Rais Magufuli wapatie wanafunzi walimu

Rais Magufuli wapatie wanafunzi walimu

gibishi

Senior Member
Joined
Aug 12, 2016
Posts
182
Reaction score
268
Kutokana na giza nene lililopo la ucheleweshaji wa ajira mpya Serikalini kutokana na kauli mbiu ya watumishi hewa kushika kasi na kutumika na serikali kama ngao ya kuchelewesha au kutotoa ajira mpya serikalini hadi sasa hasa katika sekta za vipaumbele, leo baada ya kutoka mjini Nzega, nimetembelea wilaya ya Igunga.

Safari yangu ilinifikisha katika kijiji cha *Mwamashiga* kilichopo kata ya Mwamashiga katika wilaya hiyo
Pamoja na mambo mengine nilikuwa nafanya utafiti mdogo juu ya huduma za afya vijijini pamoja na hali ya elimu nchini nikiwa nimechukua wilaya 5, katika mikoa mitatu kwa ufadhili wangu binafsi.

Pamoja na kutembelea zahanati kadhaa na shule kadhaa wilayani Igunga na kubaini mambo kadhaa kutokana na utafiti wangu mahususi, nimegundua kuwa hali ya upungufu wa walimu katika shule za Msingi na Sekondari ni kubwa sana kiasi kwamba watoto wa Masikini wanahudhuria shuleni na kurudi nyumbani bila kufundishwa.

Walimu waliopo ni Wachache kiasi kwamba wanaelemewa na mzigo na kujikuta wakiacha baadhi ya madarasa kutofundishwa kabisa.
Walimu katika shule za sekondari licha ya kuwa wachache pia, tatizo la walimu wa sayansi ni kubwa zaidi kiasi kwamba mwalimu wa sanaa mfano aliyesoma kiswahili na somo la Jiografia, analazimika kufundisha Biolojia au kemia ili walau watoto wapate msimamizi wa somo.

Baadhi ya mikoa, wanafunzi hawajasoma masomo ya sayansi tangu januari kifasaha kutokana na kukosa mtu wa kuwafundisha.

Shule za Msingi hali ni mbaya zaidi, walimu wachache, wanaishi katika mazingira Magumu huku masomo ya kufundisha yakiwa Mengi zaidi. Mfano katika Shule ya Msingi Mwamashiga wilayani Igunga, walimu waliopo kituoni wakifanya kazi kwasasa ni sita tu (06), huku idadi ya wanafunzi shuleni hapo ikiwa ni zaidi ya wanafunzi 500 ikiwa madarasa kuanzia la kwanza mpaka la saba.

Wakati nafika shuleni hapo nilikuta walimu wawili tu (02) huku wanafunzi wakipiga kelele madarasani bila kufundishwa huku wengine wakizagaa nje. Mkuu wa shule alikuwa safarini, mmoja akiwa ameshiriki mazishi ya mwanakijiji, na wengine wawili hawakutajwa waliko na Mwalimu niliyemkuta kituoni.

Kwa hali hii na kwa mfano huu mmoja utaona kuwa watoto wa Masikini wanateseka, hawana walimu, hawana msaada huku walimu wachache wakifanya kazi nzito iliyo nje ya uwezo wao.

Wakati hayo yakitokea, walimu wapo mtaani hawana ajira tangu mwaka jana huku serikali kupitia mawaziri wake wakiahidi kutekeleza ahadi ya kuajiri walimu bila mafanikio. Rais Magufuli naye aliahidi kuanza kuajiri baada ya miezi miwili lakini miezi miwili imepita bila mafanikio.

Rais wetu Mpendwa, waajiri sasa walimu na watumishi wa idara ya afya ili wawasaidie watanzania Wanyonge

Elizabeth Kapwani
Kapwani24@gmail.com
 
Halafu wanapandishiwa viwango vya ufaulu, kusoma masomo ya sayansi lazima! Wakifeli vilaza! Dah hii serikali inatia ukakasi
 
Tatizo LA Elimu Tanzania ,serikali inaamini imelitatua kwa madawati, eti hayo masuala mengine ni changamoto ndogondogo tu.Wako busy kuvunja UKUT 1st October
 
lakini mkuu anazifahamu fika changamoto za hizi shule make si ata yeye kasoma kwenye hizi shule, ajitahidi basi walau kuziboresha tu.
alafu nakumbuka enzi nasoma a level somo la GS tulikutana nalo kwenye mtihani wa mwisho tu so hatukuwahi fundishwa kabisa basi tulilifaulu kwa kulazimisha tu.
 
Ninacho cha kushauri serikali ila nachelea kukiandika hapa
Natamani ningekuwa na nafasi ya kusema huko serikalini....
 
hali ni ngumu sana ila kwakuwa sisi ni masikini tutazidi kuwa masikini hivi hivi labda tuivunje na kuiua fisie,m
 
Laiti kama na watoto wa vigogo wangekuwa wanasoma hizi shule kusingekuwa na changamoto kiasi hiki.
 
