RAIS MAGUFULI WAAGIZE CDA WAFANYE HIVI KUUPENDEZESHA MAKAO MAKUU DODOMA

tanzaniamoja

Member
Feb 12, 2015
8
4
kwanza kabisa napenda nikupongeze kwa agizo lako la kuagiza ifanyike tathmini kama kuna umuhimubwa kuwa na CDA...
Naamini kama hili wangeulizwa wananchi wa dodoma, asilimia 99.99 wangesema CDA ifutwe kabisa. CDA imekuwa kero kubwa na kushindwa kutoa huduma stahili kwa wananchi wa Dodoma.

Niende moja kwa moja kwenye Mada.
1) Kumekuwa na utaratibu wa CDA kupima viwanja na kuuza kwa wananchi kwa gharama kubwa mno. Viwanja hivyo bei yake kwa mwananchi maskini ikiwemo watumishi wa umma wa Tanzania hawezi kuimudu. Utakuta bei inaanzia 6,500 kwa sqm na kwenda juu.. Hii inazuia wananchi wengi wenye nia ya kuishi kwenye maeneo yaliyopangwa vizuri kushindwa kufanywa hivyo

pendekezo: Bei za viwanja ziangaliwe upya ili wanachi waweze kumudu gharama na kuishi kwenye makazi ya mpangilio.

2)
Size ya viwanja vinavyopimwa vingi huwa ni vidogo sana (high density) viwanja hivi vina ukubwa wa mita za mraba 600 na kurudi chini. Hasara ya kupima viwanja mojawapo ni ya kimazingira. watu wengi hurundikana eneo moja hivyo kuweka shinikizo kwenye miundombinu mbalimbali ya kijamii. Pili, na la msingi zaidi kwa ukubwa wa viwanja hivi mtu hujenga nyumba tu na hakuna hata nafasi ya kupanda mti hata mmoja.

pendekezo: vipimwe viwanja kuanzia size ya kati angalau mita za mraba 800 ili kuwezesha mwenye kiwanja kupanda miti nyumbani kwake. Na itungwe sheria kulazimisha kila mwenye kiwanja kupanda miti angalau mitatu kwenye kiwanja hicho. Na asiyefanya hivyo alipe fine kwa kiasi kitakachokubalika. Kwa namna hii mji wa dodoma utapendeza na kuwa wa kijani na utakuwa wa kuvutia sana.

Nawasilisha.
 
Cda ni jipu mbuge wa zamani malole kalia na cda lakini wameziba masikio hongera mh. Rais magufuli tuondolee cda
 
Back
Top Bottom