mwarabu wa dubai
JF-Expert Member
- Nov 29, 2015
- 317
- 305
Siungi mkono hoja yako imekaa kichama na kisiasa zaidi all in all acha siku ziende Mungu wa Israel yupo.Leo sitaki unafiki juu ya hili na naomba niwe mtetezi wa Mheshimiwa Rais Dkt. JPM juu ya lililotokea na simlazimishi yoyote kukubaliana nami.
Jamani tukumbukeni kuwa Urais ni Taasisi na siyo Magufuli kama Magufuli. Hivi inaingia akilini kweli kuwa ni Yeye ndiye aliyewaonea huruma Wanafunzi wa UDSM mwaka jana ndipo akaona awajengee Hostels zao na ambazo kiukweli zimemaliza tena kwa Kiwango kikubwa tu na ratiba yake ya uzinduzi ilishapangwa muda mrefu huku maandalizi yote ya Kiitifaki yakiwa yamekamilika halafu ifike kweli siku ya kuyazindua asiwepo?
Pili tusisahau pia kuwa ujenzi ule wa zile Hostels ni ' turufu ' kubwa sana ya Mheshimiwa Rais, Serikali yake na hata Chama chake cha CCM hasa ukizingatia kuwa aliowajengea ni ' Intellectuals ' wa baadae wa nchi na ambao pengine hata kimsingi wanaweza kuwa ' Mabalozi ' wake wazuri tu huko ' Makwao ' katika kumwombea ' Kura ' za kurudi awamu yake ya pili na ya mwisho ya Uongozi au Utawala wake.
Tatu tusishau kuwa msiba wa hawa Askari wetu umetokea ghafla tu juzi tena usiku kitu ambacho nina uhakika wa ' Kiprotokali ' kuwa tayari ratiba zote za Rais za kuwepo leo pale katika ' Uzinduzi ' wa zile Hostels zilikuwa zimepangwa kiasi kwamba ingekuwa ni ngumu mno kuzi ' adjust ' accordingly ili tu nae aweze ' kuhudhuria ' mazishi ya Askari wetu kutokana na ' timing ' na ' mazingira ' yake.
Hata hivyo kwenda kwa Waziri husika wa Wizara kuhudhuria hapo mazishini siyo jambo baya sana hasa ukizingatia kuwa uwepo wa Waziri Mwigulu Nchemba pale ni ' uwakilishi ' mzuri tu wa Mheshimiwa Rais wa JMT Dkt. Magufuli na huwezi jua anaweza Rais kama Rais asiwepo pale ILA ' rambi rambi ' zake za hali na mali zikawakilishwa vizuri sana kwa ' Wafiwa ' namaanisha wana Familia na kisiharibike kitu. Naamini kabisa wale wenye angalau a,b,c's za Protocols watakuwa wamenielewa vizuri sana.
Ukishakuwa katika Taasisi ya Urais ni lazima pia ujue kucheza na public psychology lakini pia mjue jinsi gani mtaweza kumsaidia Bosi wenu ambaye ni Rais ili aweze kuzichanga vizuri ' Karata ' zake kusudi azidi kuleta imani kwa Wananchi hasa wale wenye shida na mahitaji ya lazima hivyo hapa ndipo ile ' Principle ' ya Kiuchumi ya ' Opportunity Cost ' ndipo hutumika hasa kwamba Rais asiende katika ' Uzinduzi ' wa Hostels ambazo zitawafaidisha Wasomi wengi na kumfanya azidi kukubalika na wengi na aende ' Mazikoni ' tu kwa Askari nane ( 8 ) ambao Vifo vyao vimeshaleta ' taharuki ' katika Jamii na kuleta ' chuki ' dhidi ya Serikali yake. Hapa ' obvious ' Mtu anayejua ' kucheza ' vizuri na Siasa ataamua atume tu ' mwakilishi ' katika maziko ya Askari ila yeye ataenda kuzindua Hostels ili azidi kujiaminisha kwa Wasomi ambao ni wengi kuliko hata hao Askari nane ( 8 ) waliofariki.
Urais ni zaidi ya Magufuli jamani na si vibaya sasa tukaanza kujifunza maana hasa ya Taasisi ya Urais na dhana nzima ya Protokali hasa kwa Viongozi wakubwa wa mfano wake kuliko kuja tu ' mitandaoni ' kulalamika na kulaumu wakati kumbe hata bado hatujajiridhisha vizuri kwa mambo mengine.
Yangu ni hayo tu Mkuu.