Rais Magufuli usigeuke jiwe

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,024
2,000
KATIKA moja ya hotuba alizowahi kuzitoa Baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere, kuna ile ilizungumzia mtu aliyegeuka jiwe baada ya kuangalia nyuma kutokana na kelele nyingi za kumzomea.

Mwalimu katika hotuba hiyo, alikuwa anawapasha wale waliokuwa wakimpigia kelele na kumzomea kutokana na kuendeleza siasa yake ya ujamaa na kujitegemea aliyoiasisi.

Kama ninakumbuka vizuri, Mwalimu katika hotuba hiyo alisema kwamba, kijana mmoja aliyekuwa anafuata hazina yenye thamani iliyokuwa juu ya kilele cha mlima, litahadharishwa kabla kwamba anaweza akakifikia hazina hiyo, iwapo tu hatasikiliza kelele za kuzomea zomea ambazo atakumbana nazo.

Kwamba anachotakiwa kufanya yeye wakati akipanda mlima huo kuelekea kileleni ni kusonga mbele, bila kujali zomea zomea atakayokumbana nayo. Na akatahadharishwa kwamba kadri atakavyokuwa anakaribia kileleni, kelele za sauti ya zomea zomea ‘huyo, huyo huyo’ zitazidi kuongezeka, lakini hapaswi kamwe kuzisikiliza na badala yake aendelee bila kuangalia nyuma hadi aifikie hazina hiyo.

Aidha, akatahadharishwa kuwa, iwapo atageuka nyuma, basi atakuwa jiwe, na ndiyo utakuwa mwisho wa safari yake. Na kwa hiyo Mwalimu akasema, yeye kamwe hawezi kugeuka nyuma akawa jiwe.

Nimechukua maneno ya hotuba hiyo ya mwalimu kujaribu kuelezea ‘zomea zomea’ ambayo inaendelea sasa kutoka kwa baadhi ya wananchi, ikiwa ni pamoja na viongozi wa vyama vya siasa nchini dhidi ya msimamo wa Rais Dk. John Pombe Magufuli, kwenye masuala mengi ya kitaifa kwa hivi sasa.

Ni wazi kuwa walau kwa wenye macho ya kutazama na kuona mambo kama ilivyo kwa baadhi yetu, Tanzania sasa imepata Rais ambaye ana uchungu na maendeleo ya taifa na wananchi wake.

Aina ya Rais ambaye kwa walio wengi walikuwa wakimlilia kwa siku nyingi, mwenye msimamo ‘mkali’ kwa wale wanaohujumu mali za taifa kwa manufaa yao na jamaa zao. Hata wakati wa Mkuatano Mkuu wa CCM, Kikwete alisema, ''mlimtaka Rais mkali, tunawaletea yule mlimtaka''.

Kama Watanzania wana kumbukumbu, watajua namna suala la rushwa na ufisadi lilivyokuwa limetamalaki huko nyuma. Watajua namna watumishi wa umma, ambao walikuwa na dhamana ya kuwatumikia wananchi, jinsi walivyokuwa wametoka kwenye msitari na kuwa watawala, wakijiamulia mambo watakavyo.

Wakasahau kwamba wao ni watumishi wa wananchi, na si watawala kama ambavyo amekuwa akisisitiza Makamu wa Rais mama Samia Suluhu, kwa watumishi wa umma.

Kwamba kwa ujumla hali ilikuwa imefikia pabaya karibu kila mahali na hasa kwenye ofisi za serikali, kiasi cha watumishi wa umma kugeuka kama ‘miungu watu’ wakitaka kutumikiwa na wananchi, badala ya wao kutoa huduma kwa wananchi.

Watu walikesha wakiomba kwa imani zao, wakamulilia Mwenyezi Mungu, wapate rais atakayewajali, na ambaye atatanguliza mbele maslahi ya taifa, badala ya maslahi yake.

Na kweli tukampata Dk. Magufuli ambaye hadi sasa karibu miezi tisa ya kuwapo kwake madarakani, mwanga umeanza kuonekana. Na hii ni kutokana na hatua mbalimbali alizozichukua katika kipindi cha miezi hii michache, ambazo ‘wanaoona’ wanaweza kuziorodhesha vizuri tu.

