tajirijasiri
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 2,863
- 3,851
Mh. Rais Magufuli, serikali yako imejipatia umaarufu kwa staili ya tumbua majipu. Wewe, Waziri Mkuu, Mawaziri na Wakuu wa Mikoa na Wilaya mmekuwa na tabia ya kuita vyombo vya habari na kufukuza watumishi wa umma kwa jina kutumbua majipu.
Basi kwa staili hiyo hiyo tena, anza sasa kuwapa motisha watumishi wako wanaofanya vizuri kazini, hazarani kwa mazuri wanayoyafanya, kwa staili ile ile ya kuitisha press ili watanzania wajue kuwa kuna mema wanayoyafanya watumishi wa umma.
Usipofanya hivyo, wananchi watabaki na picha moja tu kuwa watumishi wote wa umma ni wabaya. Hii itashusha ari ya kazi kwa watumishi wazuri na watakata tamaa. Hapo usitegemee ufanisi, kwani kwa hali ilivyo sasa, hofu imewatawala watumishi kuliko hata weredi (professionalism). Kila mmoja anafanya kazi kwa hofu.
RAIS MAGUFULI TOA MOTISHA HAZARANI KWA WATUMISHI WAZURI WANAOONESHA BIDII YA KAZI. INAWEZA KUWA TUZO AU CHETI AU HATA KUMSIFIA HAZARANI MBELE YA PRESS KWA STAILI ILE ILE YA TUMBUA MAJIPU.
KUNA NGUVU KUU YA KIUFANISI WA KAZI KATIKA KUSIFIA NA KUTOA MOTISHA HAZARANI.
NISIKILIZE NIELEWE.