Mpunilevel
JF-Expert Member
- Sep 14, 2015
- 3,140
- 1,871
Kwanza nikupongeze kwa ujasiri wako unaoonyesha katika uongozi wako.
Maadui zako wamejipanga barabara kuhakikisha unakwama kuwakomboa watanzania maskini.
Nchi hii ilianza kuleta tabaka kubwa kati ya walionacho na wasiokuanacho, kupitia dhulma.
Wachache wakipora raslimali bila huruma na kujitajirisha, huku wengine wakiwa wasindikizaji.
Hili Naona umelifanyia kazi kwa weledi mkubwa sana. Ndo maana madongo ni mengi.
Kupondwa huku kunatoka kundi la watu wachache baadhi, si wote ambao wanamiliki media, na wana nguvu za kiuchumi, na ambao mambo Yao ya shot cut yamekwama. Hivyo Wewe kuwa kikwazo.
Msimamo wako na wasaidizi wako makini ndio mtakao livusha taifa hili toka mikononi mwa wajuvi hawa ambao wanaamini Nchi hii ni mali yao binafsi na bila wao mambo hayendi mbele.
Umeonyesha wazi kuwa utafanya kazi na yeyote yule mwenye nia ya dhati ya kuwatumikia watanzania kwa kuingiza kwenye serikali yako baadhi ya wapinzani.
Naomba kama kuna uwezekano mpe Nafasi Dr Slaa yoyote ile kwa professional yake katika serikali yako ili kuleta sura ya utaifa ndani ya Nchi yetu kwa kufanya kazi na vyama vya upinzani.
Najua wajuvi hili hawalitaki, lakini Dr Slaa ni mchapakazi wa kweli na husimamia anachokiamini. Si wa kuburuzwa kama ulivyo Wewe.
Combination hii italipeleka taifa mbele. Kiuchumi.
Mkuu Rais, hili ni ombi langu kwako, si shuruti.
Naomba kuwasilisha.