Kwa uchache ninaweza kuzitaja baadhi ya hatua hizo ambazo zimetia matumaini. Hatua hizo ni pamoja na suala la kupambana na ufisadi, ukianzia na lile suala la makontena bandarini. Lakini pia udhibiti wa matumizi ya fedha za serikali kwa kukata safari za nje zisizo na tija, hatua iliyookoa na inaendelea kuokoa mamilioni ya fedha za umma.

Rais Magufuli akaja kwenye kazi yake aliyojipa mwenyewe ya kutumbua majipu, ambako tulishuhudia na tunaendelea kushuhudia katika kipindi hiki kifupi, akitumbua watu. Baadhi ya vigogo waliokumbana na utumbuaji huo, ni pamoja na wale waliokuwa wakiongoza taasisi mbalimbali, zikiwamo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Bandari (TPA) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Rais Magufuli amerudisha vilevile nidhamu ya watumishi wa umma katika suala zima la kuwahudumia wananchi, na hata katika uteuzi za wasaidizi wake, msisitizo mkubwa umekuwa ni uleule wa kunasibu wasaidizi wake hao kwenda kuwatumikia wananchi.

Rais Magufuli ameweza kufanya kazi kubwa ya kukusanya kodi, kwa lengo la kuwa na fedha za kutosha kugharimia miradi ya maendeleo kwa wananchi, ikitiliwa maanani kuwa katika Bajeti yake ya kwanza ya shilingi trilioni 29, asilimia 40 ya bajeti hiyo inakwenda kwenye miradi ya maendeleo.

Kwa hili vilevile, Mwalimu aliwahi kuliongelea katika moja ya hotuba zake, akionyesha kuwa serikali iliyoathiriwa na rushwa na ufisadi, kimsingi huwa haikusanyi kodi na hasa kutoka kwa matajiri.

Mwalimu akasema, hiyo inatokana na ukweli kuwa tayari matajiri huwa wamewaweka ‘kiganjani’ viongozi wa serikali na kwa hali hiyo, hujikuta hawana uthubutu wa kuweza kuwakabili.

Hali ilivyo kwa serikali hii ya Dk. Magufuli ni tofauti, kodi inakusanywa kwa kiwango cha kuvuka malengo yanayowekwa na serikali, huku ikisisitiza wote walipe kodi na hasa matajiri. Anafanya hivyo katika nia njema ile ile ya kupata fedha za kugharimia shughuli za maendeleo, ikiwa ni pamoja na suala la elimu bure kutoka shule ya msingi hadi kidato cha nne.

Na katika hili la kutoa elimu, tunaweza pia kumnukuu Mwalimu Nyerere, ambaye katika moja ya hotuba zake akiongelea namna ya kuwakomboa maskini na hasa watoto wa maskini.

Mwalimu alinukuliwa akisema kwamba, ‘ukitaka kumkomboa mtoto wa maskini, mpe elimu’ hatua ambayo ndiyo serikali ya Dk. Magufuli, inachokifanya kwa sasa.

Haya yote yanaonyesha kwamba kuna mwanga unakuja, na kwamba serikali ya Dk. Magufuli, iko katika msitari unaotakiwa. Sasa katikati ya mwelekeo huo mzuri unaoendelea kuonyeshwa na serikali hii ya awamu ya tano, tayari wameshaanza kujitokeza watu wanao mzomea zomea, ili ageuke jiwe. Kwamba asiendelee na safari yake ya kuifikisha nchi kwenye hazina iliyo kwenye kilele cha mlima, na hivyo kumkwamisha njiani.

Zomea zomea yao imejikita katika hoja ambazo zinaweza kujadilika, kwa kuangalia mbivu na mbichi zake. Kwa mfano katika hatua yake ya kutumbua majipu, walijitokeza baadhi ya watu wakiwamo viongozi wa vyama vya siasa, waliopinga jinsi alivyokuwa anawatumbua baadhi ya watumishi wa umma, kwa kigezo cha haki za binadamu.

Kwamba kwa mujibu wa mtazamo wao, Rais Magufuli alipaswa kwanza awachunguze na akishakuwa na uhakika wa tuhuma zinazowakabili, ndipo hatua ya kuwatumbua ichukuliwe.

Kwamba watumishi hao wapate nao muda wa kusikilizwa kama inavyoelekeza sheria ya asili (natural justice), na kama maelezo yao hayakutosheleza ndipo utumbuaji ufuate. Lakini zomea zomea nyingine inayoelekezwa kwa Dk. Magufuli tunayoweza kuizungumzia kwenye makala haya, ni ile ya kupiga marufuku mikutano ya vyama vya siasa kufanyika katika kipindi hiki.

