Rais Magufuli: Wasumbufu wa sukari hawazidi 10, nitapambana nao

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
jpm.jpg

Rais John Magufuli ametangaza kupambana na wafanyabiashara wasiozidi 10 waliohodhi biashara ya sukari, akisema ndiyo wameshiriki kuua viwanda na kujitajirisha.

"Wafanyabiashara hawa walinunua viwanda vya NMC wakafungua mashine na kwenda kuuza Msumbiji na wakisimama utawasikia CCM oyee," alisema.

Aliongeza, "Utakuta Watanzania tunaendeshwa na wafanyabiashara kati ya watano au kumi tu, ukienda kwenye sukari ni haohao, walioua viwanda ni haohao, nawahakikishia nitalala nao mbele hadi mwisho," alisema.

Alisema kwa sasa kila Serikali inapojitahidi kufanya mambo ya maendeleo kuna watu wanataka kukwamisha, lakini kamwe hawatashinda. Alisema biashara ya sukari ni kama dawa ya kulevya, kuna kikundi cha watu ndiyo wanafanya biashara hii, wanakaa wanapanga leo tunatoa kiasi fulani leo hatutoi na wamekuwa wakienda Brazil kuchukua sukari iliyomaliza muda wake na kuileta nchini.

"Wanakwenda kuchukua sukari ambayo imekaribia kumaliza muda wanaileta wanawauzia Watanzania, ndiyo sababu nasema wafanyabiashara wa aina hii nitapambana nao, wawe CCM, wawe Chadema, kwangu mimi ni mkong'oto tu," alisema.

*Mbinu mbadala*

Rais alisema kutokana na hali ya biashara ya sukari sasa, ndiyo sababu anashauri wakurugenzi wa mifuko ya hifadhi ya jamii, kufanya biashara ya sukari ambayo ni ya faida kubwa na faida ya haraka.

"Njooni muombe vibali na kwenda kununua sukari na tutawapa ili kuja kuuza kwa Watanzania wakiwamo wanachama wenu. Alisema sukari inaweza kununuliwa nje kwa bei nzuri na inaweza kuja kuuzwa hapa nchini hadi kwa Sh800 kwa kilo, tena sukari ambayo ni bora.

Source: Mwananchi
 
Rais wangu unajiandalia makazi ya kudumu ndani ya mioyo ya watanzania, kama hutorudi nyuma na hii kasi yako ipo siku tutaanza kukuombea utangazwe mtakatifu kwa haya unayoyafanya hata kama utakua umekufa ila unayoyatenda hayatasahaulika vizazi na vizazi. Hao watu walikua untouchable.
 
Ni kweli mkuu ila awe makini na washauri wake
 
Rais alisema kutokana na hali ya biashara ya sukari sasa, ndiyo sababu anashauri wakurugenzi wa mifuko ya hifadhi ya jamii, kufanya biashara ya sukari ambayo ni ya faida kubwa na faida ya haraka.
"Njooni muombe vibali na kwenda kununua sukari na tutawapa ili kuja kuuza kwa Watanzania wakiwamo wanachama wenu. Alisema sukari inaweza kununuliwa nje kwa bei nzuri na inaweza kuja kuuzwa hapa nchini hadi kwa Sh800 kwa kilo, tena sukari ambayo ni bora.

Yaani naungana na Raisi.Pesa za mifuko ya jamii zinatakiwa kuwa zinazalisha faida kubwa na faida inapatikana haraka.Wajitose haraka kwenye hii biashara.Na wawashauri wastaafu au wanaostaafu walioko mikoa mbalimbali kufungua maghala ya kusambaza sukari kupitia pesa zao za kustaafu ili wawe maajenti wa kusambaza sukari maeneo yao walipo.Hii itawasaidia kuongeza kipato chao baada ya kustaafu pia.

Hii mifuko ichangamke kushika biashara kubwa zenye faida kubwa.Wana hela waweza kamata soko lote la sukari wakitaka.
 
