbinu za akilli na hekima, kumwomba Mungu awaongoze mnapodili na kesi tata au wananchi watundu na wakorofi. Ili kuzuia damu kumwagika.
Damu ya mtu haifukiwi na mchanga. Hasa mtu asiye na hatia.
23. Ni kweli hakuna ufalme usiotoka kwa Mungu. Ni kweli kabisa kwa sababu illi uwe mfalme lazima Mungu akupake mafuta.
Sasa kuongoza vibaya au vizuri ni utashi wa mpakwa mafuta.
Kufikia hapo sina la ziada.
Taikonmaster
Kwa sasa Dar es salaam.