Na hasa misemo yake ya kwamba ‘Uchaguzi umekwisha’ ‘Huu siyo muda wa kufanya siasa’ na ‘Huu ni muda wa kazi tu.’ Wengi na hasa vyama vya siasa vya upinzani, vinapinga kuzuiwa kufanya siasa wakati wote kwa kigezo kuwa katiba inawaruhusu.

Mhadhiri Mwandamizi wa Sayansi ya Siasa na Utawala, Profesa Mwesiga Baregu ni miongoni mwa watu wanaopingana na kauli hizo za rais, kuzuia vyama vya siasa kuendesha siasa wakati wote kwa msingi kuwa, siasa kwa vyama vya siasa ni sawa na hewa ya Oksijeni kwa binadamu.

Kwamba binadamu akikosa hewa ya oksijeni hata kwa dakika mbili, tatu anakufa, vivyo hivyo na kwenye vyama vya siasa zisipofanya siasa kwa muda wa dakika mbili ama tatu vitakufa.

Sasa hilo ni la mjadala hasa ikichukuliwa polisi wamesema hawajapiga marufuku mikutano ya kiutendaji naya kiutawala inayofanywa kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za vyama bali wamepiga marufuku mikutano ya hadhara na maandamano ya vyama vya siasa mpaka hali ya kiusalama itakapotengemaa.

Zomea zomea hii kwa Dk. Magufuli ukiiangalia kwa ndani kimsingi inalenga kumfanya geuke nyuma ili awe jiwe, na hivyo ashindwe kutufikisha kwenye hazina iliyoko kwenye kilele cha mlima.

Ni rai ya makala hii kwa Dk. Magufuli, kutogeuka nyuma kutokana na zomea zomea inayojitokeza hapa na pale dhidi ya msimamo wake wa kuipeleka nchi mbele, na badala yake akaze uzi, ahakikishe kuwa wembe ni ule ule. Hii ni kwa sababu tayari wananchi wameshaanza kuona mwanga kutokana na msimamo wake na serikali yake.

Pengine kwa wasiojua, kwa sasa hukuti watu wanaokunywa pombe ama kucheza ‘pool’ wakati wa kazi na hakuna mhudumu wa baa aliye tayari kuuzia mtu pombe kabla ya saa kumi jioni.
Chanzo: Kwa hisani ya Mwananchi.
 
wambeke

JF-Expert Member
Aug 30, 2013
2,656
2,000
Anasemaje? maana hata sijamuelewa. nimesoma weeeee hata sioni anachotaka. ila nimemuelewa tu hivyo hivyo.

ila ajue kuna siku Profesa Shivji aliwahi kutoa mhadhara pale Udsm akielezea sifa ya msomi. kuna jambo alisema sifa ya msomi ni kubadilika kutokana na mazingira. kwa hiyo Rais Magufuli asije ogopa kubadili misimamo yake kulingana na mazingira kisa anaogopa kugeuka Jiwe.
 
chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
4,894
2,000
Kwenye masuala ya maslahi mapana ya nchi flexibility, compromise ni muhimu, hasa pale ambako kuna situation ambapo wote mtapoteza, kuwa na msimamo ni muhimu lakini yafaa uangalie sometimes pia, ndivyo siasa na uongozi ulivyo
 
MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,024
2,000
Anasemaje? maana hata sijamuelewa. nimesoma weeeee hata sioni anachotaka. ila nimemuelewa tu hivyo hivyo.

ila ajue kuna siku Profesa Shivji aliwahi kutoa mhadhara pale Udsm akielezea sifa ya msomi. kuna jambo alisema sifa ya msomi ni kubadilika kutokana na mazingira. kwa hiyo Rais Magufuli asije ogopa kubadili misimamo yake kulingana na mazingira kisa anaogopa kugeuka Jiwe.
Wewe unaongelea usomi wakati mada inaongelea uongozi kulingana na mazingira.
 
Nshonzi

JF-Expert Member
Jul 19, 2016
2,978
2,000
KATIKA moja ya hotuba alizowahi kuzitoa Baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere, kuna ile ilizungumzia mtu aliyegeuka jiwe baada ya kuangalia nyuma kutokana na kelele nyingi za kumzomea.

