Rais Magufuli na maana nyingi za usafi siku ya uhuru

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,487
13,612
Kuna watu ambao walishazoea kutengeneza fedha ndefu kupitia sherehe za Uhuru na Mei Mosi. Kupitia matukio mengi yanayokuwa yakiendelea ndani ya siku hizo. Lakini rais Magufuli ameingia kwenye uongozi na kujaribu kuwakumbusha watanzania umuhimu wa jamii yenye mamlaka kuwatumikia walio wengi ambao vipato vyao ni vidogo. Badala ya watu kuserebuka tarehe 9 desemba, kila moja ashike fagio na kwenda kusafisha eneo analoishi au kufanyia biashara. Agizo la kila mwezi kufanyika usafi ndani ya miji yetu, lipo na linaendelea kutekelezwa.

Majuzi wakati rais Magufuli akiwa na rais Museveni wakati wakiongelea bomba la mafuta kutoka Tanga mpaka Uganda, rais ameongelea "spirit of reciprocation". Yaani binadamu hupokea kutoka kwa mwingine katika kiwango kile kile cha utoaji wake kwa wengine. Ni falsafa yenye mashiko kwenye imani za kidini. Na inapotazamwa kwa undani ni falsafa ambayo inawakumbusha wasomi, kujishusha na kuwa watumishi wa walio wengi ili nao wao waweze kushushiwa neema kutoka kwa Mungu.

Rais anatukumbusha kuachana na ufahari na kupenda kujitukuza wakati tunapoadhimisha sherehe za Uhuru, haswa kwa kusafisha mazingira yetu na kuitumia fedha ambayo tunaiokoa kwa kukwepa kufanya sherehe, kwa ajili ya ujenzi wa barabara yenye kutumiwa na walio wengi. Na wakati huo huo "spirit of reciprocation" anayoizungumzia ni ukumbusho mwingine juu ya umuhimu wa viongozi kuwa watumishi wa umma kwa matarajio ya kile wakifanyacho kuweza kukumbukwa na Mungu.

Awamu ya tano inaongozwa na wanadamu, ambao wanafanya makosa mengi na wataendelea kukosea kila kukicha, lakini angalau lipo somo la utumishi kwa faida ya walio wengi. Awamu ya nne na zile za nyuma, watanzania tulikuwa tumezama kwenye ubwana na utwana, Hatukuona aibu kujenga matabaka makubwa, huku tabaka la wasomi likigeuka bila ya aibu, kuwa ni watu wenye wajibu wa kutumikiwa. Lakini awamu hii inatukumbusha kwamba mnyonge anayo haki yake kama yule msomi mwenye cheo fulani.

Lakini ni ukweli pia kuwa Tanzania yenye neema bado ina miaka mingi mpaka iweze kufikiwa.
 
mkuu tutafika tu Mimi naamini tatizo kubwa la inchi ni uongozi ulioshindwa kuelewa umaskini wetu unatokana na nini. Lakini kwa sasa angalua mh. magu ameanza kwa kutambua na kufuta matumizi ya fedha za uma yasiyo ya lazima na kubana mianya ya ukwepaji kodi. Akimaliza hapo ataenda kwenye kupata dira na mwelekeo wa serikali yake kwa sababu sasa hivi bado ana wenge.
 
Tanzania yenye neema Na baraka tele itafikiwa endapo tu Chama Cha Mapinduzi kitapum,ika
 
Back
Top Bottom