Rais Magufuli na Rais wa Vietnam

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,735
59,154
Ikulu sasa hivi JPM yupo na rais wa vietnam ...
Magufuli anatoa speech kwa english na kwa kiswahili..anasema kuwa vietnam uzalishaji wao mwingi walianza kidogo kidogo.. ila sasa hivi wako mbali sana...
Tanzania tuna malighafi nyingi sana ila hatuzalishi kitu ni kama tumelogwa...vietnam inaingia mara tatu kwa Tanzani ila uchumi wao unapanda ila wa kwetu majipu wanaumaliza....
...anasema kuwa kaalikwa kwenda kule vietnam na yeye kasema kuwa ataenda kule ili aweze kujifunza ili kauli yake ya hapa kazi tu iwezi kutekelezeka kwa ufisadi..
sifa kuu ya vietnam ni kuthubutu na kuweza kusimamia mipango yake
...vietnam imekuwa miongoni mwa nchi chache duniani zinazongoza kwa uzalishaji wa mchele
,,...wanavuna mchele mara tatu kwa mwaka wakat Tz wanavuna mara moja...
vietnam wanaongoza duniani kwa uzalishaji wa pilipili manga...
SASA HIVI RAIS WA VIETNAM ANAONGEA ........
...anaonea kivietnam..
anashukuru kwa ukarimu hospitality ya watz...
anasema bila kujali Umbali wa kijiografia kati ya nchi mbili ila TZ ni moja ya rafiki wa kwanza wa kidiplomasia wa vietnam.
..tumekuwa na mazungumzo mazuri na rais JPM kwenye sekta ya viwanda kilimo etc..
...
pia tumeongelea amani za mataifa yenu na yanayotuzunguka..kuwa matatizo yawe yanapatiwa ufumbuzi kwa njia za amani..
..naamini kuwa urafiki wetu utaongezeka na kuimarika sana..na nimemwalika rais Magufuli aje vietnam yeye na First lady.
Tanzania ndio nchi ya kwanza kuwaunga mkono wakati vietam ilipokuwa na matatizo ya kivita..
wamemaliza sasa anaenda Lumumba kukutana na JK
 
SASA HIVI RAIS WA VIETNAM ANAONGEA ........
...anaongea kivietnam..

Haya wale akina yakhe mnaodharau lugha zenu za kiswahili mpo? Na wale wasomi koko mnaong`ang`aniza kuwa Raisi wa nchi lazima ajue kiingereza mpo? Mzee katandika kivietnam lugha ambayo si ya kimataifa na haoni shida wala aibu.Nyie mnaoona aibu kutojua kiingereza leo na nyie mmpata jibu wako maraisi wasiojua kiingereza nchi nyingine pia.

Leo mnaojua kiingereza lugha ya mkoloni wa kiingereza mmeaibika.Mkamwambia na Malkia kuwa leo Raisi wa vietnam katuadhiri na kiingereza chetu mchana kweupe
 
nadhani ni vyema kama Rais wetu JPM angezungumza kiswahili tu peke yake kama mwenzake alivyoongea ki Vietnam peke yake , kwanza inaonyesha uzalendo kwa nchi yetu .
 
Hayo majipu yaliyodumaza uchumi ni yapi? JPM achunge sana kinywa chake asije aibika mbeleni.....
 
Back
Top Bottom