Sekta ya elimu ni janga kw taifa hili...serikali inatumia fimbo ya watumishi hewa kuwadhulumu na kuwakandamiza walimu achilia mbali kucheleweshwa kw ajira mpya za walimu. Walimu wanaostahilikupandishwa madaraja yao(promosheni) walidanganywa kufanyiwa hvo toka mwezi wa pili mwaka huu....hadi leo ni kitendawili kigumu kwao, hawana hata tumaini na wanakatishwa tamaa kw kweli. Jamani kwani ualimu una laana gani kwenye taifa hili??
 
Kutokana na giza nene lililopo la ucheleweshaji wa ajira mpya Serikalini kutokana na kauli mbiu ya watumishi hewa kushika kasi na kutumika na serikali kama ngao ya kuchelewesha au kutotoa ajira mpya serikalini hadi sasa hasa katika sekta za vipaumbele, leo baada ya kutoka mjini Nzega, nimetembelea wilaya ya Igunga.

Safari yangu ilinifikisha katika kijiji cha *Mwamashiga* kilichopo kata ya Mwamashiga katika wilaya hiyo
Pamoja na mambo mengine nilikuwa nafanya utafiti mdogo juu ya huduma za afya vijijini pamoja na hali ya elimu nchini nikiwa nimechukua wilaya 5, katika mikoa mitatu kwa ufadhili wangu binafsi.

Pamoja na kutembelea zahanati kadhaa na shule kadhaa wilayani Igunga na kubaini mambo kadhaa kutokana na utafiti wangu mahususi, nimegundua kuwa hali ya upungufu wa walimu katika shule za Msingi na Sekondari ni kubwa sana kiasi kwamba watoto wa Masikini wanahudhuria shuleni na kurudi nyumbani bila kufundishwa.

Walimu waliopo ni Wachache kiasi kwamba wanaelemewa na mzigo na kujikuta wakiacha baadhi ya madarasa kutofundishwa kabisa.
Walimu katika shule za sekondari licha ya kuwa wachache pia, tatizo la walimu wa sayansi ni kubwa zaidi kiasi kwamba mwalimu wa sanaa mfano aliyesoma kiswahili na somo la Jiografia, analazimika kufundisha Biolojia au kemia ili walau watoto wapate msimamizi wa somo.

Baadhi ya mikoa, wanafunzi hawajasoma masomo ya sayansi tangu januari kifasaha kutokana na kukosa mtu wa kuwafundisha.

Shule za Msingi hali ni mbaya zaidi, walimu wachache, wanaishi katika mazingira Magumu huku masomo ya kufundisha yakiwa Mengi zaidi. Mfano katika Shule ya Msingi Mwamashiga wilayani Igunga, walimu waliopo kituoni wakifanya kazi kwasasa ni sita tu (06), huku idadi ya wanafunzi shuleni hapo ikiwa ni zaidi ya wanafunzi 500 ikiwa madarasa kuanzia la kwanza mpaka la saba.

Wakati nafika shuleni hapo nilikuta walimu wawili tu (02) hukua wanafunzi wakipiga kelele madarasani bila kufundishwa huku wengine wakizagaa nje. Mkuu wa shule alikuwa safarini, mmoja akiwa ameshiriki mazishi ya mwanakijiji, na wengine wawili hawakutajwa waliko na Mwalimu niliyemkuta kituoni.

Kwa hali hii na kwa mfano huu mmoja utaona kuwa watoto wa Masikini wanateseka, hawana walimu, hawana msaada huku walimu wachache wakifanya kazi nzito iliyo nje ya uwezo wao.

Wakati hayo yakitokea, walimu wapo mtaani hawana ajira tangu mwaka jana huku serikali kupitia mawaziri wake wakiahidi kutekeleza ahadi ya kuajiri walimu bila mafanikio. Rais Magufuli naye aliahidi kuanza kuajiri baada ya miezi miwili lakini miezi miwili imepita bila mafanikio.

Rais wetu Mpendwa, waajiri sasa walimu na watumishi wa idara ya afya ili wawasaidie watanzania Wanyonge

Elizabeth Kapwani
Kapwani24@gmail.com
Hongera kwa utafiti, ila kuna jambo moja umesahau, ungefanya utafiti na shule za serikali zilizoko mjini!Kwa ufupi waalimu walikuwa wanahamia mjini kwa hila mbalimbali zikiwemo kuolewa au kuhonga!Hakuna uwiano wa mjini na kijijini!Maadam sasa ni kazi tu, naamini waalimu watakaopangiwa safari hii ama wasiende la sivyo hakuna nafasi ya kuhama!Afisa elimu/mkurugenzi atakayesign vibali vya uhamisho, atatafuta kazi ya kufanya maana hiyo itakuwa imemshinda
 
Waalimu wapo kwenye mgomo mamboleo, Ile hela waliyotumia kununua ndege 3 si zingetosha kuwalipa waalimu vizuri ili wafanye kazi kwa moyo wote?
 
Back
Top Bottom