Rais mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete ateuliwa kuwa Balozi wa heshima

Peter Dafi

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
389
272
KIKWETE ATEULIWA KUWA BALOZI WA HESHIMA.

KITUO cha Ufundi cha Kilimo na Maendeleo Vijijini (Technical Centre for Agricultural and Rural Cooperation, CTA) kilicho chini ya Umoja wa Ulaya (EU) chenye makao makuu mjini Wageningen, Uholanzi kimemteua Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete kuwa Balozi wa Heshima (Goodwill Ambassador) wa Maendeleo ya Kilimo katika Mabara ya Afrika, Karibiani na Pacific.

Katika barua iliyokabidhiwa na mjumbe wa Bodi ya CTA, Prof. Faustin Kamuzora, CTA wameainisha kuwa Dk. Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, ameteuliwa kwa kutambua mchango na juhudi zake katika kukiendeleza kilimo nchini Tanzania na barani Afrika.

Katika wadhifa wake huo mpya, CTA imemuomba Dk. Kikwete aweze kuiwakilisha katika makongamano ya kimataifa ambapo atazungumzia umuhimu wa kukiendeleza kilimo kwa ajili ya kutoa fursa ya ajira zenye staha na uhakika kwa vijana na wanawake katika nchi za barani Afrika, Karibiani na Pasifiki. Pia ataisaidia CTA katika kuandaa makala na kufanya mahojiano na waandishi wa habari katika nchi mbalimbali.

Dk. Kikwete amekubali uteuzi huo na kuahidi kushirikiana na CTA katika kutekeleza mambo ambayo ameombwa kuisaidiana na taasisi hiyo ambayo ni ya ushirikiano wa Umoja wa Ulaya na Kundi la nchi za Afrika, Karibiani na Pasifiki wenye makao makuu mjini Brussels, Ubelgiji.

Prof. Kamuzora ambaye pia ni Katibu Mkuu, Mawasiliano ni mjumbe wa Bodi ya CTA akiwakilisha nchi za ukanda wa Afrika Mashariki kwa miaka mitano tangu 2013 hadi 2018.
 
Ni vichekesho eti kwa kuendeleza kilimo Tanzania na bara la Afrika. Haya amkabidhi Magu hilo rungu la uenyekiti wa CCM.
 
Hizi jumuiya za mataifa binafsi sijawahi kuzielewa kamwe. any way jk hakikisha unakabidhi chama kwenye mikono salama ya mwenyekiti vinginevyo mtasaga meno huko mbeleni...
 
8e9u3503.jpg

bye bye mkuu.

swissme
 
KIKWETE ATEULIWA KUWA BALOZI WA HESHIMA.

KITUO cha Ufundi cha Kilimo na Maendeleo Vijijini (Technical Centre for Agricultural and Rural Cooperation, CTA) kilicho chini ya Umoja wa Ulaya (EU) chenye makao makuu mjini Wageningen, Uholanzi kimemteua Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete kuwa Balozi wa Heshima (Goodwill Ambassador) wa Maendeleo ya Kilimo katika Mabara ya Afrika, Karibiani na Pacific.

Katika barua iliyokabidhiwa na mjumbe wa Bodi ya CTA, Prof. Faustin Kamuzora, CTA wameainisha kuwa Dk. Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, ameteuliwa kwa kutambua mchango na juhudi zake katika kukiendeleza kilimo nchini Tanzania na barani Afrika.

Katika wadhifa wake huo mpya, CTA imemuomba Dk. Kikwete aweze kuiwakilisha katika makongamano ya kimataifa ambapo atazungumzia umuhimu wa kukiendeleza kilimo kwa ajili ya kutoa fursa ya ajira zenye staha na uhakika kwa vijana na wanawake katika nchi za barani Afrika, Karibiani na Pasifiki. Pia ataisaidia CTA katika kuandaa makala na kufanya mahojiano na waandishi wa habari katika nchi mbalimbali.

Dk. Kikwete amekubali uteuzi huo na kuahidi kushirikiana na CTA katika kutekeleza mambo ambayo ameombwa kuisaidiana na taasisi hiyo ambayo ni ya ushirikiano wa Umoja wa Ulaya na Kundi la nchi za Afrika, Karibiani na Pasifiki wenye makao makuu mjini Brussels, Ubelgiji.

Prof. Kamuzora ambaye pia ni Katibu Mkuu, Mawasiliano ni mjumbe wa Bodi ya CTA akiwakilisha nchi za ukanda wa Afrika Mashariki kwa miaka mitano tangu 2013 hadi 2018.
TUNAKARIBISHA MAONI YENU WALE CHUKI BINAFSI
 
Hizi jumuiya za mataifa binafsi sijawahi kuzielewa kamwe. any way jk hakikisha unakabidhi chama kwenye mikono salama ya mwenyekiti vinginevyo mtasaga meno huko mbeleni...
Hivi hizi jumuiya huwa zinatumia kigezo gani kumteua mtu kushika nyazifa zao? Hivi huwa wanatafuta ushauri kwa viongozi wa nchi husika au wanafanya kama wapendavyo wao.
 
.sasa kama aliyeteuliwa hajawai kukataa mualiko au teuzi yoyote unategemea nini?
 
Safi sana Mh Jakaya Mrisho Kikwete!

Lowasa huko aliko anatamani kujinyoga akisikia jinsi unavyo zidi kupaa!
 
Back
Top Bottom