Rais Magufuli kwa hili uliloongea kwa Dangote nakuomba sana uwe unachagua maneno!

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,593
36,010
Rais Magufuli mbele ya Aliko Dangote amewashambulia vilivyo wafanyakazi ambao kimsingi ndiyo wanaomuwakilisha Dangote hapa Tanzania wakati yeye akisaka uwekezaji duniani.

Rais akiituhumu kampuni ya usambazaji gesi ya AQUA kuwa ni madalali walioingia kati ya TPDC na kampuni ya Dangote ili wamsambazie gesi amejikuta akianza kuwashambulia wafanyakazi wa kampuni ya Dangote eti wanafanya sabotage kwa Dangote ili kuuwa kampuni yake.

Rais anaongea huku kweli akiwa hana data za kutosha kwani ameishia tu kuongea.

"Mheshimiwa Dangote, inawezekana hawa wafanyakazi uliowaweka hapa wanafanya sabotage ili kukuangamiza. Tena inawezekana kuwa wanatumiwa na viwanda vingine hivyo naomba uangalie watu wako" hiyo imekuwa ni sehemu ya hotuba ya rais Magufuli leo.

Kwa kweli rais haelewi kuwa ni kiasi gani atakuwa ameacha sintofahamu kubwa na kivumbi cha aina yake baada ya yeye kuondoka. Pengine Dangote akawafukuza tu wafanyakazi wake kwa kuwa kauli ya rais huwa ni nzito. Mbaya zaidi huenda Dangote haelewi vizuri hulka za rais Magufuli.

Ukweli ni kuwa kumualika rais Magufuli kwenye kampuni au mradi wako ni lazima ujue kuwa kutakuwa na hasara kubwa kuliko faida.

Mheshimiwa rais amekuwa akituhumu hadharani bila kujua madhara halisi ya tuhuma anazotoa. Tuhuma nyingi ya hizo ikiwa ni hisia tu.

Hivi kweli CEO muwakilishi wa kampuni anaweza kuwa sehemu ya uhujumu kampuni tena kwa kushirikiana na kampuni nyingine? Mbaya zaidi rais Magufuli ameongea bila kuwa na data yoyote ile.

Kuna wamiliki kadhaa wa viwanda ambao nawafahamu hulka zao na pengine siku rais Magufuli akienda kutembelea hivyo viwanda na kisha akaongea alichoongea leo basi atakuwa amewasha moto mkubwa sana ndani ya hivyo viwanda. Ni kweli kuwa kunaweza kutokea uzembe katika utendaji na hilo likabaki kuwa kama uzembe lakini kitendo cha kusema kuwa kiongozi wa kitengo au kampuni anashirikiana na kampuni nyingine kuua kampuni yake bila kuwa na ushahidi (nasema hivyo kwa kuwa rais ametumia neno "pengine hata" kwenye utangulizi wa tuhuma zake) ni tuhuma ya juu sana na inayoweza kuchanganya utendaji na kuzoroteshea mbali maendeleo ya kampuni.

Hata hivyo nimefurahi pale ambapo rais Magufuli muda wote alipokuwa akimtaja Dangote ametumia maneno "Mheshimiwa Dangote"
 
Rais Magufuli mbele ya Aliko Dangote amewashambulia vilivyo wafanyakazi ambao kimsingi ndiyo wanaomuwakilisha hapa Tanzania wakati yeye akisaka uwekezaji duniani.

Rais akiituhumu kampuni ya usambazaji gesi ya AQUA kuwa ni madalali walioingia kati ya TPDC na kampuni ya Dangote ili wamsambazie gesi amejikuta akianza kuwashambulia wafanyakazi wa kampuni ya Dangote eti wanafanya sabotage kwa Dangote ili kuuwa kampuni yake.

Rais anaongea huku kweli akiwa hana data za kutosha kwani ameishia tu kuongea.

"Ndugu Dangote, inawezekana hawa wafanyakazi uliowaweka hapa wanafanya sabotage ili kukuangamiza. Tena inawezekana kuwa wanatumiwa na viwanda vingine hivyo naomba uangalie watu wako" hiyo imekuwa ni sehemu ya hotuba ya rais Magufuli leo.

Kwa kweli rais haelewi kuwa ni kiasi gani atakuwa ameacha sintofahamu kubwa baada ya yeye kuondoka. Pengine Dangote akawafukuza tu wafanyakazi wake kwa kuwa kauli ya rais huwa ni nzito. Mbaya zaidi huenda Dangote haelewi vizuri hulka za rais Magufuli.

Ukweli ni kuwa kumualika rais kwenye kampuni au mradi wako ni lazima ujue kuwa kutakuwa na hasara kubwa kuliko faida.

