Rais Mstaafu Kikwete atunukiwa tuzo Kwa kuwapa kipaumbele Wanawake katika Uongozi

tatum

JF-Expert Member
Jan 16, 2018
5,786
4,490
DrKeMpcX0AAjzz4 (1).jpg

Rais Mstaafu Dr.Jakaya Kikwete ametunukiwa Tuzo ya Uongozi uliotukuka kutoka Taasisi ya Women Advacement for Economic and Leadership Empowerement Foundation (WAELE) huko Namibia kwa kutambua mchango wake kwa Kuwapa Wanawake Kipaumbele katika Uongozi.

-----
Rais Mstaafu Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ametunukiwa Tuzo ya Uongozi Uliotukuka na Taasisi ya Women Advacement for Economic and Leadership Empowerement Foundation (WAELE), kwa kutambua mchango wake kwa Kuwapa Wanawake Kipaumbele katika Uongozi.

Tuzo hiyo ilikabidhiwa na Waziri Mkuu wa Namibia, Mheshimiwa Saara Kuugongelwa katika Mkutano wa 8 wa WAELE uliofanyika tarehe 2-3 Novemba, 2018 jijini Windhoek ambao ulijadili "Nafasi ya Mwanamke katika Amani na Maendeleo Endelevu Afrika".

Rais Mstaafu Kikwete ameishukuru WAELE kwa tuzo hiyo na kwa kutambua mchango wake katika kusukuma agenda ya ushiriki wa wanawake katika uongozi.

Amesema kuwa, hakufanya hivyo kwa kutegemea kupata tuzo siku moja, bali alitimiza wajibu wake wa uongozi wa kuhakikisha kuwa wanawake wanapata nafasi za uongozi kwa kuwa ni haki yao na sio fadhila.

Aidha, amewashukuru wanawake aliowateua kaika uongozi kwa kutomuangusha katika madaraka aliyowapa.
 
View attachment 921224
Rais Mstaafu Dr.Jakaya Kikwete ametunukiwa Tuzo ya Uongozi uliotukuka kutoka Taasisi ya Women Advacement for Economic and Leadership Empowerement Foundation (WAELE) huko Namibia kwa kutambua mchango wake kwa Kuwapa Wanawake Kipaumbele katika Uongozi.
Mi-Chadema ni shida kweli kweli, hiyo hiyo ndiyo iliyokuwa ikimwandika kuwa ni kiongozi dhaifu, ameporomosha uchumi, ufisadi umeongezeka, anachekacheka. Leo hiyo hiyo michadema inaleta hoja kama hizi !!!! Mijitu mizima Ovyooooo
 
Anastahili; aliwaamini sana wanawake katika utawala wake kitu ambacho ni ishara ya mtu kwenda shule kuelimika na kustaarabika. Dalili moja kubwa ya kuelimika ni kustaarabika na kuthamini utu wa mtu mwigine.
 
Rais Mstaafu Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ametunukiwa Tuzo ya Uongozi Uliotukuka na Taasisi ya Women Advacement for Economic and Leadership Empowerement Foundation (WAELE), kwa kutambua mchango wake kwa Kuwapa Wanawake Kipaumbele katika Uongozi.

Tuzo hiyo ilikabidhiwa na Waziri Mkuu wa Namibia, Mheshimiwa Saara Kuugongelwa katika Mkutano wa 8 wa WAELE uliofanyika tarehe 2-3 Novemba, 2018 jijini Windhoek ambao ulijadili "Nafasi ya Mwanamke katika Amani na Maendeleo Endelevu Afrika".

Rais Mstaafu Kikwete ameishukuru WAELE kwa tuzo hiyo na kwa kutambua mchango wake katika kusukuma agenda ya ushiriki wa wanawake katika uongozi.

Amesema kuwa, hakufanya hivyo kwa kutegemea kupata tuzo siku moja, bali alitimiza wajibu wake wa uongozi wa kuhakikisha kuwa wanawake wanapata nafasi za uongozi kwa kuwa ni haki yao na sio fadhila.

Aidha, amewashukuru wanawake aliowateua kaika uongozi kwa kutomuangusha katika madaraka aliyowapa.
IMG-20181104-WA0014.jpeg
IMG-20181104-WA0011.jpeg
 
Mi-Chadema ni shida kweli kweli, hiyo hiyo ndiyo iliyokuwa ikimwandika kuwa ni kiongozi dhaifu, ameporomosha uchumi, ufisadi umeongezeka, anachekacheka. Leo hiyo hiyo michadema inaleta hoja kama hizi !!!! Mijitu mizima Ovyooooo
Na yule anaedai kuwa kamwachia hewa kila mahali naye ni Chadema.....!!?
 
Mi-Chadema ni shida kweli kweli, hiyo hiyo ndiyo iliyokuwa ikimwandika kuwa ni kiongozi dhaifu, ameporomosha uchumi, ufisadi umeongezeka, anachekacheka. Leo hiyo hiyo michadema inaleta hoja kama hizi !!!! Mijitu mizima Ovyooooo

Kwani kiongozi akiwa dhaifu hawezi kufanya jambo lolote zuri? Ridiculous. Hata Mzee Mwinyi alikuwa kiongozi dhaifu lakini aliifanyia nchi hii mambo mengi mazuri. Tatizo katika zama hizi kuna watu wameambukizwa roho mbaya kiadi hawataki hata kuona viongozi wa zamani wa nchi hii wakizungumziwa kwa uzuri wowote
 
Hongera kwake. Anastahili. Ilifikia hatua kwenye Serikali yake aliteua Waziri wa Fedha/Uchumi Mwanamke.. Speaker alipatikana Mwanamke... Achilia mbali nafasi za Ukuu wa Mikoa/Wilaya n.k.

Ingekuwa bado yupo madarakani, haters wangesema katunukiwa tuzo baada ya kuwapa ulaji mahawara wake!

That's how a Tanzanian mind operates..

Sad!
 
Uongozi wa awamu ya tatu ulipoingia madarakani ulikuta mambo mengi yamekwenda ndivyo sivyo lakini kwa sababu ya upeo mkubwa na kujua maana ya Uongozi hata sijui haukulamika wala kujisifu pale ulipofanikiwa vizuri tu. Badala yake ulifanya kazi kimya kimya na matokeo yamewabeba awamu zote zilizofuata. Uongozi unaolalamikia watangulizi wake na kutumia makosa yao kujijengea umaarufu ujue umepwaya sana.
 
Back
Top Bottom