Rais Magufuli, unazijua hasira zetu watumishi?

Private investigator

JF-Expert Member
Dec 28, 2012
303
287
Kwenye mikataba ya ajira, ongezeko LA mishahara in July 1 kila mwaka.

Uliahidi May 1 kuwa tukupe muda. Kama sikosei ulisema 2 months.

Pia nakumbuka, ulijitamba 2015 kuwa serikali yako haitokuwa "serikali ya michakato", vipi huu wimbo wa uhakiki, sio mchakato?

Kwanini utese watumishi wote kwa uzembe wa wachache?

Kuna wimbo unaupenda kuwa " Umeinua uchumi", Ila sio kweli, sema umepora haki za watumishi na kuzijaza hazina BOT. Ingekuwa saw a kama ungeendeleza haki za watumishi huku hizo research zikisema yasemwayo sasa kuwa uchumi umekua.

Serikali yako imejaa matamko, matamko ya kila aliyepaswa kuwajibika na kushindwa kiss anataka kuuimba wimbo uupendao. Inasemwa kuwa unapenda ubabe na hushauriki, Nina uhakika hata washauri wazuri waliopaswa kukushauri hawakushauri vyema maana wanakuogopa, nikwambie tu kuogopwa sio sifa, hasa kwa mapungufu uliyonayo.

Jingine linalokutesa ni LA "elimu bure". Kiukweli uchangiaji ulikuwa mzigo kwa wazazi Ila serikali haikupaswa kujitwika mzigo wote. Kuna gharama zingebaki tu kwa wazazi na bodies za shule zingepewa mamlaka kuamua michango, wakurugenzi na DEO wanaogopa hata kuruhusu michango ya study tours? Gharama za NECTA?

Ninayo mengi Ila kiufupi, usitegemee kupoza vidonda hivi mwaka 2019 Lisa titakuwa tukielekea Uchaguzi. Kwa taarifa yako watu was uraiani na watumishi wametunza hasira zao.

Kumbuka ushindi wako haukufika hats 60%, kwa machungu haya naamini utapoteza zaidi ya 10% na unayofikiri mazuri ufanyayo yatafunikwa na aibu ya kuwa " Rais was 1 term Tz".

Hautaacha Legacy yoyote labda Chatu International Airport.

Hasira za watumishi na wanyonge wote zitakutafuna wewe na chama chako.

Serikali yako sio rafiki kwa wananchi, mzee unapenda kuogopwa na kuabudiwa, Mungu hapendi hivyo.

Wajibika ili watu waseme unafaa, sio kuongea sana uonekane unafaa sana.

Toa dira ya utendaji wenye kutoa matokeo chanya kwa watu, sio machungu.
 
Kweli watumishi wamenyimwa haki zao,hata vyama vya utetezi navyo vipo kimiya,vinazungumzia habari za mwaka fedha unaokuja wakati kuna increment ya kisheria haijaonekana,madaraja ya waliopandishwa na kupewa mwenz mmoja mshahara baada ya hapo wakakata kwa kuambiwa watarekebisha baada ya miezi miwili bado iko vilevile,kama mtumishi alipandishwa daraja tokea mwez wa tatu mwaka jana ina maana mpaka mwaka huu anadai zaid ya milion moja n kitu,si kuiongezea maden serikali,watumishi tuna hasira kweli,
 
Bora kukaa kimya, ila Nina uhakika matokeo ya 2020 ya NEC huenda Jecha ajae atayafuta ya Bara. Watu wamemchukia boss huyu kuanzia mama lishe hadi Ma Bar maids, pia hata watumishi WA umma hasa wale wa kada za chini 90% they are not appreciating him at all.

Akitaka kuamini aagize watu walio wakweli wamfanyie utafiti kuhusu kukubalika kwake atapata majibu. Ampe HIYO kazi WARIOBA na baadhi ya wazee wenye hofu ya Mungu kama Mwinyi watampa mrejesho.

Rais ni MZURI sana, shida yake vitisho vingi hadi wasaidizi wake wanaogopa kumwambia ukweli!!!

Tukimshauri humu kwenye mitandao kama hii tunatishiwa kushikwa, Sasa atakamata wangapi? Magereza ameyapanua?
 
magufuli amewin wamachinga na mama lishe na watu maskini wengi sana wanamshangilia...

2020 hata watumishi wote wasimpe kura ccm itashinda kwa kishindo sababu watumishi wachache sana kuliko hao watu...

na chadema ilisumbua sana baada ya wamachinga kuwa chadema na ndio waliokuwa wanalinda kura za lowassa vituoni na kushangilia sana...

sasa magufuli alivyo mjanja amewawin wamachinga na watu duni wengi huku anawabana watumishi ambao ni wachache...

mark my world hali ikiendelea hivi hivi bado 2020 atashinda kwa kishindo kikubwa sana magufuli more than 90 parcent...

kwanza hakuna mtumishi mwenye uwezo wa kulinda kura kama wamachinga walivyofanya kwa lowasa na chadema

watumishi wa uma ni selfish.. wenyewe hawapendani... ccm ilishajua ilikosea wapi..

ukiteka vijana wenye hali ngumu utatawala africa mpaka uchoke... ndio magufuli anateka hao... ameshaanza na machinga, mama ntilie na boda boda now days ukiwagusa tu hao watu unatumbuliwa.

tafuta video ya kariakoo juzi alivyoenda kuzindua dart... wamachinga wanaimba na kushangilia mpaka unaona kabisa chadema kazi wanayo...ccm ni nomaaaaa
 
Bora kukaa kimya, ila Nina uhakika matokeo ya 2020 ya NEC huenda Jecha ajae atayafuta ya Bara. Watu wamemchukia boss huyu kuanzia mama lishe hadi Ma Bar maids, pia hata watumishi WA umma hasa wale wa kada za chini 90% they are not appreciating him at all.

