Rais Magufuli, weledi unahitajika kwenye hili, ukivimba tunapasuka

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
6,236
15,602
Hichi ndo kipindi Rais anatakiwa kuonesha ukomavu wa fikra, weledi, na kufanya maamuzi ya manufaa. Baada ya tamko la USA jana ni dhahiri lazima serikali iseme kitu ama la ifanye maamuzi ya kimkakati.

Kama ingalikuwa sisi ni 'Russia' tungekwenda jino kwa jino (tungevimba), ikiwa na maana na sisi pia tungepiga travel ban kwa afisa yoyote wa USA mwenye ushawishi. Ila kwa sababu sisi sio 'Russia' yafaa Rais afanye tathmini ya ni vipi amezipokea hizi taarifa na ni vip anazifanyia kazi.

Busara kubwa kwa sasa ni viongozi wa serikali kujizuia kutoa maneno yoyote ya jazba dhidi ya USA. Kumtolea jazba ama kejeli USA litakuwa kosa moja kubwa sana kufanywa na utawala. Huwezi kuitolea jazba USA tena kwa tamko lililotolewa na Secretary of State 'Michael Pompeo' huko ni sawa na kucheza na moto na tukifanya hivo tutaungua.

Busara hapa ni kujishusha, Rais ajishushe ikibidi ili kuonesha ameguswa na tamko, amuondoe hata Makonda kwenye ukuu wa mkoa.

Kinyume na hapo, kuvimba maana yake ni kwamba tunaenda kuwa Zimbabwe mpya. Ukweli usemwe kwa reserve hii ya Dola bilioni 5 hapo BOT tukipigwa sanction leo uchumi wetu hauta survive hata miezi 4. It will be dead than abyss.

Rais na serikali yako, toa tamko.. jishushe jishushe jishushe jishushe ukivimba Tanzania itapasuka.
 
Wenye jukumu la kuwaondoa madarakani hawa WAHUNI ni sisi Wananchi, Marekani ana taarifa zote za MAUAJI NA NAMNA YALIVYOFANYIKA. Akijaribu kuwaonesha JEURI wataanza kuwarushia CLIP MOJA MOJA TU za mauaji ya akina Saa Nane, Azory Gwanda na wengineo. Kama mnampenda MTUKUFU WENU mshaurini katika hili amevuliwa nguo, ACHUTAME TU.
 
Acha ajifanye mbishi, uchumi ukiporomoka akakosa mishahara ya wajeda na polisi itakuwa rahisi kumkamata na kumpa haki yake kwa Yale aliyowatendea wenzie.

Anadhani ile soft coup ya zimbabwe ilitokana na nini?
Na ndo vitu US huwa anavi target, wameshafanya research ya kutosha kuhusu Tz wakianza vikwazo vyao end product itakuwa ni mtu kufurushwa madarakani
 
Usije kuta yee na Bashite wake wamejifungia kwenye kachumba kadogo sasaivi wakipanga mipango ya kumteka POMPEO..!!!
Madhara ya kuongozwa na wehu ndio yanaonekana dhahiri sasaivi.
Intelligence ya US pia sio ya kitoto.. mnaweza kuwa mnapanga mnapigiana ma simu kumbe US yupo tu anawaangalia. Aisee hawa watu ni nyoko. Usidhani utapanga kitu US asijue
 
Wenye jukumu la kuwaondoa madarakani hawa WAHUNI ni sisi Wananchi, Marekani ana taarifa zote za MAUAJI NA NAMNA YALIVYOFANYIKA. Akijaribu kuwaonesha JEURI wataanza kuwarushia CLIP MOJA MOJA TU za mauaji ya akina Saa Nane, Azory Gwanda na wengineo. Kama mnampenda MTUKUFU WENU mshaurini katika hili amevuliwa nguo, ACHUTAME TU.
Umeongea point sana ila kuna mambumbu bado ndo huwa wanatulet down sana
 
Back
Top Bottom