Vyuo havitengi hela ya kuelendeleza walimu vijana, vinavizia waliostaafu vichukue, hii ni sawa kaka?Si wazo zuri Elimu duniani kote vikongwe ndo huwa Waliimu wa Vyuo Vikuu mi naona wako sahihi Ualimu wa vyuo safari yao huanza Wakiwa na Miaka 50 kuendelea na ndo wanakua wazuri sana. Yaani Serikali imteme Professor wa Muhimbili University aliyefanya Successful Operations/Surgery 1000 na Kumuajiri Kijana mwenye miaka 30
Ahsante kwa upotoshaji mkubwa ulioweka hapa (kwa uelewa wangu). Sidhani kama unaelewa hali halisi ndani ya hivi vyuo. Sitawatetea wale ambao wako kwenye nafasi za utawala ni imani yangu wako watanzania wa kutosha kuzijaza hizo. Issue yangu ni kuhusu nafasi za wanataaluma tukiweka siasa elimu itashuka. Kwa ufupi Tanzania haijasomesha wataalam wakutosha kwenye nyanja kadha ukiwaondoa hao unaowaita wazee vyuo vita-athirika. Vyuo vitengeneze succession plans na serikali iwekeze fedha (ijenge required human capital) na baada ya miaka kadha utaweza kupunguza uhitaji wa hao "wazee". Halafu pia kuna issue ya ku-define wazee kitaluma ni wakina nani? 55 au 60 au miaka mingapi.Vyuo vingi havina walimu bali vimekusanya wazee waliochoka waliostaafu kwenye vyuo vya umma na kusababisha Vijana wanaomaliza vyuo kupata ajira vyuo vikuu kwa taabu sana. Utakuta Makamu Mkuu wa chuo ni mstaafu, Naibu Makamu mkuu wa chuo taaluma ni mstaafu, Naibu Makamu Mkuu wa chuo mipango na fedha ni msataafu, Bwana fedha (Bursar) ni mstaafu, wakuu wa vitivo ni wastaafu. Wastaafu hawa huwa wanapenda kuajiri wastaafu wenzao katika nafasi mbalimbali katika vyuo na kuacha kuwaajiri vijana kwa kuogopa eti vijana wanachangamoto nyingi zikiwemo za kuhoji hoji mambo na kuhitaji kuendelezwa kitaaluma. Hii inasababisha hasara zifuatazo kwa taifa.
1. Wazee wengi hawana jipa ila wanaendeleza kufundisha vijana kile wanachokifahamu tu na walichofanyiwa wao enzi zao hata kama hakikuleta manufaa kwa taifa.
2. Wazee wengi wamechoka sana, muda mwingi wanaumwa (mgongo, pressure, kisukari, macho, mifupa)
3. Taifa linawekeza (semina, mafunzo) kwa wazee tena ambao muda wao umekwisha badala ya kuwekeza kwa vijana ambao wana kesho nyingi.
4. Wazee wanapunja nafasi za ajira kwa vijana wanaotakiwa kurejesha mikopo bodi ya mikopo
5. Baadhi ta wazee hawapendi kuona vijana wanafaulu sana kwenye masomo ya fani zao ili kuepuka kuchukua nafasi zao. Yaani hawana hawaandai warithi wao (succession plan).
6. Baadhi ya wazee wana frustrations mbalimbali zilizotokana na maisha waliyoishi siku za nyuma, hivyo kuwafundisha vijana namna ya kuichuikia nchi yao.
7. Wazee mara nyingi hawakai ofisini/hawafundishi kwasababu za kusafirisafiri sana, kifamila au kiafya.
Kifupi, vyuo vingi havina walimu vibrant wa kufundisha vijana vyuo vikuu ila wastaafu waliojikusanya kwenye vyuo binafsi kuganga njaa zao baada ya kutumika kwenye vyuo vya umma. Ni wazuri kwa kuwakumbusha vijana maadili ya taaluma (babu) lakini sio productive and innovative.
Lazima kutolewe muongozo kuhusu idadi ya wastaafu vyuoni ili kuinusuru taaluma yetu.
Atakayekukatalia ni mchawi,4. Wazee wanapunja nafasi za ajira kwa vijana wanaotakiwa kurejesha mikopo bodi ya mikopo
call spade spade.... Hata mimi nitakuwa mzee, lakini ni lazima nijiandae kustaafu na kuwaacha vijana wenye mawazo mapya kwa nchi yao, mimi kazi yangu sasa hivi ni kumuandaa mrithi wangu leoleo atakayechukua nafasi yangu mimi na sio kutamani kufia kazini. Sana sana wataniita tu kwa kipindi kimoja au mada maalumu, lakini sio permanent (full time) na NSSF upya tena.Wewe ni kijana wa leo na mzee wa baadae. Sasa kumbuka kuwa manyanyaso au lugha ya unyanyapaa dhidi ya wazee, na wewe yatakuja kukukuta siku moja.
Unaweza ukawa na hoja fulani yenye kueleweka tatizo maandishi yako yameshindwa kuufikisha ujumbe uliokusudiwa.
You sound sarcastic but you could have used a better way of sending your message to the public.
Utaalamu wa chuo ni tofauti na utumishi mmngine kadri unavyokaa ndio unavyohitajika Zaidi, kwani unaendelea kugundua vitu vingine zaid na zaid katika utafiti . Sio suala la kufikisha miaka 60 na kupisha. Hapa unazungumzia utafiti na contribution of knowledge to the world.call spade spade.... Hata mimi nitakuwa mzee, lakini ni lazima nijiandae kustaafu na kuwaacha vijana wenye mawazo mapya kwa nchi yao, mimi kazi yangu sasa hivi ni kumuandaa mrithi wangu leoleo atakayechukua nafasi yangu mimi na sio kutamani kufia kazini. Sana sana wataniita tu kwa kipindi kimoja au mada maalumu, lakini sio permanent (full time) na NSSF upya tena.
Mkuu kwa tabia hiyo wazee wametuaminisha vijana kuwa lazima uwajiriwe na kufanya kazi kwa mtu milele hadi ufe. Ndo maana vijana wetu hawafikirii kujiajiri wenyewe na kutaka lazima waajiriwe kama maprofessor wao ambao ndio role model wao kwenye elimu ambao bado wanatumikishwa hata na uzee wa mikaka 80.Hapa naweza kupinga hoja yako, nakumbuka wakati ninasoma walimu wazee (Maprofessa) wengi ndio waliuwa wanafundisha vizuri kwa kutoa mifano hai ya vitabu/machapisho yao na hata miradi mikubwa waliofanyia kazi, walimu vijana wengi wao walikuwa na majivuno/ubababishaji mwingi nafikiri kwenye fani hii uzee ni dawa.
Vile vile hizo nafasi ulizozitaja (uongozi wa juu wa chuo) huwa zina vigezo/masharti mfano mtu awe na PhD, machapisho kwenye Journal kubwa duniani nk. ili uweze kuvipata vigezo hivyo ni nadra sana kukuta kijana mdogo mwenye miaka 30 ama chini amevitimiza nafikiri wale wataalamu wa maswala ya elimu ya juu wanaweza kutupa maelezo zaidi.