Brigedia Chan-ocha
JF-Expert Member
- Mar 7, 2014
- 1,353
- 2,846
Ili Kuondoa vitendo vya Ubadhirifu, Ukwepaji Kodi, Matumizi mabaya ya fedha za Umma, Nk. Nashauri Mh. Rais Atunge Sheria zenye adhabu kali Zaidi ambazo hazitakuwa na option ya adhabu na kesi zote zisichukue si Zaidi ya miezi 6.
Kwa mfano, mfanyabiashara akithibitika kukwepa kodi ya serikali apigwe faini ya sh. Milioni 300, pamoja na onyo kali la maandishi, adhabu hiyo itaenda sambamba na kampuni/shirika au biashara yake kuwa chini ya "Uangalizi Maalumu wa Wizara Husika pamoja na vyombo vya dola" kwa Mwaka mmoja.
Ikiwa Mfanyabiashara atarudia kosa hilo, Kiwanda, Taasisi, au kampuni yake itataifishwa rasmi na kuwa mali ya serikali na adhabu hiyo itaenda sambamba na kufilisiwa kwa mfanyabiashara huyo ili kufidia hasara aliyoisababishia serikali. hii ni kwa wenye "Makampuni, viwanda, na wafanyabiashara wote.
Kwa watumishi wa umma watakaothibitika kufanya ubadhilifu na kuisababishia serikali hasara, adhabu yao bila option iwe ni kukamatwa, kufilisiwa mali zake alizonazo na kuswekwa gerezani si chini ya miaka 10-15, kikosi maalumu kitakachoongozwa na Mkurugenzi mkuu wa Takukuru akishirikiana na Mkurugenzi wa TISS Pamoja na IGP kitachunguza kama mtumishi huyo ana mali alizoandika majina ya ndugu zake au majina ya kufoji, ikiwa itadhibitika Ndugu huyo aliyekubali jina lake litumike kuficha mali isiyo halali atafungwa jela si chini ya miaka 10-15 pamoja na kazi ngumu.
Yeyote atakayebainika kusaidia, kuzembea au kufumbia vitendo vya ubadhirifu wa mali za umma, ukwepaji kodi nk. adhabu yake ni kuachishwa kazi, kukamatwa, kushtakiwa na adhabu ni kufilisiwa mali zake na kifungo cha miaka si chini ya miaka 15-20 jela na kazi ngumu.
Vile vile, makosa haya hayatakuwa na msamaha wowote kutoka kwa Rais au mtu yeyote.
huu ndiyo mwarobaini wa Kuondoa mfumo wizi na ubadhirifu hapa nchini, hakuna namna nyingine kabisa.