Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Tanzania inatarajia kuanza ujenzi wa kiwanda kikubwa cha kuzalisha mbolea kabla ya mwisho wa mwaka huu wa 2016 katika wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi.
Kiwanda hicho ambacho kitatumia rasilimali ya gesi asili na miamba ya matumbawe (coral reefs) iliyopo wilayani Kilwa, kitajengwa kwa ubia kati ya Tanzania na nchi za Denmark, Ujerumani na Pakistani na kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 3,800 za mbolea kwa siku.
Balozi wa Ujerumani hapa nchini Mhe. Egon Kochanke na Balozi wa Denmark hapa nchini Mheshimiwa Eina Hebogrd waliokutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 19 Mei, Ikulu Jijini Dar es salaam, wamesema kiwanda hicho kikubwa barani Afrika kitakuwa na uwezo wa kuzalisha mbolea nyingi itakayotosheleza mahitaji ya wakulima wa Tanzania na nyingine kuuzwa nje ya nchi.
Kiwanda hicho kinatarajiwa kuzalisha ajira zaidi ya 5,000 na uwekezaji wake utagharimu dola za kimarekani Bilioni 3.
Pamoja na kuwahakikishia kuimarishwa kwa uhusiano na ushirikiano kati ya serikali yake na nchi za Ujerumani na Denmark, Rais Magufuli amewaahidi mabalozi wanaowakilisha nchi hizo hapa nchini kuwa serikali yake ya awamu ya tano itatoa ushirikiano wa kutosha kuharakisha utekelezaji wa mradi huu mkubwa na amependekeza mchakato wa ujenzi uanze na kukamilishwa haraka.
Aidha, Rais Magufuli na Mabalozi hao wamezungumzia maeneo mengine ya ushirikiano kati ya nchi hizo na Tanzania ikiwemo kukuza biashara na uwekezaji, kuendeleza bandari za Tanzania na kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa.
Wakati huo huo, Rais Magufuli amezungumza na Balozi wa Uturuki hapa nchini Mhe. Yasemin Eralp ambapo pamoja na kukubaliana kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano baina ya nchi hizi mbili, ameikaribisha nchi hiyo kuwekeza hapa Tanzania katika uzalishaji wa dawa za kutibu binadamu na kujenga viwanda vya kuzalisha bidhaa mbalimbali kutokana na nchi hiyo kubobea katika maeneo yao.
Katika hatua nyingine, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya nchi za Afrika, kusini mwa Jangwa la Sahara (SADC) Dkt. Stergomena Tax na kuzungumzia hali ya ulinzi na usalama katika Jumuiya hiyo.
Rais Magufuli ambaye kuanzia mwezi Agosti mwaka huu 2016 atakuwa mwenyekiti wa Taasisi ya Ulinzi, Usalama na Siasa iliyo chini ya SADC amesema pamoja na majukumu mengine ya Jumuiya hiyo ni muhimu kwa sasa kujikita zaidi katika uchumi na maendeleo ya wananchi hususani ujenzi wa viwanda.
Kwa upande wake Dkt. Stergomena Tax ameungana na Rais Magufuli kuwasihi watanzania na wanajumuiya wote wa SADC kuchangamkia fursa za kiuchumi zilizopo katika kilimo, masoko, viwanda na ajira ndani na nje ya jumuiya.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
19 Mei, 2016