Rais ni binadamu, Rais ana hofu ya Mungu, twende naye taratibu atatuelewa wananchi wake

engijape

Senior Member
Nov 8, 2014
178
97
Habari zenu wote watanzania wenzangu. Pamoja na matukio mbalimbali yanayotokea katika taifa letu kwa sasa, tuna kila sababu ya kujiuliza vitu viwili ama vitatu kuhusu Rais wetu Mpendwa Mhe John Pombe Magufuli.

Mosi, Rais ni binadamu kama binadamu wengine na bila shaka ana nyama na damu kama binadamu wengine. Katika muktadha huo, naweza kusema kwamba matukio yanayotokea katika nchi yetu, serikali yake kwa asilimia 60% haihusiki. Mheshimiwa Magufuli ni mtu ambaye kama binadamu, ana huruma kama walivyo wanadamu wengine. Pia Mheshimiwa Magufuli na serikali yake wana damu na nyama kama binadamu wengine walivyo, na hivyo basi nadiriki kusema tusipende kuituhumu serikali mpaka pale itakavyodhibitika kwamba kweli ni serikali inahusika na haya matukio kwa namna moja au nyingine.

Sisi sote ni watanzania, Je serikali tukufu ya Magufuli itakubali kuwa ni ya kwanza kwa historia ya kumwaga damu za watu wasio na hatia?? sidhani kama lengo ni hilo. kwa sasa naiomba serikali yangu ishirikiane na watanzania wote kujaribu kutafuta namna ya kukabiliana na matukio haya.

Pili, Rais wetu pamoja na watendaji wake wana hofu ya Mungu(ni wacha Mungu), Je haogopi ya kwamba kila tendo baya juu taifa letu na watu wake watakuja kuulizwa???? kweli tumefika mahala pa kupotezana kirahisi namna hiyo kama vile mtu anavyodondosha karatasi barabarani? HAPANA.

Tatu, Mheshimiwa wangu Rais, dhamira yako ya kuleta maendeleo kwa watanzania ni dhahiri na hakuna anayekupinga kwa hili. Pamoja na dhamira hii, tunawahitaji watanzania wote zaidi ya tunavyowahitaji wanaccm peke yao. Nafahamu kabisa hakuna mtu anayeweza kwa Tanzania kushika dola ama kupata nyasifa yeyote bila chama. Na kwa mantiki hiyo, na kama ulivyojinasibu kuwa huna chama, ungana na wananchi wote bila kujali chama, bila kujali anayekukosoa kwani kukosolewa ni sehemu ya kufanya vizuri zaidi. Kwanini usikosolewe Mheshimiwa wangu Rais na ndipo utakapojua pa kurekebisha serikali yako.

WATANZANIA, mimi kwa kweli hasa wanajukwaa, tuikosoe Serikali yetu kwa staha. mtoto anapomkosea babake adabu, hana budi kufundishwa adamu. Sasa hapa katika kufundishwa adabu ndipo tuanapohitaji baba achague aina ya fimbo ya kumchapia mtoto ili ajirekebishe.

NISIWACHOSHE SANA !!!!!
 
Binafsi ukisema tu eti ana dhamira ya kutuletea maendeleo sikuelewi kabisa, analeta maendeleo toka wapi?? Pesa zetu alete maendeleo si chato ingeendelea kitambo na hapo ndo tunawatukuza bila kujua...wao wakae na sisi kwa amani na utulivu tupange na kuamua juu ya maendeleo yetu halafu wao ndo wasimamie kwa niaba yetu tuliyo yaamua! Sasa kuteka, kufunga, kununua wapinzani, fukuza na nyanyasa watumishi tulikubaliana wapi??
 
analeta maendeleo ya wanaokufa? tukio la lissu na saa nane hajawai betua mdomo wake. je bdugu zake na hawa watamuombea? je ndugu zao akina lissu, saa8, aziri siyo watz wa kumuombea yeye. angetoka adharani na kusema naomba mniombee ili maalamia yaliyotenda maovu tajwa niyakamate. kupiga mnwaaa tu kuwa tukuombee na una dhamira safi hakuna huku watu wanapotea, hakuna anayekuamini ata mmoja
 
Sema Rais wako Mpendwa sio rais wetu mpendwa na nani? Mbona mnapenda kuzinenea nafsi zingine uongo? Kiufupi tusitarajie huyu kiumbe anaweza kubadilika, maendeleo na viwanda tutaendelea kusikia kwa matelevision yao, ukija kwenye uhalisia wa mambo hakuna chochote kinachofanyika. Hakuna uongozi mbovu kuwahi kutokea kama huu
 
Nahisi unafanya utafiti kwasababu kama ni maoni hakuna hata cha kusema, nadhani una test capacity ya adrenaline za watu, sasa hapa kwa mfano tuchangie nini........?? Tusemeje yani ?? sawa lakini sawa tumekuelewa
 
Mpaka umefikia kuandika Ujumbe wako, basi ujue huyo mtu unayemzungumzia(kama ni mtu kweli) si mtu wa kawaida...mtu hatari yan, unayoyaandika ni kama unatamani angekuwa tofauti,
 
Habari zenu wote watanzania wenzangu. Pamoja na matukio mbalimbali yanayotokea katika taifa letu kwa sasa, tuna kila sababu ya kujiuliza vitu viwili ama vitatu kuhusu Rais wetu Mpendwa Mhe John Pombe Magufuli.

