General Mangi
JF-Expert Member
- Dec 21, 2013
- 15,316
- 23,178
Wakuu salam!!!...
Ni takribani siku ya 26 sasa tangu Rais mpya kuapishwa Dr John Magufuli.
Pamoja na spidi na mikakati yote, bado naona anaipendelea Dar pekee.
Ziara yake ya pili alikwenda Hospitali ya taifa muhimbili.
Baada ya kuzindua bunge pale dodoma, Rais Magufuli alipendekeza pesa za sherehe za bungee zielekezwee Muhimbili kununua vitanda.
Rais bado anadhani matatizo yapo Dar peke yake, hakujua pia dodoma ambazo pesa hizo zilipatikana eneo hilo hakuna hospitali yenye matatizo kama muhimbili.
Hiyo haitoshi, Jana kapendekeza fedha za sherehe za Uhuru zipelekwe kupanua barabara ya mwenge zaidi ya sh. 4 billion ili kupunguza msongamano. Rais bado hajajua tatizo la Dar kuwa na folen ni ofisi nyingi za serikali kujaa posta na shughuli za biashara kuwa K.koo na posta.
Sisi kama wananchi kila jambo tunashangilia pasipo kutatua matatizo yanao tukabili.
Rais anapaswa kutambua kuwa Tanzania ina mikoa zaidi ya 30, mikoa yote hii inataka kuona inanufaika na nchi hii na sio kila kitu ni Dar.
Fedha za uhuru ni bora zingeelekezwa kwenye shule za msingi ambazo zinamatatizo ya vyoo nchi nzima.
Tunataka kasi yake ya utendaji ije pia mikoani ambapo huku ndipo uonzo mwingi.
Pia ni bora kila wizara kusambazwa mikoani ili kupunguza msongamano, na kukuza miji mingine kibiasharaa.
Rais tunakuomba utambuee kuwa hata sisi wa mikoani ni watanzania tunastahili haki kma Dar, umekuja dodoma hukutembeleaa taasisi zako hata moja, hata kama ni kwa unafki lkn ungetembelea tu.
Salaam!!!