Mwalimu katika hotuba hiyo, alikuwa anawapasha wale waliokuwa wakimpigia kelele na kumzomea kutokana na kuendeleza siasa yake ya ujamaa na kujitegemea aliyoiasisi.

Kama ninakumbuka vizuri, Mwalimu katika hotuba hiyo alisema kwamba, kijana mmoja aliyekuwa anafuata hazina yenye thamani iliyokuwa juu ya kilele cha mlima, litahadharishwa kabla kwamba anaweza akakifikia hazina hiyo, iwapo tu hatasikiliza kelele za kuzomea zomea ambazo atakumbana nazo.

Kwamba anachotakiwa kufanya yeye wakati akipanda mlima huo kuelekea kileleni ni kusonga mbele, bila kujali zomea zomea atakayokumbana nayo. Na akatahadharishwa kwamba kadri atakavyokuwa anakaribia kileleni, kelele za sauti ya zomea zomea ‘huyo, huyo huyo’ zitazidi kuongezeka, lakini hapaswi kamwe kuzisikiliza na badala yake aendelee bila kuangalia nyuma hadi aifikie hazina hiyo.

Aidha, akatahadharishwa kuwa, iwapo atageuka nyuma, basi atakuwa jiwe, na ndiyo utakuwa mwisho wa safari yake. Na kwa hiyo Mwalimu akasema, yeye kamwe hawezi kugeuka nyuma akawa jiwe.

Nimechukua maneno ya hotuba hiyo ya mwalimu kujaribu kuelezea ‘zomea zomea’ ambayo inaendelea sasa kutoka kwa baadhi ya wananchi, ikiwa ni pamoja na viongozi wa vyama vya siasa nchini dhidi ya msimamo wa Rais Dk. John Pombe Magufuli, kwenye masuala mengi ya kitaifa kwa hivi sasa.

Ni wazi kuwa walau kwa wenye macho ya kutazama na kuona mambo kama ilivyo kwa baadhi yetu, Tanzania sasa imepata Rais ambaye ana uchungu na maendeleo ya taifa na wananchi wake.

Aina ya Rais ambaye kwa walio wengi walikuwa wakimlilia kwa siku nyingi, mwenye msimamo ‘mkali’ kwa wale wanaohujumu mali za taifa kwa manufaa yao na jamaa zao. Hata wakati wa Mkuatano Mkuu wa CCM, Kikwete alisema, ''mlimtaka Rais mkali, tunawaletea yule mlimtaka''.

Kama Watanzania wana kumbukumbu, watajua namna suala la rushwa na ufisadi lilivyokuwa limetamalaki huko nyuma. Watajua namna watumishi wa umma, ambao walikuwa na dhamana ya kuwatumikia wananchi, jinsi walivyokuwa wametoka kwenye msitari na kuwa watawala, wakijiamulia mambo watakavyo.

Wakasahau kwamba wao ni watumishi wa wananchi, na si watawala kama ambavyo amekuwa akisisitiza Makamu wa Rais mama Samia Suluhu, kwa watumishi wa umma.

Kwamba kwa ujumla hali ilikuwa imefikia pabaya karibu kila mahali na hasa kwenye ofisi za serikali, kiasi cha watumishi wa umma kugeuka kama ‘miungu watu’ wakitaka kutumikiwa na wananchi, badala ya wao kutoa huduma kwa wananchi.

Watu walikesha wakiomba kwa imani zao, wakamulilia Mwenyezi Mungu, wapate rais atakayewajali, na ambaye atatanguliza mbele maslahi ya taifa, badala ya maslahi yake.

Na kweli tukampata Dk. Magufuli ambaye hadi sasa karibu miezi tisa ya kuwapo kwake madarakani, mwanga umeanza kuonekana. Na hii ni kutokana na hatua mbalimbali alizozichukua katika kipindi cha miezi hii michache, ambazo ‘wanaoona’ wanaweza kuziorodhesha vizuri tu.

Kwa uchache ninaweza kuzitaja baadhi ya hatua hizo ambazo zimetia matumaini. Hatua hizo ni pamoja na suala la kupambana na ufisadi, ukianzia na lile suala la makontena bandarini. Lakini pia udhibiti wa matumizi ya fedha za serikali kwa kukata safari za nje zisizo na tija, hatua iliyookoa na inaendelea kuokoa mamilioni ya fedha za umma.