Mosi, Rais ni binadamu kama binadamu wengine na bila shaka ana nyama na damu kama binadamu wengine. Katika muktadha huo, naweza kusema kwamba matukio yanayotokea katika nchi yetu, serikali yake kwa asilimia 60% haihusiki. Mheshimiwa Magufuli ni mtu ambaye kama binadamu, ana huruma kama walivyo wanadamu wengine. Pia Mheshimiwa Magufuli na serikali yake wana damu na nyama kama binadamu wengine walivyo, na hivyo basi nadiriki kusema tusipende kuituhumu serikali mpaka pale itakavyodhibitika kwamba kweli ni serikali inahusika na haya matukio kwa namna moja au nyingine.

Sisi sote ni watanzania, Je serikali tukufu ya Magufuli itakubali kuwa ni ya kwanza kwa historia ya kumwaga damu za watu wasio na hatia?? sidhani kama lengo ni hilo. kwa sasa naiomba serikali yangu ishirikiane na watanzania wote kujaribu kutafuta namna ya kukabiliana na matukio haya.

Pili, Rais wetu pamoja na watendaji wake wana hofu ya Mungu(ni wacha Mungu), Je haogopi ya kwamba kila tendo baya juu taifa letu na watu wake watakuja kuulizwa???? kweli tumefika mahala pa kupotezana kirahisi namna hiyo kama vile mtu anavyodondosha karatasi barabarani? HAPANA.

Tatu, Mheshimiwa wangu Rais, dhamira yako ya kuleta maendeleo kwa watanzania ni dhahiri na hakuna anayekupinga kwa hili. Pamoja na dhamira hii, tunawahitaji watanzania wote zaidi ya tunavyowahitaji wanaccm peke yao. Nafahamu kabisa hakuna mtu anayeweza kwa Tanzania kushika dola ama kupata nyasifa yeyote bila chama. Na kwa mantiki hiyo, na kama ulivyojinasibu kuwa huna chama, ungana na wananchi wote bila kujali chama, bila kujali anayekukosoa kwani kukosolewa ni sehemu ya kufanya vizuri zaidi. Kwanini usikosolewe Mheshimiwa wangu Rais na ndipo utakapojua pa kurekebisha serikali yako.

WATANZANIA, mimi kwa kweli hasa wanajukwaa, tuikosoe Serikali yetu kwa staha. mtoto anapomkosea babake adabu, hana budi kufundishwa adamu. Sasa hapa katika kufundishwa adabu ndipo tuanapohitaji baba achague aina ya fimbo ya kumchapia mtoto ili ajirekebishe.

NISIWACHOSHE SANA !!!!!
Kwamba usituchoshe kwa sababu Unajua umeandika ujinga, mbona unatumia nyingi Sana kumsafisha?
Tafuta kazi ndugu, huyo mtu wako hiyo nafasi haimfai hata kidogo, hata yeye alishangaa kupewa ndo maana anaboronga hivyo.
 
Sema Rais wako Mpendwa sio rais wetu mpendwa na nani? Mbona mnapenda kuzinenea nafsi zingine uongo? Kiufupi tusitarajie huyu kiumbe anaweza kubadilika, maendeleo na viwanda tutaendelea kusikia kwa matelevision yao, ukija kwenye uhalisia wa mambo hakuna chochote kinachofanyika. Hakuna uongozi mbovu kuwahi kutokea kama huu
Ni Rais wako hata ukimkataa kwa sababu unaishi Tanzania.
 
Kwamba usituchoshe kwa sababu Unajua umeandika ujinga, mbona unatumia nyingi Sana kumsafisha?
Tafuta kazi ndugu, huyo mtu wako hiyo nafasi haimfai hata kidogo, hata yeye alishangaa kupewa ndo maana anaboronga hivyo.
Ndugu yangu, kwa hakika sitafuti kazi na sidhani kama amewahi kuhisi kama kuna mtu kama mimi. Cha msingi ni Ukweli.
 
ukitaka kujua Hana hofu ya Mungu kiasi gani, itisha press conference ya kukosoa utawala wake, acha kujikomba kwa binadamu kama wewe
Asante kwa mawazo yako na uko sahihi. Cha msingi usitumie matusi. Chuki haiwezi kudhiirishwa kwa matusi na kama unafikiri matusi ni majibu ni sawa kwa sababu ndivyo ulivyo mkuu.
 
Ndugu yangu, kwa hakika sitafuti kazi na sidhani kama amewahi kuhisi kama kuna mtu kama mimi. Cha msingi ni Ukweli.
Huo ukweli unauona wewe peke yako mkuu? Hebu tazama maoni ya watu kwenye mada yako kisha jitathimini upya utetezi wako kwa huyu mtu.
Kapeleka watu kusoma Korea na Ufaransa ili waweze kutudukua humu, yaani hataki kukosolewa wakati yeye ni binadamu tu, roho yake inatamani damu za watu
 
Asante kwa mawazo yako na uko sahihi. Cha msingi usitumie matusi. Chuki haiwezi kudhiirishwa kwa matusi na kama unafikiri matusi ni majibu ni sawa kwa sababu ndivyo ulivyo mkuu.
Msamehe bure mkuu ,kuna watu wameumizwa mno na huu utawala halafu wewe unatetea.
 
Back
Top Bottom