Habari zenu wote watanzania wenzangu. Pamoja na matukio mbalimbali yanayotokea katika taifa letu kwa sasa, tuna kila sababu ya kujiuliza vitu viwili ama vitatu kuhusu Rais wetu Mpendwa Mhe John Pombe Magufuli.
Mosi, Rais ni binadamu kama binadamu wengine na bila shaka ana nyama na damu kama binadamu wengine. Katika muktadha huo, naweza kusema kwamba matukio yanayotokea katika nchi yetu, serikali yake kwa asilimia 60% haihusiki. Mheshimiwa Magufuli ni mtu ambaye kama binadamu, ana huruma kama walivyo wanadamu wengine. Pia Mheshimiwa Magufuli na serikali yake wana damu na nyama kama binadamu wengine walivyo, na hivyo basi nadiriki kusema tusipende kuituhumu serikali mpaka pale itakavyodhibitika kwamba kweli ni serikali inahusika na haya matukio kwa namna moja au nyingine.
Sisi sote ni watanzania, Je serikali tukufu ya Magufuli itakubali kuwa ni ya kwanza kwa historia ya kumwaga damu za watu wasio na hatia?? sidhani kama lengo ni hilo. kwa sasa naiomba serikali yangu ishirikiane na watanzania wote kujaribu kutafuta namna ya kukabiliana na matukio haya.
Pili, Rais wetu pamoja na watendaji wake wana hofu ya Mungu(ni wacha Mungu), Je haogopi ya kwamba kila tendo baya juu taifa letu na watu wake watakuja kuulizwa???? kweli tumefika mahala pa kupotezana kirahisi namna hiyo kama vile mtu anavyodondosha karatasi barabarani? HAPANA.
Tatu, Mheshimiwa wangu Rais, dhamira yako ya kuleta maendeleo kwa watanzania ni dhahiri na hakuna anayekupinga kwa hili. Pamoja na dhamira hii, tunawahitaji watanzania wote zaidi ya tunavyowahitaji wanaccm peke yao. Nafahamu kabisa hakuna mtu anayeweza kwa Tanzania kushika dola ama kupata nyasifa yeyote bila chama. Na kwa mantiki hiyo, na kama ulivyojinasibu kuwa huna chama, ungana na wananchi wote bila kujali chama, bila kujali anayekukosoa kwani kukosolewa ni sehemu ya kufanya vizuri zaidi. Kwanini usikosolewe Mheshimiwa wangu Rais na ndipo utakapojua pa kurekebisha serikali yako.
WATANZANIA, mimi kwa kweli hasa wanajukwaa, tuikosoe Serikali yetu kwa staha. mtoto anapomkosea babake adabu, hana budi kufundishwa adamu. Sasa hapa katika kufundishwa adabu ndipo tuanapohitaji baba achague aina ya fimbo ya kumchapia mtoto ili ajirekebishe.
NISIWACHOSHE SANA !!!!!