Rais Magufuli akaja kwenye kazi yake aliyojipa mwenyewe ya kutumbua majipu, ambako tulishuhudia na tunaendelea kushuhudia katika kipindi hiki kifupi, akitumbua watu. Baadhi ya vigogo waliokumbana na utumbuaji huo, ni pamoja na wale waliokuwa wakiongoza taasisi mbalimbali, zikiwamo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Bandari (TPA) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Rais Magufuli amerudisha vilevile nidhamu ya watumishi wa umma katika suala zima la kuwahudumia wananchi, na hata katika uteuzi za wasaidizi wake, msisitizo mkubwa umekuwa ni uleule wa kunasibu wasaidizi wake hao kwenda kuwatumikia wananchi.

Rais Magufuli ameweza kufanya kazi kubwa ya kukusanya kodi, kwa lengo la kuwa na fedha za kutosha kugharimia miradi ya maendeleo kwa wananchi, ikitiliwa maanani kuwa katika Bajeti yake ya kwanza ya shilingi trilioni 29, asilimia 40 ya bajeti hiyo inakwenda kwenye miradi ya maendeleo.

Kwa hili vilevile, Mwalimu aliwahi kuliongelea katika moja ya hotuba zake, akionyesha kuwa serikali iliyoathiriwa na rushwa na ufisadi, kimsingi huwa haikusanyi kodi na hasa kutoka kwa matajiri.

Mwalimu akasema, hiyo inatokana na ukweli kuwa tayari matajiri huwa wamewaweka ‘kiganjani’ viongozi wa serikali na kwa hali hiyo, hujikuta hawana uthubutu wa kuweza kuwakabili.

Hali ilivyo kwa serikali hii ya Dk. Magufuli ni tofauti, kodi inakusanywa kwa kiwango cha kuvuka malengo yanayowekwa na serikali, huku ikisisitiza wote walipe kodi na hasa matajiri. Anafanya hivyo katika nia njema ile ile ya kupata fedha za kugharimia shughuli za maendeleo, ikiwa ni pamoja na suala la elimu bure kutoka shule ya msingi hadi kidato cha nne.

Na katika hili la kutoa elimu, tunaweza pia kumnukuu Mwalimu Nyerere, ambaye katika moja ya hotuba zake akiongelea namna ya kuwakomboa maskini na hasa watoto wa maskini.

Mwalimu alinukuliwa akisema kwamba, ‘ukitaka kumkomboa mtoto wa maskini, mpe elimu’ hatua ambayo ndiyo serikali ya Dk. Magufuli, inachokifanya kwa sasa.

Haya yote yanaonyesha kwamba kuna mwanga unakuja, na kwamba serikali ya Dk. Magufuli, iko katika msitari unaotakiwa. Sasa katikati ya mwelekeo huo mzuri unaoendelea kuonyeshwa na serikali hii ya awamu ya tano, tayari wameshaanza kujitokeza watu wanao mzomea zomea, ili ageuke jiwe. Kwamba asiendelee na safari yake ya kuifikisha nchi kwenye hazina iliyo kwenye kilele cha mlima, na hivyo kumkwamisha njiani.

Zomea zomea yao imejikita katika hoja ambazo zinaweza kujadilika, kwa kuangalia mbivu na mbichi zake. Kwa mfano katika hatua yake ya kutumbua majipu, walijitokeza baadhi ya watu wakiwamo viongozi wa vyama vya siasa, waliopinga jinsi alivyokuwa anawatumbua baadhi ya watumishi wa umma, kwa kigezo cha haki za binadamu.

Kwamba kwa mujibu wa mtazamo wao, Rais Magufuli alipaswa kwanza awachunguze na akishakuwa na uhakika wa tuhuma zinazowakabili, ndipo hatua ya kuwatumbua ichukuliwe.

Kwamba watumishi hao wapate nao muda wa kusikilizwa kama inavyoelekeza sheria ya asili (natural justice), na kama maelezo yao hayakutosheleza ndipo utumbuaji ufuate. Lakini zomea zomea nyingine inayoelekezwa kwa Dk. Magufuli tunayoweza kuizungumzia kwenye makala haya, ni ile ya kupiga marufuku mikutano ya vyama vya siasa kufanyika katika kipindi hiki.

