Rais Magufuli na wateule wake waonywa

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) kimesema hakitamvumilia kiongozi yoyote wa kisiasa ambaye ambaye atafanya unyanyasaji dhidi ya watumishi wa umma.

Chama hicho kimemtaka Rais John Magufuli kufanya kazi kwa misingi inayolinda na kuheshimu Katiba ya nchi kwa kuwa nchi inaendeshwa sheria, kanuni na taratibu.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Selemani Kikingo, Mwenyekiti wa TALGWU taifa wakati wa ufunguzi wa kikao cha Baraza la wafanyakazi kilichofanyika kitaifa mjini hapa.

“Chama chetu hakina shida na utumbuaji watu wanaoitwa majipu, ambao wanashindwa kutimiza majukumu yao lakini kinachotakiwa ni kuzingatia sheria na taratibu za ajira. Utumbuaji ufanyike kwa watu walio ndani ya mamlaka yake ya uteuzi lakini siyo kwa watumishi ambao wameajiriwa kwa kuzingatia sheria na taratibu za ajira,” amesema.

Amedai kuwa, kwa sasa umeibuka mtindo wa baadhi ya wanasiasa kuwanyanyasa wafanyakazi ambao wameajiriwa kwa taratibu, sheria na kanuni za kazi.

“Huu mchezo wa viongozi wa kisiasa kuwanyanyasa watumishi wa serikali za mitaa unasababisha wafanyakazi kufanya kazi kwa hofu na wakati mwingine kushindwa kufanya kazi kwa kiwango kinachotakiwa.

“Hatutaweza kuwavumilia viongozi hao ambao wamekuwa wakiingilia sheria na taratibu za utumishi kwa kuwasimamisha kazi au kuwapa adhabu ambazo haziwahusu, ni vyema kila mmoja akaheshimu mipaka ya kila mtu katika utendaji wa kazi,” amesema Kikingo.

Kumekuwa na matukio mbalimbali ya viongozi wa kisiasa wakiwemo wakuu wa wilaya, mikoa na wakurugenzi kufanya unyanyasaji dhidi ya watumishi wa umma likiwemo tukio la mwalimu mmoja kuamuriwa kudeki darasa mbele ya wanafunzi.

Wateule hao muhimu wa Rais Magufuli pia wamekuwa wakikingiwa kifua na mamlaka yao ya uteuzi kwani hakuna hatua zozote kali za kinidhamu walizochukuliwa mpaka sasa.
 
Ni yupi ametumbuliwa na JPM huku akiwa hayupo katika mamlaka yake ya uteuzi? Maana tusipende tu kuongea ili tuonekane tunajua kukosoa.
 
Boss hanumiwi wala kuonywa.
 
Yote ayo yanasababishwa nakatiba mbovu atuwezi kufika kwa style hii ata angekuwa maraika kama katiba aitalekebishwa nae hata weza tunachokisubiri nchi ifikie kupata majanga makubwa (Vita vya wenyewe)

Miaka kumi kupita bila maendeleo yoyote tutakumbuka kuwa katiba ninini
 
yani saizi nchi ni Kama inaendeshwa kihuni.
kila MTU anakuja na lake.
 
Tarehe 9/1/2017ndani ya manispaa ya Musoma, DC aliamuru mkuu wa shule ya secondary ya Kiara kwenda rumande kwa shule hiyo kukosa Ratiba.
 
Back
Top Bottom