Mzee wetu, Hazina yetu na baba wa Demokrasia wa Nchi hii Al Hajj Dr Ali Hassan Mwinyi wiki hii alitmiza umri wa miaka 92.
Binafsi natamani ningekuwa na remote control ya maisha nikarudisha umri wake kisha akarudi tena madarakani kutuongoza. Rais Mwinyi hakuwa Rais tuu bali akuwa ni Kiongozi na si Mtawala. Alitupenda sisi kama wanae na alikuwa sio tuu ni commander in Chief bali pia alikuwa ni comforter in chief.
Rais Mwinyi alipoingia maadarakani alikuta hali ya nchi ni mbaya sana. Nchi hiaikuwa na Tax base yoyote ile ya kuweka kukusanya kodi na vijiduka vichache vya wahindi. Alichokifanya Mzee wetu na hazina yetu ni kuwawezesha wananchi wawe na kipato, ili wenye kuanzisha biashara waanze, Then kisha uongozi wake ukatoa Tax Incentive kwa kutowatoza kodi ili Biashara zikomae, then walipopatikana watu wa kutosha wa kuwatoza kodi ndio kuwatoza kodi.
Mkapa alipoingia Madarakani angalau aliwakuta watu wachache ambao ni Taxable, ambao walipata utajiri wao kipindi cha Mwinyi. Mzee wetu na Hazina yetu Mwinyi hakuwa na Privilege hii, alikuta nchi hohehahe na wananchi hohehahe lakini alitujali na yote hii kwa sababu yeye mwenyewe alikulia kwenye familia ya hali ya chini sana na hivyo aliweza ku empathise na sisi wananchi wake.
Kwa machache tuu....
1. Alifungua uchumi wa solo huria (economic liberalisation); serikali ikaanza kujitoa kwenye uchuuzi; nchi ikatoka kwenye ujima kuelekea maendeleo ya kisasa.
2: Alisimamia mabadiliko ya kutoka mfumo wa chama kimoja kwenda vyama vingi bila hiana wala vitisho vya dola. Wapinzani waliruhusiwa kufanya mikutano yao ya ndani na nje bila woga
3: Hakuwahi kuangaishwa sana na "kelele za mlango"; kutafuta wachawi na wanaompinga.
4: Ni mtu muungwana sana, mnyenyekevu ambaye alijaribiwa sana lakini akabakia kama binadamu, akasamehe na kusahau; Hana visas wala mtimanyongo
5: Hakulewa madaraka na kujiona kama Mungu mtu.
6. Ni Kiongozi pekee duniani aliyewahi (kuchaguliwa) na wananchi kuongoza nchi mbili tofauti (Zanzibar na Tanzania).
7. Aliamini Maendeleo ya Watu kuliko Maendeleo ya Vitu.
8. Ndiye aliyetuletea TV Tanzania na kuvunja falsafa ya Nyerere kuwa kuangalia TV ni anasa
9.Ndiye aliyeruhusu wa Tanzania wave nguo mpya badala ya nguo za mitumba
10.Ndiye aliyeruhusu wa Tanzania kupiga mswaki kwa dawa za meno (colgate etc) bila woga wa kukamatwa na kufungwa
11. Ndiye aliyeruhusu watanzania kununua magari toka nje bila kuomba kibali (vilikuwa vinachukua 5yrs kuvipata)
12. Zama zake foleni ya Michele, Sembe na Sukari hazikuwepo
13. Kiongozi pekee nchi hii aliyefukuza baraza zima la mawaziri kazi kwa sababu ya incompetency yao
14. Aliruhuhusu Magazeti, TV, Radio binafsi na vilikuwa huru kisawasawa
15.Ndiye aliyeruhusu kuwepo kwa saluni za kunyoa nywele. Kabla tulikuwa tunanyolewa kwa mikono na wembe chini ya miembe
16. Ndiye aliyeruhusu wa Tanzania kwenda dubai kuchukua mzigo na kuleta nchini kufanya biashara.
17. Awamu yake Pesa ilikua nje nje na maisha yalikuwa mazuri sana kwa Mtanzania miaka hiyo
18. Kwenye elimu aliruhusi private school zisaidie serikali na makanisa na taasisi nyengineh zikaingia kusaidia elimu na kuondoa ukiritimba.
19. madaktari bingwa wengi walikimbia nchi zama nyerere angalau wakaanza kubaki zama za baba yetu Mzee Mwinyi baada ya maslahi yao kuanza kuangaliwa na hospitali kujengwa mpya na kuimarishwa.
20. alifungua kilimo na kwa mara ya kwanza nchi yetu iliweza kujitosheleza kwa chakula tangu 1970.
21. Alikuta wafanyakazi hoi na raia waloamrishwa kufunga mikanda...sijui kama mnajua hili la kufunga mikanda...ila aliifungua akasema tafuteni rizi za ziada muishi kama watu.
22. aliruhusu wananchi kufanya shughuli nyingine ya ziada baada ya saa zako za kazi, kwa kujiongezea kipato chako halal.
Nathubutu kusema kuwa kwa hapa tulikofika alofanya Mzee wetu na Hazina Yetu Al Hajj Ali Hassan Mwinyi hakuna anayemfikia hata mmoja