yoga
JF-Expert Member
- Jan 6, 2013
- 1,820
- 8,498
Kuna mambo sasa serikali inapaswa kuyabadili ili kupanua vyanzo vya mapato. hii nikutokana na kutegemea Bandari kwa asilimia kubwa kama chanzo cha mapato ya serkali kuu na kukosa ubunifu mpya wa namna gani serikali inaweza kupata mapato makubwa zaidi. mambo ambayo nahisi serikali inapaswa kuya tumia ama kuyabadili kukuza pato la taifa nikama yafuatayo;
a) kutumia kitengo cha magereza na jeshi nchi nzima kama chanzo cha mapato ya serikali kwa magereza yenyewe kuwekeza katika;-
i) kilimo kikubwa cha umwagiliaji wa mazao ya biashara na ya chakula nchi nzima
ii) ufugaji wa ng'ombe wa biashara wa nyama, kuku na asali
iii) viwanda vya chakula, samani za ndani, vyombo na nguo za kuvaa
hii itasaidia serikali kupunguza bajeti ya kuhudumia magereza na jeshi kwa asilimia kubwa na badalayake magereza na jeshi kujiendesha kwa asilimia kubwa nakuchangia katika pato la serikali kwa uwekezaji tajwa hapo juu.
b) Wilaya zote za tanzania zinapaswa sasa kufanya ya fuatayo;-
i) kutazama ni aina ipi ya kiwanda/viwanda vinapaswa kujengwa katika wilaya zao
ii) lakini pia wilaya zenye ardhi ya kilimo zitenge ardhi sasa kwa ajili ya aina 2 za kilimo, kilimo kikubwa cha mazao yaina mbali mbali na kiwe cha umwagiliaji lakini pia kilimo cha ufugaji wa mifungo mbalimbali na kuwa kusanya vijana woote wasio naajira rasmi wenye taaluma na wasio na taaluma kisha kuwapangia majukumu ya kusimamia miradi ya viwanda na mashamba na kufanya kazi kwenye viwanda hivyo na mashamba hayo kwa kila wilaya.
hii itasaidia wilaya kupata mapato zaidi kwa kuwekeza yenyewe katika kilimo na viwanda na kupunguza tatizo la ajira kwenye wilaya zao! wanachopaswa kufanya ni kuaandaa mpango kujua gharama na kisha kuweka mpango huo kwenye kila bajeti yao ya wilaya ya kila mwaka kwa utekelezaji.
c) serikali ifumue mfumo wa sasa wa elimu na kuufanya kuwa mfumo unao endana na kipaji cha mtoto husika. Uta kuta hali ya sasa kata moja ina shule nne za sekondri zinazotoa mfumo uleule wa elimu. serikali sasa ifike mahala ifanye kwamba katika shule nne, shule moja ifuate mfumo wa sasa wa elimu kwa wanafunzi wenye uelekeo wa aina hiyo ya mfumo wa elimu, shule inayo fuata itoe mafunzo ya ufundi tu, kama vile magari, uselemala, umeme na nk, shule nyingine itoe elimu ya michezo tu, naiboreshewe miundo mbinu ya michezo hiyo, na shule ya mwisho iwekewe mfumo wa masommo ya sayansi yaani ubunifu katika teknolojia.
d) serikali iingie katika kukusanya kodi ya ardhi na jengo kwa mfumo wa kielectroniki ambapo sasa kila mtanzania anapaswa kuwa na tin number ambayo iwe included kwenye vitambulisho vya utaifa kuweka mazingira kwa kila raia wa tanzania mwenye nyumba na mpangaji wote sasa wawe walipa kodi
e) serikali ipunguze matumizi kwa kufanya ya fuatayo
i) kununua magari ya viongozi yenye bei nafuuu; mfano colora ama vits mpya za milion 25 mwisho
ii) kuondoa posho zote za vikao kwa 100%
iii) kujiondoa kwenye misamaha ya kodi 100%
iv) kununua samani za bei na fuu na kutogharamia maswala ya chai na vitafunwa kwa viongozi
haya ni baadhi tu unaweza pia ukakosoa ama kuongezea ili TANZANIA iende!!!!!!!!