Na hasa misemo yake ya kwamba ‘Uchaguzi umekwisha’ ‘Huu siyo muda wa kufanya siasa’ na ‘Huu ni muda wa kazi tu.’ Wengi na hasa vyama vya siasa vya upinzani, vinapinga kuzuiwa kufanya siasa wakati wote kwa kigezo kuwa katiba inawaruhusu.

Mhadhiri Mwandamizi wa Sayansi ya Siasa na Utawala, Profesa Mwesiga Baregu ni miongoni mwa watu wanaopingana na kauli hizo za rais, kuzuia vyama vya siasa kuendesha siasa wakati wote kwa msingi kuwa, siasa kwa vyama vya siasa ni sawa na hewa ya Oksijeni kwa binadamu.

Kwamba binadamu akikosa hewa ya oksijeni hata kwa dakika mbili, tatu anakufa, vivyo hivyo na kwenye vyama vya siasa zisipofanya siasa kwa muda wa dakika mbili ama tatu vitakufa.

Sasa hilo ni la mjadala hasa ikichukuliwa polisi wamesema hawajapiga marufuku mikutano ya kiutendaji naya kiutawala inayofanywa kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za vyama bali wamepiga marufuku mikutano ya hadhara na maandamano ya vyama vya siasa mpaka hali ya kiusalama itakapotengemaa.

Zomea zomea hii kwa Dk. Magufuli ukiiangalia kwa ndani kimsingi inalenga kumfanya geuke nyuma ili awe jiwe, na hivyo ashindwe kutufikisha kwenye hazina iliyoko kwenye kilele cha mlima.

Ni rai ya makala hii kwa Dk. Magufuli, kutogeuka nyuma kutokana na zomea zomea inayojitokeza hapa na pale dhidi ya msimamo wake wa kuipeleka nchi mbele, na badala yake akaze uzi, ahakikishe kuwa wembe ni ule ule. Hii ni kwa sababu tayari wananchi wameshaanza kuona mwanga kutokana na msimamo wake na serikali yake.

Pengine kwa wasiojua, kwa sasa hukuti watu wanaokunywa pombe ama kucheza ‘pool’ wakati wa kazi na hakuna mhudumu wa baa aliye tayari kuuzia mtu pombe kabla ya saa kumi jioni.
Chanzo: Kwa hisani ya Mwananchi.
Uchungu wa wananchi wake huo unatoka wapi wakati alikuta tunanunua sukari kwa bei rahisi nayeye akaipandisha hadi sasa sisi masikini tunaishia kushindia magimbi kwa uji tu?
 
Daisam

JF-Expert Member
May 23, 2016
1,643
2,000
Ni kweli kabisa mtoa hoja. Rais Magufuli ni rais ambaye kwa muda mfupi ameweza kufanya mambo mengi mazuri ambayo watanzania tulikuwa tunayahitaji. Kwa mtanzania mwenye uzalendo wa kweli ataunga mkono juhudi za Rais Magufuli katika kuwaletea watanzania maendeleo. Nchi ilivyokuwa mimi nisingetegemea kwamba kungejitokeza mtanzania yeyote kubeza juhudi za Rais Magufuli katika utendaji wa kazi unaoendelea mpaka sasa. Katika hali isiyo ya kawaida kuna baadhi ya watanzania wenzetu ambao hawaoni hata kidogo kazi anazozifanya rais Magufuli, wamekuwa wakilalamika kwa mambo yasiyo na msingi wowote ule. Kwa maoni yangu mimi ningependekeza kuwa rais angechukua hatua kali zaidi hasa kwa watu wanaoonekana kuwa hawaitakii mema nchi yetu kwa kueneza habari za uzushi juu ya shughuli zinazofanywa na serikali iliyopo madarakani kwa sasa.
 
Yiyu Sheping

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
1,720
2,000
Uchungu wa wananchi wake huo unatoka wapi wakati alikuta tunanunua sukari kwa bei rahisi nayeye akaipandisha hadi sasa sisi masikini tunaishia kushindia magimbi kwa uji tu?
[

DVd hii ya sukari imechuja huku mtaani haiuziki tena na kushauri tafuta nyingine. Hapa wananchi wanaelewa nia nzuri aliyo nayo Mh Rais na wa megundua kuwa kuna wanaofanya juhudi na maarifa kumkwamisha.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom