Mkuu wetu tumeona jitihada zako kuanzia kutumbuwa kule bandarini na kushughulikia wakwepa kodi,kushughulikia waliovamia viwanja na ubomoaji hapa Dar es Salaam, kuzuiya vibali vya kuagiza sukari nje na kubana matumizi ya serikali.Nadhani ilikuwa lengo ni kuimarisha maisha ya wananchi na kuleta maendeleo.Wataalamu mbali mbali na wanasiasa kila mmoja na uoni wake wengine wanaponda wengine wanasifia wengine wanatoa muda wanasema ni mapema.
Jambo moja mimi naliona rais wangu, WAKATI JITIHADA HIZO ZIKIENDELEA NI UKWELI ULIO WAZI KWAMBA MAISHA YA WANACHI YANAZIDI KUWA MAGUMU. Fedha imekuwa adimu na ngumu kupatikana, bidhaa zimekuwa ghali mno, biashara zimepwaya na baadhi ya bidhaa kuwa adimu kidogo (Sukari)
Ajira ni ngumu na misuguano ya kisiasa imeanza kuchipuka yote haya yanafanya maisha ya jumla ya wananchi kuwa magumu.Tunahitaji majibu sahihi maana wengine tulitarajia wakati jitihada hizi zikiendelea basi unafuu wa maisha uanze kupatikana sasa kuna nini huko tatizo nini?
Nafikiri kwa uoni wangu hili ni suali muhimu kwa rais wetu Dr Magufuli.
Kwanini maisha ya wananchi yanakuwa magumu licha ya jitihada hizi?
Asante.