Ciprofloxacin.
JF-Expert Member
- Apr 15, 2015
- 1,583
- 2,697
Rais wangu Magufuli, wewe ni mcha Mungu na kwa hiyo una hofu kubwa na Mungu, Na mcha Mungu huwa na moyo wa huruma kwa wanyonge na maskini. Rais wangu, Tanzania ilipata uhuru zaidi ya miaka 50 iliyopita na miaka yote serikali ilikuwepo ikitumikia wananchi hadi sasa hivi, serikali haijawahi kulala iwe usiku au mchana, ipo macho muda wote na miaka yote,serikali ina wataalamu ktk sekta zote na wizara zote, ila pengine haina wataalamu ktk wizara ya ardhi.
Wizara yangu mambo ya ndani ina jeshi la police, mtu akiiba au kuua hukamatwa na akitoroka hutafutwa hadi apatikane.
Wizara ya ardhi ina husika pia na makazi ya watu. Watu wamejenga maeneo yasiyofaa miaka nenda rudi, iwe walijenga kwa makusudi au bahati mbaya ila point ni kwamba serikali ilikuwepo na iliwaona wakijenga ikaridhika na kukaa kimya wakati uwezo wa kuwazuia ilikuwa nao, hizo nyumba hazikuja ghafla kama muujiza, zilijengwa taratibu hadi zikaisha na serikali ikishuhudia.
Leo hii wanapobomolewa watu kila huruma ni kosa lao au la serikali?
Rais wangu hebu jaribu kuvaa uhusika wa msiba wa kubomolewa nyumba, sisi watanzania wengi wetu tuna hali ngumu hata kula yetu ni shida na nyumba tena zibomolewe?
Nakuomba ushiriki huu msiba hatuna pa kwenda.