KAMUGUNGA
JF-Expert Member
- Mar 25, 2013
- 238
- 269
Mheshimiwa Rais naamini wewe ni msomaji mzuri wa mitandao ya kijamii hivyo uzi huu utapata kuusoma na kuufanyia kazi.
Nimesikia kesho unasafari ya kwenda Bukoba Manispaa kuwapa pole wahanga wa tetemeko. Sitii neno kwenye safari yako ya Bukoba.
Ninachoomba kutoka kwako ni wakati ukitokea Chato kwenye Bukoba pitia pale Halmashauri ya Wilaya ya Muleba ushuhudie uozo wa Halmashauri hiyo. Wilaya ya Muleba ni mojawapo ya Wilaya zilizofuja mabilioni ya miradi ya maendeleo na kuwaachia wananchi umaskini.
Wilaya hii imekuwa ikipata hati zenye mashaka lakini mambo yanafunikwafunikwa.
Wilaya hii ndiyo ambayo Diwani wa Chama cha Mapinduzi aliamua kujiuzuru kwenye kamati ya Fedha baada ya kushindwa kuvumilia uozo na ubadhirifu aliokuwa akishuhudia lakini matokeo yake aliandamwa mpaka alipoamua kufikisha kilio chake kwenye ofisi yako.
Wilaya hii imefuja miradi mikubwa na ya mabilioni ya maji kama Mradi wa Kata Buhangaza, Kyota Kata Kimwani, kata Mubunda na mingine mingi.
Wilaya hii inatumia mkandarasi mmoja mwenye kujisajiri kwa majina tofauti tofauti na aliwahi kutimuliwa na aliyekuwa naibu waziri wa TAMISEMI Mh Agrey Mwanri kwa kosa la kujenga nyumba za NHC chini ya kiwango na naibu waziri akaagiza asipewe kazi nyingine ya ukandarasi lakini huyu ndi mkandarasi wa kila mradi na miradi mingi inajengwa chini ya kiwango kabisa kabisa. Lakini anabebwa na uongozi na mbunge mmojawapo wa majimbo haya ya Muleba.
Mheshiwa Rais naamini watataka kukupitisha kimyakimya Muleba lakini okoa wananchi hawa kwa kupita pale Halmashauri na kutumbua kama utaona inafaa.
Uozo ni mwingi mno ukifika pale wananchi watakueleza. Karibu Muleba tunakuomba usipitilize Muleba.