mchimbadhahabutz
Member
- Oct 15, 2016
- 56
- 49
Mh. Magufuli chonde chonde tumesahaulika TUNAOMBA UJE !
Wakazi wa kijiji cha KAKOLA wilayani kahama takribani kilomita moja na nusu kutoka mgodi mkubwa wa dhahabu nchini Bulyanhulu unaomilikiwa na kampuni ya ACACIA baada ya wachimbaji wadogowadogo kutimuliwa mwaka 1996.
Ifahamike kuwa jamii ya maeneo haya kwa asilimia 90 ni wachimbaji wadogowadogo sasa pamoja na kuwekezaji huo pamekua na ujirani usioridhisha kati ya wakazi na mgodi huu katika mambo yafuatayo;
1. Kila wachimbaji hao wanapogundua madini huonekana ni eneo la mwekezaji huyo kwa mfano NAMBA 2 na IYENZE. Hivyo wachimbaji huvulumishwa na kubaki mitaani wakilandalanda vijiweni na kujihusishavna matukio hatarishi kama vile wizi na uvamizi kwa sababu tu ya ukosefu wa kazi na ajira kwa kuwa hata mwekezaji huyo hana ubavu wa kuwaajiri hata robo yao.
2. Huduma mbovu za kijamii: Najua kwamba katika mikataba ya mwekezaji huyu kipengele mojawapo ni kuhakikisha anajenga miundombinu na huduma za kijamii, lakini vha kushangaza ukifika KAKOLA usishangae kuona watu wana ndoo kichwani wakifuata maji umbali wa kilomita moja na dumu likuzwa sh.1000 wakati mwekezaji amevuta maji kutoka katika ziwa Victoria kuendeshea mitambo yake na kumwagilia MAUA ili yastawi!
Huduma ya afya unabipata umbali wa kilomita 20 kata ya LUNGUYA ama MSALALA kijiji cha KAKOLA eti hamna pamoja na muwekezaji huyo kuwepo kwa zaidi ya miaka 20!
Shule ya sekondari Bulyanhulu ni aibu ukiiona haifuaninii na hilo jina kabisa! angharau kidogo waliwajengea wafanyakazi wao shule nzuri kwenye nyumba zao za cotors BUGARAMA!
BARABARA ni zaidi ya aibu! Huwezi amini kama barabara ya kuunganisha mgodi wa Buly na Kahama mjini ambayo ni takribani KM80 ni vumbi na imejaa corrogation kwa sababu ya makontena ya mchanga wa dhahabu unaosafirishwa kwenda bandari ya DSM! Miaka zaidi ya 20 ya kuvuna dhahabu yetu ni shida bora hata enzi tunachimba sie wenyewe. pamoja na kuvuna takribani dhahabu yenye zaidi ya USD 45 trilion lakini barabara ya 80km-80bil imewashinda kabsaaa!
KAKOLA PAMOJA NA UMUHIMU WAKE NA MCHANGO WAKE KATIKA PATO LA TAIFA IMESAHAULIKA SANA, VIONGOZI WENGI WAKUBWA HAWAPATEMBELEI KUJUA KERO ZETU, NATUMAINI SERIKALI HII YA MH. MAGUFULI ITATEMBELEA NA KUTATUA KERO NYINGI ZA WANANCHI WAO.