Rais na Mwenyekiti wa Chama

ikyenja

Senior Member
May 28, 2013
103
52
Amani iwe kwenu wadau.
Kwa muda sasa nimekuwa najiuliza mantiki au uhusiano wa dhana ya Chama kuisimamia serikali.
Ni pale ambapo chama cha siasa kinachounda serikali kinadai kuisimamia serikali ilihali kiongozi mkuu wa Chama hicho hicho ni mkuu wa serikali.
Hapo najiuliza huyu Rais wa nchi na Mwenyekiti wa Chama anasimamiwa na chama au yeye anasimamia Chama!!?
Hii ni kwa sababu mwenyekiti wa Chama ana madaraka makubwa, labda awe chini ya Kamati kuu ya Chama ili asimamiwe.

Mimi sina uwezo mzuri wa kujenga hoja, hivyo hitaji langu ni kuelezwa au kufafanuliwa.

Asanteni
 
Back
Top Bottom