Rais Magufuli unapotubana sana usisahau kuwa uliahidi viwanda kila mkoa!

Mwabhleja

JF-Expert Member
Jan 27, 2016
1,351
2,061
Salamu zenu wana JF!
Nimejaribu kupitia kwa umakini taarifa ya serikali juu ya wadaiwa wa bodi ya mikopo ambao hawana ajira. Ni jambo zuri kwa serikali kukusanya mapato kwa kadri iwezekanavyo lakini kuwa na nia ya kukusanya mapato kwa watu ambao unawazibia mianya ya kukusanya mapato ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu kisha kupanga mikakati ya kuyabeba maji hayo kwenye chujio.
Ni jambo la kawaida sana kuona au kusikia shida kubwa inayoongeza tatizo la ajira ni pamoja na wahitimu wengi wa vyuo vikuu kukosa dhama kiasi kwamba hawakopesheki na taasisi za fedha, pamoja na hayo yote bado serikali ya Mhe. Magufuli inapanga kupeleka taarifa za wadaiwa wa bodi ya mikopo benki kuu (BOT) kusudi wasikopesheke kwa kuwa tu bado hawajaanza kurejesha mikopo yao kutokana na kukosa ajira. Mimi nafikiri serikali ya Mhe. Magufuli inatakiwa itekeleze ahadi zake za kujenga viwanda ili vijana wapate ajira. Pia vijana kibao wana taaluma mbalimbali, zile milioni 50 kila kijiji zitengenezewe business plans na wahitimu kusudi wafanye shughuli za kiuchumi na kukuza vipato vyao kisha walipe madeni yao.
Ni vema kuwa na tabia ya mbuzi kuliko kuwa na tabia ya kondoo kusudi ikiwa kama utachinjwa upige kelele za msaada. JISOMEE ZAIDI HAPO CHINI
HATUA ZITAKAZOCHUKULIWA NA SERIKALI
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mdaiwa yeyote wa bodi hiyo atakayeshindwa kulipa deni lake bila sababu za msingi, kwanza atakuwa akikabiliwa na kesi ya madai chini ya kifungu cha 6 C na H cha Sheria ya Bodi ya Mikopo namba 9 ya mwaka 2004.
Mbali na kukabiliwa na kesi hiyo, pia mkopo wake kwa namna unavyochelewa kuanza kulipwa, utakuwa ukijilimbikizia riba ya asilimia 10.
Taarifa hiyo ya bodi imeeleza kuwa mdaiwa huyo taarifa zake zitapelekwa katika taasisi za kumbukumbu ya mikopo zilizo chini ya Benki Kuu (BoT), ambazo zitazuia wadaiwa hao kupata mikopo katika mabenki na asasi zote za fedha.
Mdaiwa huyo pia atazuiwa kupata udhamini wa Serikali katika muendelezo wa masomo yake, lakini pia atazuiwa kujiunga na chuo chochote cha elimu ya juu ndani na nje ya nchi.
Aidha kwa mujibu wa taarifa hiyo, taarifa zao pia zitawasilishwa katika Idara ya Uhamiaji iliyo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na katika ofisi zote za kibalozi, ili wakose kibali cha kusafiri nje ya nchi.
Hasara nyingine watakayokabiliwa nayo wadaiwa hao, ni Tozo ya Kulinda Thamani ya Mkopo (VRF) ya asilimia sita kila mwaka, itakayotozwa kwa kila mkopo, ili wadaiwa watakapoanza kulipa mkopo waliochukua, walipe kwa thamani ya sasa.
Tozo hiyo imelenga kuepuka athari ya mfumuko wa bei tangu mdaiwa aliponufaika, lakini pia kuwezesha urejeshwaji wa deni, uwe na thamani ya kumhudumia mwanafunzi mwingine mwenye mahitaji kwa sasa na baadaye.
Ambao hawajaajiriwa
Taarifa hiyo pia imeonya wadaiwa wanaodhani kuwa kutokuajiriwa ni sababu ya kutolipa mkopo huo, kwamba mkopo huo unatakiwa kulipwa baada ya kumalizika kwa mwaka mmoja tangu mdaiwa alipofanikiwa kuhitimu masomo yake, au mwaka mmoja tangu mhusika alipokatisha masomo yake kwa sababu yoyote.
Aidha, taarifa hiyo imeelekeza watakaojitokeza, kama wameajiriwa, asilimia nane ya mshahara wao wa kila mwezi, itatakiwa kukatwa na kuwasilishwa kwenye Bodi ili kulipa deni husika.
Lakini pia Bodi hiyo imetengeneza utaratibu kwa ambao hawajaajiriwa, kwamba wanaweza kulipa kiasi cha chini cha Sh laki moja kila mwezi katika akaunti za Bodi zilizopo Benki ya Posta yenye namba CCA0240000032; Benki ya NMB namba 2011100205 na Benki ya CRDB namba 01J1028467503.
 
Hili la mikopo kwa watu wasio na ajira wavumiliwe ila kama umeajiriwa kazima uwajibushwe
 
jabulani: Kibaya zaidi ni kuwatengenezea mazingira ya kutokopesheka nchini mwao na kuwazuia kutafuta fursa zaidi nje ya nchi
 
Hii ni serikali ya Kukurupuka. Kwani masharti ya MKopo yalikuwa yanasema hivyo? au ubabe unatumika? Je, na walioikopesha serikali nao wadai fidia?
 
