Rais Magufuli tunyooshe tu,kama ndio hivi wapinzani wanavyo tufanyia sisi WANANCHI..

Wote wanaounga hoja humu hamjui maana ya upinzani. Kwa mfano wapinzani wakawa upande wa raisi nani atampa changamoto raisi? Waacheni wapinzani wawe wanafanya hivyo ili raisi ajue kuwa kumbe ana mambo ya kufanya
Wapinge vitu vya maana, lakini leo rais akisema kala ugali wao watapinga watasema kala wali na ushahidi upo!
 
Naunga mkono hoja
Wapinzani hawajui wanasimamia ajenda gani wamebaki kuota ota na kuweweseka usiku na kukabwa na majinamizi.
Sintomsamehe Mbowe kwa kukiharibu chama mwaka ule maana sasa kila ajenda tulinyang'anywa kutokana na kuja mzee yule.
 
Hayo yote uliyoyaandika ni mazuri sana na tungependa afanye mazuri zaidi, ila tatizo ni pale anapoamini kwamba anaweza kufanya kila kitu peke yake bila kushauliwa na asikosee.

Pia apunguze ubabe kwa wananchi wake make kuna vitu na sisi tunaona kabisa anakosea ila tukisema anatujibu ku*ya.
 
Mkuu shida ni kwamba si kila USHAURI una maana kibaya zaidi wanaomshauri ndio Balaaa.....ACha tu aongoze anavyoona ni sahihi....tutamuhukumu 2020.......
 
Cocochanel vipi nakupenda mamy eeeeh mbona ivo ctakuwa mpinzani sikiliza ombi langu ntaacha siasa twende kwetu ukanywe ulanzi

Ha ha ha haaaaaaa wewe, eeeeh subiri watakuja watakaokuvutia

Ulanzi ni nini, napenda kufahamu.
 
mtoa mada nimekuelewa tatizo hapa kwa watu wengi tunaomba mkulu aunusuru uchumi wa nchi hii, hali mbaya sana, biashara nyingi zinakufa, purchasing power imedecline sana.
 
Umeandika mambo mengi kumbe hata alichosema Zito hujaelewa. Kasome tena uombe hata mtu akusaidie kukuelewesha.
 
Ili tujue wamechokwa tuweke tume huru ya uchaguzi na wakurungezi wasiwe sehemu ya tume pamoja na polisi kuwa neutral kabisa! Baada ya kushinda hapo tunawapa hongera nje hapo ni ushindi wa goli ka mkono!!
 
Kweli mkuu.Mtukufu raisi naomba uongeze kukaZa awa wapingA maendeleo tuachane nao
 

HUO NDIO UKWELI MTUPU.

Viongozi wa upinzani ni watu wazima, wasomi, waliokomaa kisiasa na siasa za uharakati, mabingwa wa majukwaa, maandamano, operesheni, kufitinisha, kukejeli, kudhihaki, kulalama na aina yote ya kunyooshea utawala vidole vya lawama.

Ni mtu mwenye nia mbaya tu na nchi hii, ambaye atakebehi juhudi za Rais Magufuli kurekebisha uozo katika utendaji kazi na uwajibikaji.

Viongozi wa upinzani sikilizeni sauti za wanyonge ambao nia yao ni maendeleo siyo nyie mnaotaka uhuru usio na mipaka au haki pasipo kuwajibika.

TUMEWACHOKA NA KELELE ZENU ZA KITOTO.
 

Nakubaliana na hizi hoja zote kwa asilimia mia, Piga kazi Kiongozi wetu shupavu, watoto wetu na vizazi vijavyo watakushukuru na kukumbuka maana unaona mbali sana kwa unayoyasimamia, wapinzani hasahasa chadema wanatushangaza sana, labda wanawaza leo tu ndio maana wanakuwa vigeugeu.... Kwa kiasi kikubwa unayoyasimamia ndicho kilikuwa kilio chetu na chao kwa muda mrefu. Uzalendo ni kuipenda nchi yako kwanza kwa dhati na kwa vitendo then mambo mengine kama ushabiki wa vyama nk yanafuhata. Inasikitisha hata mambo ya kijinga mtu anashabikia eti kwasababu mtu yupo chama tofauti. Akili ya wapi mtu unafikia stage ya kushabikia madawa ya kulevya! - Hopeless kabisa
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…