Hivi kweli CEO muwakilishi wa kampuni anaweza kuwa sehemu ya uhujumu kampuni tena kwa kushirikiana na kampuni nyingine? Mbaya zaidi rais Magufuli ameongea bila kuwa na data yoyote ile.
Wewe hujui kinachoendelea Dangote kaa kimya huna point
 
Dangote ni mfanyabiashara na mwekezaji mkubwa sana. Katika biashara na uwekezaji wake, ameishakutana na ma Rais au viongozi wa kila aina - wezi, wala rushwa, waadilifu, madikteta, wapenda sifa, wajinga, wapumbavu, werevu, waropokaji nk
Anajua ku deal na kila aina ili mradi biashara zake ziende vizuri.
 
Rais Magufuli mbele ya Aliko Dangote amewashambulia vilivyo wafanyakazi ambao kimsingi ndiyo wanaomuwakilisha hapa Tanzania wakati yeye akisaka uwekezaji duniani.

Rais akiituhumu kampuni ya usambazaji gesi ya AQUA kuwa ni madalali walioingia kati ya TPDC na kampuni ya Dangote ili wamsambazie gesi amejikuta akianza kuwashambulia wafanyakazi wa kampuni ya Dangote eti wanafanya sabotage kwa Dangote ili kuuwa kampuni yake.

Rais anaongea huku kweli akiwa hana data za kutosha kwani ameishia tu kuongea.

"Ndugu Dangote, inawezekana hawa wafanyakazi uliowaweka hapa wanafanya sabotage ili kukuangamiza. Tena inawezekana kuwa wanatumiwa na viwanda vingine hivyo naomba uangalie watu wako" hiyo imekuwa ni sehemu ya hotuba ya rais Magufuli leo.

Kwa kweli rais haelewi kuwa ni kiasi gani atakuwa ameacha sintofahamu kubwa baada ya yeye kuondoka. Pengine Dangote akawafukuza tu wafanyakazi wake kwa kuwa kauli ya rais huwa ni nzito. Mbaya zaidi huenda Dangote haelewi vizuri hulka za rais Magufuli.

Ukweli ni kuwa kumualika rais kwenye kampuni au mradi wako ni lazima ujue kuwa kutakuwa na hasara kubwa kuliko faida.

Hivi kweli CEO muwakilishi wa kampuni anaweza kuwa sehemu ya uhujumu kampuni tena kwa kushirikiana na kampuni nyingine? Mbaya zaidi rais Magufuli ameongea bila kuwa na data yoyote ile.
Kwanini ikiwezekane? hawa make CEO ndio wanamiliki kampuni ndogo mdogo zinazofanya biashara na waajiri wao.Mfano,Mbowe ndiye muuzaji wa magari chadema
 
Kuna wakati inabidi ukae kimya uangalie tu kwa kweli! Maana huu ufitin ni mtihan mkubwa sana kwa mzee wetu
 
Hapa Dangote Ataendelea na wafanyakazi wake walewale kwasababu ni smart na hakurupuki..

Ndiyo utajua nani ana uelewa mzuri wa biashara kuliko mwenzie..
 
Rais Magufuli mbele ya Aliko Dangote amewashambulia vilivyo wafanyakazi ambao kimsingi ndiyo wanaomuwakilisha hapa Tanzania wakati yeye
Rais akiituhumu kampuni ya usambazaji gesi ya AQUA kuwa ni madalali walioingia kati ya TPDC na kampuni ya Dangote ili wamsambazie gesi amejikuta akianza kuwashambulia wafanyakazi wa kampuni ya Dangote eti wanafanya sabotage kwa Dangote ili kuuwa kampuni yake.

Rais anaongea huku kweli akiwa hana data za kutosha kwani ameishia tu kuongea.

"Ndugu Dangote, inawezekana hawa wafanyakazi uliowaweka hapa wanafanya sabotage ili kukuangamiza. Tena inawezekana kuwa wanatumiwa na viwanda vingine hivyo naomba uangalie watu wako" hiyo imekuwa ni sehemu ya hotuba ya rais Magufuli leo.

Kwa kweli rais haelewi kuwa ni kiasi gani atakuwa ameacha sintofahamu kubwa baada ya yeye kuondoka. Pengine Dangote akawafukuza tu wafanyakazi wake kwa kuwa kauli ya rais huwa ni nzito. Mbaya zaidi huenda Dangote haelewi vizuri hulka za rais Magufuli.

Ukweli ni kuwa kumualika rais kwenye kampuni au mradi wako ni lazima ujue kuwa kutakuwa na hasara kubwa kuliko faida.

Hivi kweli CEO muwakilishi wa kampuni anaweza kuwa sehemu ya uhujumu kampuni tena kwa kushirikiana na kampuni nyingine? Mbaya zaidi rais Magufuli ameongea bila kuwa na data yoyote ile.[/QUOTE
You can wait for hundreds years .but you will never hear a good speach from him
 
Dangote
f60b7426b80b4c1ae8e1921a46ca2d84.jpg
 
Back
Top Bottom