Rais Magufuli Usiamini World Bank na IMF

Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,373
6,084
Baada ya ripoti ya kamati ya madini kutolewa ni uhakika makampuni yaliyoathirika na ripoti hii yataanza kutumia mawakala wao wakubwa World Bank na IMF katika kuishindika serikali ya Tanzania ili kuwe na makubaliano ambayo yanaweza kuendelea kuileta hasara nchi hii.

Pamoja na mikopo tunaopewa naona mashirika hayo lakini mikopo yao ni kama chambo katika kukamatia samaki

Hivi karibuni Rais wa World Bank na baadaye makamu wake walifanya ziara hapa Tanzania.
 
Mkuu haya makampuni ya madini yaliingia humu nchini na yapo kisheria.

Tulitengeneza mikataba sisi wenyewe kupitia bunge letu lenye wabunge wengi wa CCM likapitisha hiyo mikataba with majority votes.

Tusijitoe fahamu hivi sasa kama vile hawa watu wameingia huko kwenye migodi illegally.
 
Mwenyekiti akasema, nchi ni tajiri inaweza kujiendesha bila kutegemea mikopo.
Thubutuuuu baadaye kidogo akapokea mikopo ya fasta kutoka WB kisha akamuomba Zuma amjengee reli, reli ambayo alituambia tuna hela yetu inayotosheleza kuijenga yote.

Mleta uzi una maono ya Mwenyekiti, hutaki kua tegemezi lakini unapingana na ukweli kua ili kuacha utegemezi lazima kuwe na mchakato. Mchakato wenyewe siyo wa kushindiliana kodi na kuwaconvert trafiki wawe wakusanya mapato.
Na au kula rambirambi maana majanga hayatokei kila siku.

Bahati mbaya think tank wa chama wamemkera wamemtaja kwenye ripoti, sijui atabuni nini lakini ni dhahiri nyoka wa makengeza msaka pesa wamemuudhi.

Sasa hivi nani atakua anawapa dira?
Bashite?
 
Tambua mikataba sio msahafu
 
Soon JPM atakuwa mdogo kama chembe ya mpunga. Rais wa Venezuela aliyepo madarakani alifanya kama anavyofanya JPM lkn yeye ni kwenye mafuta. Alipopata urais tu akaanza oooh ! Tunaibiwa, mikataba ni mibovu na kisha kuwabughudhi mabeberu. Sasa hivi Venezuela haikaliki, ni full maandamano.
 
Nadhani unatakiwa kufahamu role ya hizo taasisi kwenye issues kama hizi!!! Kama Acacia hawataridhika na kuamua kutafuta njia za kisheria hususani zile zinazowalinda, basi suala la hizo taasisi halikwepeki na JPM hana choice!!

Sina kumbukumbu vizuri... ni ama World Bank (75%) au IMF (25%), mmoja wao ni mdhamini wa hizi multinational investments. Udhamini unaoweza kuwafanya wao wawalipe hao investors inapotokea mambo kama haya!!!
 
Tumempata Rais Mzelendo
Kiukweli Huyu ndiye Rais bora na anaye tufaa watanzania
tunahitajika kumuombea Rais wetu
 
Watanzania acheni woga, mbona mnapenda kuwa na fear of unknown?

Kosa kubwa kabisa la Acacia ni kutotambulika kisheria nchini, kosa la pili ni ku-underdeclare ya huo mchanga wa makinikia, unadhani Kwa akili yako, huyo Prof. Mruma na timu yake eti watakuwa wamekosea? weeee!!! thubutu....!

Acacia ni lazima wazungumze hivyo ili kuwapoza shareholders, ndio maana umesikia huyo Chairman wao kaja.
 
Mwenyekiti akasema, nchi ni tajiri inaweza kujiendesha bila kutegemea mikopo.
Thubutuuuu baadaye kidogo akapokea mikopo ya fasta kutoka WB kisha akamuomba Zuma amjengee reli, reli ambayo alituambia tuna hela yetu inayotosheleza kuijenga yote.

Mleta uzi una maono ya Mwenyekiti, hutaki kua tegemezi lakini unapingana na ukweli kua ili kuacha utegemezi lazima kuwe na mchakato. Mchakato wenyewe siyo wa kushindiliana kodi na kuwaconvert trafiki wawe wakusanya mapato.
Na au kula rambirambi maana majanga hayatokei kila siku.

Bahati mbaya think tank wa chama wamemkera wamemtaja kwenye ripoti, sijui atabuni nini lakini ni dhahiri nyoka wa makengeza msaka pesa wamemuudhi.

Sasa hivi nani atakua anawapa dira?
Bashite?
Mwenyekiti alikaa akatafakari kwanini Tanzania iendelee kuwa ombaomba wakati tunapigwa kwenye madini.
Ushirikiano wako ni muhimu kwenye vita hivi ingalau watanzania watue baadhi ya kodi.
 
Watanzania acheni woga, mbona mnapenda kuwa na fear of unknown?

Kosa kubwa kabisa la Acacia ni kutotambulika kisheria nchini, kosa la pili ni ku-underdeclare ya huo mchanga wa makinikia, unadhani Kwa akili yako, huyo Prof. Mruma na timu yake eti watakuwa wamekosea? weeee!!! thubutu....!

Acacia ni lazima wazungumze hivyo ili kuwapoza shareholders, ndio maana umesikia huyo Chairman wao kaja.
Kuna uzi unasema hatimaye acacia wakiri hawajasajiliwa una ufafanuzi mzuri tu.
Halafu pia unasema prof hawezi kukosea hao maprof wengine waliotuleta hapa haujawahi kuwasikia?
 
Baada ya ripoti ya kamati ya madini kutolewa ni uhakika makampuni yaliyoathirika na ripoti hii yataanza kutumia mawakala wao wakubwa World Bank na IMF katika kuishindika serikali ya Tanzania ili kuwe na makubaliano ambayo yanaweza kuendelea kuileta hasara nchi hii.

Pamoja na mikopo tunaopewa naona mashirika hayo lakini mikopo yao ni kama chambo katika kukamatia samaki

Hivi karibuni Rais wa World Bank na baadaye makamu wake walifanya ziara hapa Tanzania.
Mkuu Bowie unaipenda nchi yako lakini ujue maarifa namna ya kuingia mikataba tunapungukiwa. Imagine wb akija na sharti la weka masharti mazuri kwa wawekezaji. Being out of world system is the best option.
 
Nadhani unatakiwa kufahamu role ya hizo taasisi kwenye issues kama hizi!!! Kama Acacia hawataridhika na kuamua kutafuta njia za kisheria hususani zile zinazowalinda, basi suala la hizo taasisi halikwepeki na JPM hana choice!!

Sina kumbukumbu vizuri... ni ama World Bank (75%) au IMF (25%), mmoja wao ni mdhamini wa hizi multinational investments. Udhamini unaoweza kuwafanya wao wawalipe hao investors inapotokea mambo kama haya!!!
Ni Word Bank
 
Back
Top Bottom