Akitaka kuamini aagize watu walio wakweli wamfanyie utafiti kuhusu kukubalika kwake atapata majibu. Ampe HIYO kazi WARIOBA na baadhi ya wazee wenye hofu ya Mungu kama Mwinyi watampa mrejesho.

Rais ni MZURI sana, shida yake vitisho vingi hadi wasaidizi wake wanaogopa kumwambia ukweli!!!

Tukimshauri humu kwenye mitandao kama hii tunatishiwa kushikwa, Sasa atakamata wangapi? Magereza ameyapanua?

Mm sijaona uzuri wa huyu rais ht kdg yan tumechoka tuna hasira sanaaaa 2020 itukute wazim tho 2015 pia sikumchagua mm aiseeee hali ni mbayaaa mnoo no ajira no uhamisho no madawa no increment yan ht ajenge fly over mpk kwangu ila sitomchagua never everrrrrr
 
Juzi jimbo na kata 19 zimerudi CCM.Tanzania hawajawa tayari kwa maba
diliko

Bora kukaa kimya, ila Nina uhakika matokeo ya 2020 ya NEC huenda Jecha ajae atayafuta ya Bara. Watu wamemchukia boss huyu kuanzia mama lishe hadi Ma Bar maids, pia hata watumishi WA umma hasa wale wa kada za chini 90% they are not appreciating him at all.

Akitaka kuamini aagize watu walio wakweli wamfanyie utafiti kuhusu kukubalika kwake atapata majibu. Ampe HIYO kazi WARIOBA na baadhi ya wazee wenye hofu ya Mungu kama Mwinyi watampa mrejesho.

Rais ni MZURI sana, shida yake vitisho vingi hadi wasaidizi wake wanaogopa kumwambia ukweli!!!

Tukimshauri humu kwenye mitandao kama hii tunatishiwa kushikwa, Sasa atakamata wangapi? Magereza ameyapanua?
 
Uzuri kuna Jehanamu na kuna watu wanajikatia tiketi yakwenda Jehanamu kwa kuyatenda Yale ambayo hawakuwai tendewa Ktk maisha yao....Miaka 10 ni fraction ya macro second Ktk muda wa Mungu Muweza....Haki ya MTU ni haki alioumbiwa na Mungu wake sasa ole wake ujifanye unaukatiri zaidi ya ISIS watalia na kusaga meno.....Watumishi Maisha ya Mekua Magumu maradufu Ndoto za watumishi Kumiliki Nyumba zao zimeyeyuka wapo waliojitahidi kufikisha kwenye renta zimekomea apoapo wapo walioishia kwenye misingi Leo misingi yao imeanza kumeguka nk nk wapo watumishi wamepaki au kuuza magari yao nk nk....Annual increments ipo kisheria kwan ndan ya kipindi cha mwaka parameters za kimaisha zimebadirika km familia kuongezeka nk nk iweje salary ibaki ileile uku familia inakua? Madaraja ya mishahara na kupandishiwa mishahara Ipo kisheria kulingana na taratibu za kiutumishi....iweje ujilipe 10M uku ukiishi bure kwa kila kitu alafu uyu umlipe 500000 uku ata nyumba,chakula ,mtibabu na Ada zikiwa apoapo..God forbid kuna watu watalia na kusagasaga Meno pindi parapanda itapopigwa lakini walipewa macho na masikio na Akili lakini hawakuvitumia....
 
Hakuna kinachoniuma kama kuzuia uhamisho aisee… yaani kidonda hicho maumivu yake yanazidi kabisa ya incriment nna madaraja, yaani naendesha nyumba mbili usawa huuu… mnatutakia nini michepuko ama?? Kuna watu wanaroho ngumu zaidi ya ibilisi!

kwan ww sio mwanaume wa kiafrica mkuu wa kaya kwenye mazish ya masaburi alisema mwanaume wa kiafrika lazima uwe na wake wengi please timiza wajibu ongeza mke uko uko ulipohamishiwa ww
 
Mkuu hii habari yako itume kwenye tovuti ya Ikulu, itafika moja kwa moja kwa Mhe Rais.
Tovuti Rasmi ya Rais
Ofisi ya Rais - Ikulu
 
Mm sijaona uzuri wa huyu rais ht kdg yan tumechoka tuna hasira sanaaaa 2020 itukute wazim tho 2015 pia sikumchagua mm aiseeee hali ni mbayaaa mnoo no ajira no uhamisho no madawa no increment yan ht ajenge fly over mpk kwangu ila sitomchagua never everrrrrr
yani nlkuwa nasoma tu bila kuangalia id.nkasema tu huyu alieandika lazma atakuwa mwanamke na kweli kuvheck id ni female....
 
Back
Top Bottom