Yakuza
Senior Member
- May 22, 2011
- 114
- 43
Ukweli kuhusu Umakini na Uzalendo wa Rais Magufuli:
HITIMISHO: Watanzania ninaomba tuweke utaifa wetu mbele. Tanzania iwe kwanza kisha mengine yafuate. Hii ya kila kukicha kubeza, kutukana na kukebehi kazi nzuri inayofanywa na Mhe. Rais wetu na Serikali yake kamwe haiwezi kutuacha salama. Wanaokosoa Serikali waikosoe kwa lugha yenye staha na ukosoaji utanguliwe na uzalendo.
Ninafahamu kuna watu watatoa matusi juu ya mtazamo wangu huu kwa sababu walitaka wawe wao. Tayari nimewasamehe wote wependao kuwatusi na kuwadharau wenzao.
Ee Mwenyezi Mungu, ninakuomba umbariki sana Mpendwa wetu Rais J. P. Magufuli na tubariki watanzania wote.
Hakika, Rais Magufuli ni Nuru na Mkombozi wa Watanzania
- Rais JPM anapigana vita ya dhati dhidi ya rushwa na walarushwa (zero tolerance to corruption). Kazi buti na tunakuombea sana Mhe. Rais;
- Amefanya reforms za dhati ndani ya chama chake cha CCM bila kuangalia sura. Kuna watu ndani ya CCM walidhani CCM ina wenyewe na waliozoea njia za mkato. Watu wanaisoma namba. Chaguzi zinazoendelea ndani ya CCM ni ushahidi tosha. Hongera sana Mhe. Mwenyekiti wa CCM Taifa;
- Watanzania tumeanza kulipa kodi. Wafanyabiashara wengi na hata wafanyakazi hawapendi kulipa kodi inayostahili. Waliozoea kutolipa kodi wanaona maisha ni magumu. Keep it up Mr. President!
- Kuna ongezeko kubwa la nidhamu kazini, hususani kwenye taasisi za Umma. Huu ni msingi mkubwa wa maendeleo wa taifa lolote. Hatuna cha kukupa Watanzania Mhe. Rais;
- Rais Magufuli anabana matumizi kwa nguvu zake zote. Katika awamu zilizopita tulikuwa tunapiga kelele kwa sababu ya matumizi yasiyo ya lazima. Safari za Mhe. Rais zinaenda na mahesabu. Siyo kweli kwamba Mhe. Rais hapendi kusafiri kwenda Ulaya na Amerika. Predisent yuko conscious na gharama za safari huko nje. Anaona bora hiyo hela inunue madawa mahospitalini. Mhe. Rais, Mungu akuongezee maisha marefu hapa duniani;
- Mhe. Rais tokea ameingia Ikulu Nov 2015, amepambana na mfumko wa bei. Hata hivyo thamani ya shilingi haijatulia sana...na hii ni kwa sababu ya visababishi vingi kutoka nje ya nchi (external factors). Mhe. Rais, unajenga uchumi imara. Chapa Mwendo Baba;
- Nchi haiwezi kuachwa ifanye siasa kuanzia mwanzo wa uchaguzi mmoja hadi mwingine, Januari hadi Desemba. HAIWEZEKANI. Na haipo popote duniani. Lazima ifikie mahala watanzania tulijue hilo na tufanye kazi kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu tukitanguliza uzalendo mbele;
- Serikali ya JPM inafanya kazi usiku na mchana. Baraza la mawaziri halilali, wakuu wa mikoa na wengine wote wapo wanakimbia. Ni kweli, kuna baadhi ya watendaji wanatia doa Serikali. Kuonesha namna Serikali ya JPM inavyofanya kazi, subiria kidogo utawasikia hao wachache;
- Miradi mingi ipo inaanzishwa na mingine inaendelea. Mradi kama wa Standard Gauge Rail kama utakamilika, Tanzania itapiga hatua kubwa kiuchumi. Shinkanse (bullet train) ya Japan iliaza kujengwa miaka 1956 na kukamilika miaka kumi baadae. Japan ilijenga treni hiyo kwa mkopo kutoka benki ya dunia na wahisani wengine. Shinkanse anayoijenga JPM ndiyo iliwakomboa Wajapan kutoka taifa masikini hadi taifa lenye uchumi bora duniani. Hivi Watanzania, Mungu atupe nini?
- Katika kipindi cha takribani miaka 2 sasa, hakika Rais JPM amefanya mambo makubwa kwa nchi yetu. Pamoja na changamoto zilizopo kwenye elimu ya msingi na sekondari, ni mtanzania yupi hafahamu kuwa ni Rais JPM ndiye kamaliza tatizo la madawati nchini?. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Hongera Mhe. Rais!