AUGUSTINO CHIWINGA
JF-Expert Member
- Apr 23, 2017
- 220
- 689
Tanzania ina watumiaji wa mitandao ya simu wapatao million 40 huku Kenya ikiwa na watumiaji wa simu wapatao million 38 tu.
Katika orodha ya walipaji kodi bora Tanzania kampuni za simu za Tanzania,ziko nyuma kulinganisha na majirani zetu Kenya ambao kampuni kama Safaricom ndo hua anashika namba moja kwa ulipaji bora wa kodi.Katika Miaka sita iliyopita kampuni za simu zimechangia ukuaji wa uchumi wa Kenya kwa asilimia 250%
Hii inaonesha kwamba pamoja na kampuni za hapa nyumbani kua na idadi kubwa ya wateja lakini ulipaji wao kodi ni wa kusuasua, hili haliingii akili hata kidogo.
Sitaki kuamini kama kwa muda wote huo huo kampuni hizi hazipati faida na kama zingekua zinapata hasara zingekua zimesha shafunga biashara.
Mchango wa makampuni haya pato la ndani ni asilimia 2.1 pekee huku hapo Kenya ni asilimia 7.
Ni ukweli usiofichika kwamba makampuni haya yamekua yanaficha kwa makusudi taarifa sahihi za mahesabu yao kwa kuandaa vitabu viwili vya mahesabu moja ikionesha hasara hicho hupelekwa serikali na kingine kinachoonesha faida hicho hupelekwa kwa wamiliki wa makampuni.
Kwa kutambua hilo ndio maana serikali ikaja na mwarobaini wa kisheria wa kuyalazimisha kampuni hizo za simu zijiandikishe katika soko la hisa la Dar Es Salaam (DSE) kufanya mabadiliko katika sheria ya Mawasiliano ya Kielekroniki na Posta Namba 2 ya mwaka 2016 .(EPOCA)
Hatua hii itasaidia nchi kupata taarifa sahihi cha kiwango cha faida kilichopatikana na serikali kuchukua kodi yake stahiki .Lakini kwa taarifa zilizopo ni kampuni ya Vodacom pekee ambayo tayari imeweza kujisajili na DSE na imeanza kuuza hisa zake.
Hatua hiyo ya makampuni hayo ya mawasiliano kuchelewa kujiunga na soko la hisa ndiyo iliyomfanya Mh Rais Magufuli kuiagiza mamlaka ya mawasiliano (TCRA) kuzifuta kampuni zote zitakazokaidi kujisajili katika soko la hisa DSE.
Naunga mkono maagizo hayo Mh .Rais kwa sababu kwanza ni takwa la kisheria kwa kampuni hizo kujiunga na kuuza hisa zao DSE na pili muda wa kuwachekea wakwepa kodi umeshaisha.Mh.Rais Magufuli ana dira ya kuitoa Tanzania kutoka nchi yenye uchumi wa chini kwenda nchi yenye uchumi wa kati na kwa mwendo anaokwenda nao Mh .Rais hilo litawezekana kwa sababu mianya ya ukwepaji kodi imefungwa, nchi itapata fedha nyingi na itajenga uwezo wa ndani wa kupangilia mipango yake sawia.
Hakuna Taifa lolote duniani lililoendelea bila ya kukusanya kodi .
Na Ufunguzi wa kituo cha ukusanyaji wa kodi kwa njia ya kielektroniki ni tiba sahihi ya kujua kila shilingi inayopatikana katika makampuni haya ya mawasiliano .Ni furaha yangu kuona sasa Taifa langu halitoibiwa tena na wafanyabiashara au makampuni yasiyo waaminifu.
Ni wazi kwamba juhudi hizi Mh. Rais Magufuli za ukusanyaji wa kodi na udhibiti wa mianya ya ukwepaji kodi zitakuza uchumi wetu kwa kasi sana na ndio maana nimemtunuku cheo cha FUNDI WA UCHUMI (ECONOMY MAESTRO) kwa sababu anakusanya kodi kwa juhudi kubwa huku anapunguza matumizi yasiyo ya lazima, matokeo yake ni kwamba Taifa litakua na akiba ya kutosha ya fedha za kufanyia maendeleo kwa wananchi na hii ndio itakua TANZANIA MPYA tuitakayo.
MUNGU MBARIKI MH MAGUFULI.
VIVA MAGUFULI VIVA.
Augustino Chiwinga.