Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,684
- 149,889
Ni yule ambaye;
1.Siku anaingia madarakani atatangaza mali na madeni yake hadharani na pia siku anatoka madarakani atatangaza mali na madeni yake.
2.Atatangaza hadharani mshahara wake na kuahidi kuupunguza ili kusiwe na gap kubwa baina ya mshahara na wa watumishi wengine wa umma.
3.Ataanzisha na kusimamia mchakato wa kufuta kinga ya Raisi kutoshitakiwa popote pale.
4.Atapeleka wanawe katika shule za serikali na kuto shariti kwa wateule wake wake wawe tayari kupeleka wanao katika shule za umma.
5.Ataifuta sheria ya magazeti ya mwaka 1976.
6.Atasimamia mchakato wa kufuta katiba inayopendekezwa na kuanzisha upya Bunge la katiba litakaloundwa na sheria mpya kabisa tofauti na ile ya awali.
7.Raisi kama sehemu ya Bunge atahakikisha Spika wa Bunge na Makamu wake hawatokani na wabunge wala chama chochote cha siasa
8.Raisi atakaefuta utaratibu wa kujengewa nyumba baada ya kustaafu.
9.Raisi atakaefuta utaratibu wa Raisi mstaafu kulipwa pensheni ya asilimia 80 ya mshahara wa Raisi alieko madarakani ikiwa ni pamoja na Makamu wa Raisi mstaafu na Waziri Mkuu mstaafu.
10.Raisi atakaeleta Sheria ya Kifungo cha Maisha kwa makosa ya matumizi mabaya ya madaraka, ufisadi,uhujumu uchumi,ujangili,kukata viungo Albino na kujihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya.
11.Raisi atakaefuta utaratibu wa Raisi kuteua Jaji Mkuu na majaji wengine wa Mahakamu Kuu na Mahakama ya Rufaa.
Huyu ndie Raisi nimtakae na nitaamunga mkono bila kujali anatoka chama gani hata kama ni CCM.