Salamu zenu wana JF!
Nimejaribu kupitia kwa umakini taarifa ya serikali juu ya wadaiwa wa bodi ya mikopo ambao hawana ajira. Ni jambo zuri kwa serikali kukusanya mapato kwa kadri iwezekanavyo lakini kuwa na nia ya kukusanya mapato kwa watu ambao unawazibia mianya ya kukusanya mapato ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu kisha kupanga mikakati ya kuyabeba maji hayo kwenye chujio.
Ni jambo la kawaida sana kuona au kusikia shida kubwa inayoongeza tatizo la ajira ni pamoja na wahitimu wengi wa vyuo vikuu kukosa dhama kiasi kwamba hawakopesheki na taasisi za fedha, pamoja na hayo yote bado serikali ya Mhe. Magufuli inapanga kupeleka taarifa za wadaiwa wa bodi ya mikopo benki kuu (BOT) kusudi wasikopesheke kwa kuwa tu bado hawajaanza kurejesha mikopo yao kutokana na kukosa ajira. Mimi nafikiri serikali ya Mhe. Magufuli inatakiwa itekeleze ahadi zake za kujenga viwanda ili vijana wapate ajira. Pia vijana kibao wana taaluma mbalimbali, zile milioni 50 kila kijiji zitengenezewe business plans na wahitimu kusudi wafanye shughuli za kiuchumi na kukuza vipato vyao kisha walipe madeni yao.
Ni vema kuwa na tabia ya mbuzi kuliko kuwa na tabia ya kondoo kusudi ikiwa kama utachinjwa upige kelele za msaada. JISOMEE ZAIDI HAPO CHINI
HATUA ZITAKAZOCHUKULIWA NA SERIKALI
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mdaiwa yeyote wa bodi hiyo atakayeshindwa kulipa deni lake bila sababu za msingi, kwanza atakuwa akikabiliwa na kesi ya madai chini ya kifungu cha 6 C na H cha Sheria ya Bodi ya Mikopo namba 9 ya mwaka 2004.
Mbali na kukabiliwa na kesi hiyo, pia mkopo wake kwa namna unavyochelewa kuanza kulipwa, utakuwa ukijilimbikizia riba ya asilimia 10.
Taarifa hiyo ya bodi imeeleza kuwa mdaiwa huyo taarifa zake zitapelekwa katika taasisi za kumbukumbu ya mikopo zilizo chini ya Benki Kuu (BoT), ambazo zitazuia wadaiwa hao kupata mikopo katika mabenki na asasi zote za fedha.
Mdaiwa huyo pia atazuiwa kupata udhamini wa Serikali katika muendelezo wa masomo yake, lakini pia atazuiwa kujiunga na chuo chochote cha elimu ya juu ndani na nje ya nchi.
Aidha kwa mujibu wa taarifa hiyo, taarifa zao pia zitawasilishwa katika Idara ya Uhamiaji iliyo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na katika ofisi zote za kibalozi, ili wakose kibali cha kusafiri nje ya nchi.
Hasara nyingine watakayokabiliwa nayo wadaiwa hao, ni Tozo ya Kulinda Thamani ya Mkopo (VRF) ya asilimia sita kila mwaka, itakayotozwa kwa kila mkopo, ili wadaiwa watakapoanza kulipa mkopo waliochukua, walipe kwa thamani ya sasa.
Tozo hiyo imelenga kuepuka athari ya mfumuko wa bei tangu mdaiwa aliponufaika, lakini pia kuwezesha urejeshwaji wa deni, uwe na thamani ya kumhudumia mwanafunzi mwingine mwenye mahitaji kwa sasa na baadaye.
Ambao hawajaajiriwa
Taarifa hiyo pia imeonya wadaiwa wanaodhani kuwa kutokuajiriwa ni sababu ya kutolipa mkopo huo, kwamba mkopo huo unatakiwa kulipwa baada ya kumalizika kwa mwaka mmoja tangu mdaiwa alipofanikiwa kuhitimu masomo yake, au mwaka mmoja tangu mhusika alipokatisha masomo yake kwa sababu yoyote.
Aidha, taarifa hiyo imeelekeza watakaojitokeza, kama wameajiriwa, asilimia nane ya mshahara wao wa kila mwezi, itatakiwa kukatwa na kuwasilishwa kwenye Bodi ili kulipa deni husika.
Lakini pia Bodi hiyo imetengeneza utaratibu kwa ambao hawajaajiriwa, kwamba wanaweza kulipa kiasi cha chini cha Sh laki moja kila mwezi katika akaunti za Bodi zilizopo Benki ya Posta yenye namba CCA0240000032; Benki ya NMB namba 2011100205 na Benki ya CRDB namba 01J1028467503.
Na we unaona viwanda kila mkoa ni suala linalowezekana?
Tanzania ya Kufikirika
 
PAIN KILLER: Kama haiwezekani basi hata mdaiwa asiye na ajira hawezi kulipa 100,000tsh kila mwezi maana na yenyewe itakuwa kusadikika
 
Elimu yetu haitujengi kujiamini,katika hiki kilichopo tu tunashindwa kucompete na wageni,elimu yetu inatuandaa katika kuamini kua ukimaliza kusoma utaajiriwa...tuboreshe elimu yetu tuwekeze katika taasisi zetu...haya mambo ya mtu kua ana ujuzi wa hali ya juu katika masuala ya nyuklia alafu anaingia kwenye siasa hayatatufikisha popote...wataalamu wetu wapewe platform ya kutumia utaalamu wao..platform isiwe siasa.
 
Back
Top Bottom