Rais muamshe usingizini DED wa Kilosa

Rais muamshe usingizini DED wa Kilosa

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2021
Posts
3,211
Reaction score
3,614
Natamani Rais angeniteua DED wa Kilosa au aipandishe hadhi Mikumi Mji kuwa Halmashauri ya Mamlaka ya Mji Mdogo yaani TC ili aniteue Mkurugenzi wake.

Kwanini nalisema hili?

1. Mikumi umekuwa mji mkubwa sasa hivi kiasi kwamba hata wilaya inastahili kuwa.

2. Kilosa ni kubwa kuliko Dsm lakini ina majimbo 2 tu ya uchaguzi wakati Dsm ina majimbo 9 na wilaya 5 jiji 1 na manispaa 4. Ukubwa wa Kilosa ni kilomita za mraba 14,918 sawa na maili za mraba 5,760. Ukubwa wa Dsm ni kilomita za mraba 1,393 sawa na maili za mraba 537.84.

3. Kilosa ina rasilimali nyingi kuliko Dsm.

4. 90% ya mapato ya Kilosa DC yanategemea upande wa Magharibi ya wilaya ambako Mikumi mji upo. Upande wa Mashariki ya wilaya palipo makao makuu ya wilaya ni zero-resourced.

5. Upande wa Magharibi ya wilaya ya Kilosa una yafuatayo:
a) Hifadhi ya wanyama.
b) Ufugaji.
c) Kilimo (biashara na chakula)
d) Madini ya mawe na kokoto
za Msolwa zilizojenga
miundombinu ya nchi.
e) Wakala wa Misitu.
f) Mapori ya akiba.

Kwanini DED wa Kilosa amesinzia usingizi?

Mikumi ina faida kijiografia kwa sababu ni makutano ya Kilosa, Morogoro, Kilombero na Kilolo.

Fursa ambazo DED wa Kilosa hazioni kwa miwani yoyote hadi labda asubirie Rais aone kwa niaba yake:-

1. Mikumi haina Hoteli za hadhi ya kitalii kwa maana ya nyota 3 na kuendelea.

2. Mikumi haina ukumbi mkubwa wa kisasa wa hoteli na sherehe.

3. Mikumi haina maduka makubwa ya bidhaa za kitalii na za kawaida.

4. Mikumi haina Hospitali ya hadhi ya wilaya.

5. Mikumi haina soko kubwa la bidhaa na mazao licha ya kuwa ukanda wa kilimo.

6. Mikumi haina mnada mkubwa wa mifugo licha ya kuwa ukanda wa ufugaji mifugo jamii ya wanyama na ndege.

7. Mikumi Mji umeelemewa na idadi kubwa ya malori yanayosubiri huduma ya mizani.

8. Mikumi Mji umeelemewa na idadi kubwa ya malori na magari yanayozuiwa na kikosi cha usalama barabarani kutosafiri usiku zaidi ya muda uliowekwa kisheria. Hali hii inazua msongamano kwenye barabara ya T1 (Tanzania One) kwa eneo hilo la Mikumi.

Hapa pana fursa kubwa ambayo macho ya DED hayaoni. Fursa hii ni kwamba DED angetenga eneo kubwa kabisa hapo Mikumi akajenga maegesho kubwa ili traffic ipungue kwenye barabara ya T1 na kwamba angeingizia council mapato mengi ya maegesho, maliwato na maduka kwenye eneo hilo.

Hii pia ingefanya Mikumi kuendelea kukuwa. Hivi sasa DED hawezi kukusanya mapato ya maegesho pembezoni mwa T1 kwa sababu ni eneo la Tanroads kisheria na barabara lazima iwe na reserve au service road (pembezoni) ambapo hapa huwezi kutoza vyombo vya usafiri kwa kuegesha eneo kama hilo kwa sababu service road ni haki ya mtumiaji wa barabara.

Rais nipe U-DED Kilosa au Mikumi nipabadilishe.
 
Mkuu, hizi teuzi zinakuja tu, wakati mwingine michongo na koneksheni pia vinahusika sana. Je, wewe kama wewe umeifanyia nini Kilosa? Au hapo ulipo tu mtaani kwako umefanya jambo gani ambalo tunaweza tukasema kweli unastahili?
 
Mkuu, hizi teuzi zinakuja tu, wakati mwingine michongo na koneksheni pia vinahusika sana. Je, wewe kama wewe umeifanyia nini Kilosa? Au hapo ulipo tu mtaani kwako umefanya jambo gani ambalo tunaweza tukasema kweli unastahili?
Viongozi 90% wameteuliwa ambao hawajafanya kitu kwa jamii kwa nguvu zao wenyewe. Huyo wa Kilosa alifanya nini kwanza?
 
Mikumi pana kilimo gani mzeebaba?
Eneojimbo la Mikumi kuna:-

1. Mahindi.
2. Viazi vitamu.
3. Mbaazi.
4. Miwa.
5. Alizeti.
6. Maharagwe.
7. Ufuta.
8. Maghimbi.
9. Viazi mviringo.
10. Mpunga.
11. Kundekunde (Legumes)
12. Mafenesi.
13. Maembe.
14. Ndizi.
15. Machungwa.
16. Mtama kwa wastan.
17. Ulezi kwa wastan.
18. Asali.
 
Natamani Rais angeniteua DED wa Kilosa au aipandishe hadhi Mikumi Mji kuwa Halmashauri ya Mamlaka ya Mji Mdogo yaani TC ili aniteue Mkurugenzi wake.
Konekshen unayo au?😅usijisumbue bloo maDED wengi sio wabunifu,wanafanya Bora liende.Wanashindwa kuelewa DED ni Kama CEO wa kampuni kubwa.
 
Kuna Ranchi ya Mkata, kilimo cha mpunga, kilimo cha Mkonge kuanzia Rudewa Batini mpaka Kimamba, Uchimbaji Ruby vijiji vya Kidong'we.

Mitaa ya Ilonga mpaka Kilosa Mjini kumejaa vyuo vya kati vya kilimo,maendeleo,ualimu na uuguzi.Pembezoni mwa barabara ya Dumila, Rudewa, Ilonga mpaka Kilosa town kumepoa ukipita njia ya kilosa ulaya mpaka Mikumi town huko ndio balaa poripori.
 
Back
Top Bottom