Kuna watu ukiwagusa basi nchi haitatawalika " by waziri mkuu mmoja " nadhani ndo hawa anao wataja Raisi... pambana nao mkuu wetu....
 
Rais wangu unajiandalia makazi ya kudumu ndani ya mioyo ya watanzania, kama hutorudi nyuma na hii kasi yako ipo siku tutaanza kukuombea utangazwe mtakatifu kwa haya unayoyafanya hata kama utakua umekufa ila unayoyatenda hayatasahaulika vizazi na vizazi. Hao watu walikua untouchable.
Ni kweli aisee, watu 10 wanaitia nchi jamba jamba maisha magumu kila kitu hakikamatiki.

Wananunua sukari iliyo expired halafu wanaleta kuuza Tshs 3,000 kwa kilo wakati kumbe bei hata Tshs 800 haifiki??
 
Duh! Huyu Ngosha amekuwa tishio mno kwa wafanyabiashara walanguzi. Na kwa kweli wana kazi.Muda utasema.

Wafanyabiashara wanaotishia nyau serikali wajiandae kufilisika.

Magufuli alijiandaa kushika nchi hakukurupuka.Ni mwanamikakati makini ambaye huwezi msoma ukamjua akiwa huku atatokea wapi kwenye jambo fulani.Wale wanaombeza wakae chonjo Magufuli ni namba ingine hasomeki.
 
Nasubiri apewe chama nione kama makada na wanasiasa waliofanya dhambi watatumbuliwa maana tusubiri!
Anaweza kuwatifua tifua sana tu.

Juzi kamdindia JK kwenye katibu wa wabunge, alitaka kumpitisha jamaa yake Ngosha akadinda leo Mbunge yule wa Bukoba ndiye kachaguliwa.

Halafu inavyoonekana wazee wa chama wanampa sapoti kubwa sana ndani ya Chama.
 
jpm.jpg

Rais John Magufuli ametangaza kupambana na wafanyabiashara wasiozidi 10 waliohodhi biashara ya sukari, akisema ndiyo wameshiriki kuua viwanda na kujitajirisha.

"Wafanyabiashara hawa walinunua viwanda vya NMC wakafungua mashine na kwenda kuuza Msumbiji na wakisimama utawasikia CCM oyee," alisema.

Aliongeza, "Utakuta Watanzania tunaendeshwa na wafanyabiashara kati ya watano au kumi tu, ukienda kwenye sukari ni haohao, walioua viwanda ni haohao, nawahakikishia nitalala nao mbele hadi mwisho," alisema.

Alisema kwa sasa kila Serikali inapojitahidi kufanya mambo ya maendeleo kuna watu wanataka kukwamisha, lakini kamwe hawatashinda. Alisema biashara ya sukari ni kama dawa ya kulevya, kuna kikundi cha watu ndiyo wanafanya biashara hii, wanakaa wanapanga leo tunatoa kiasi fulani leo hatutoi na wamekuwa wakienda Brazil kuchukua sukari iliyomaliza muda wake na kuileta nchini.

"Wanakwenda kuchukua sukari ambayo imekaribia kumaliza muda wanaileta wanawauzia Watanzania, ndiyo sababu nasema wafanyabiashara wa aina hii nitapambana nao, wawe CCM, wawe Chadema, kwangu mimi ni mkong'oto tu," alisema.

*Mbinu mbadala*

Rais alisema kutokana na hali ya biashara ya sukari sasa, ndiyo sababu anashauri wakurugenzi wa mifuko ya hifadhi ya jamii, kufanya biashara ya sukari ambayo ni ya faida kubwa na faida ya haraka.

"Njooni muombe vibali na kwenda kununua sukari na tutawapa ili kuja kuuza kwa Watanzania wakiwamo wanachama wenu. Alisema sukari inaweza kununuliwa nje kwa bei nzuri na inaweza kuja kuuzwa hapa nchini hadi kwa Sh800 kwa kilo, tena sukari ambayo ni bora.

Source: Mwananchi
Huyu jamaa hatari ni pigo kwa sukari grabbers
 
Back
Top Bottom